kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,636
- 7,005
Mitihani ya vyuo vinavyosimamiwa na NACTE husimamiwa na wasimamizi wa nje wanaotoka vyuo tofauti.Hili ni jambo zuri.Ila zipo changamoto zilizotengenezwa maksudi ama kwa kutokujali zinazofanya usimamizi huu uwe duni kabisa.
Kwanza kitendo cha kupanga msimamizi yule yule katika kituo kimoja kila mwaka.
Jambo hili lina madhara makubwa na athari kwa ubora kwani baadhi wamekuwa hawana maadili kiasi kwamba wanashirikiana na wamiliki kusaidia wanafunzi ili wafaulu.Kuna mashaka makubwa kuwa wanachukua mlungula na hakuna ufuatiliaji wa karibu kwenye suala hili.
Baadhi kutaka kushiriki ngono na baadhi ya watoto wa kike na wanaokataa wanatishwa kwani kila mwaka anatarajiwa kurudishwa katika chuo kile kile kuwa msimamizi.
Pamoja na mitihani kuwekewa utaratibu wa udhibiti lakini upo uwezekano wa baadhi ya vyuo kuwa huwa wanapata mitihani au baadhi ya maswali ya mitihani hiyo.
Je kwa nini usiwekwe utaratibu wa udhibiti kama mitihani ya NECTA?
Mimi nawapa tahadhari tu maana tayari tumeanza kuona dalili mbaya ambazo zinahitaji hatua za umakini zichukuliwe.
Si vema kufanya kazi kwa mazoea,au mnaweza kuleta sintofahamu isiyo ya lazima.
Sent using Jamii Forums mobile app