NACTE kuweni macho na elimu ya nchi hii

KALEBE

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
773
338
ni takribani mwezi mmoja na wiki kadhaa zimepita toka vyuo vya ualimu tanzania kuhama kutoka katika mtaala wa content based curriculum kwenda kwenye competence based curriculum, kwa mujibu wa baraza la taifa la elimu ya ufundi(NACTE) mtaala uliokuwepo ulikuwa hauwajengei walimu umahiri baada ya kuhitimu mafunzo yao na hii imekuwa ikisababisha kiwango cha ufaulu katika shule za msingi na sekondali kushuka mwaka hadi mwaka na kwa sababu hiyo baraza la taifa la elimu ya ufundi kuanzisha mtaala wa umahili katika vyuo vyote vya ualimu tanzania bara. lakini pia kutoa fursa pana kwa walimu wa shule za msingi kupata nafasi ya kujiendeleza katika masomo yao kwani hapo awali nafasi ilikuwa finyu sana kwao jambo ambalo wengi wao walikuwa wanaishia ngazi ya cheti hadi kustaafu kutokana na mazingira kutokuwa rafiki kwao. binafsi sina shida na haya mabadiliko kwa upande wangu naona ya kuwa nchi ilikuwa imechelewa kufanya mabadilko haya hasa ikizingatiwa ya kuwa nchi nyingi katika bara letu la afrika na kwingineko wanatumia mtaala unaowajengea wahitimu wao ujuzi. lakini pia kwa kuwa tanzania tunategemea kuingia katika shirikisho la pamoja la nchi za afrika mashariki na kati basi ni wakati mwafaka kwetu sisi kuwa katika sehemu hii ili tuweze kutoa nafasi ya ushindani na wenzetu katika shirikisho hilo.
tatizo langu na hili baraza la taifa la elimu ya ufundi katika vyuo hivi vya ualimu ni kuwa walisema watakuja kutoa maelekezo kwa wakufunzi ya namna ya kutekeleza mafunzo haya kwani kwa wakufunzi walio wengi jambo hili kwao ni jipya ikizingatiwa ya kuwa walikuwa wanafundisha mtaala wa content based kwa muda mrefu lakini hadi sasa NACTE hawajawahi kufika katika chuo chochote kwa ajili ya kutoa maelekezo ya awali.
 
Back
Top Bottom