NACTE kwanini mnawaluhusu wamiliki wa A3 company ltd kuwadhulumu walimu wa Kigamboni City College na Dodoma City college?

HakiWhisleblower

New Member
Aug 13, 2021
2
1
A3 Company Ltd ni wamiliki wa City college Mikwambe, Kigamboni City college na Dodoma city college. Hawa wamiliki wa A3 Company Ltd wako bize kufungua vyuo vipya Arusha na Mwanza kwa idhini ya NACTE huku walimu wa Kigamboni City college na Dodoma City college hawajarlipwa mshahara ya mwezi wa saba.

Hii kama sio ufujaji wa hela za kuendeshea hizi vyuo ni nini? TAKUKURU tunaomba muwachunguze hawa wamiliki wa A3 Company ltd pesa za kufungua vyuo vipya Arusha na Mwanza wanatoa wapi kama sio kufuja pesa za Kigamboni City college na Dodoma City college huku walimu wenye familia na mahitaji mengine wakiendelea kuteseka?

Chuo kama Kigamboni City College ina wanafunzi zaidi ya 2000 na makusanyo ya mwaka no zaidi ya bilioni mbili shida iko mahali gani?

Kingine cha kujiuliza, je, walimu wataweza kweli kusimamia mitihani ya mwisho wa muhula inayoanza Jumatatu ijayo wakiwa na njaa na familia zao zikiwa kwenye mateso?

Wizara ya Afya angalieni hili jambo kwa umakini elimu ya kada ya afya inahujumiwa.
 
Back
Top Bottom