NACTE komesheni utapeli unaofanywa na Chuo cha Ualimu Northern Highlands Moshi

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Niwaombe Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kukomesha utapeli unaofanywa na Chuo cha Ualimu cha Northern Highlands kilichopo mjini moshi mkoani Kilimanjaro pamoja na vyuo vingine jamii ya hiyo.

Chuo hicho kinachomilikiwa na bwana Henry Mallya, kimekuwa kikiwadahili wanafunzi wasiokuwa na sifa za kujiunga na chuo na kuchukua pesa zao ambazo ni ada kwa miaka miwili wakisoma kozi ya English Medium lakini kozi hiyo ikiwa haijasajliwa na NACTE,na mwisho wa siku wanafunzi wanafukuzwa chuoni eti kisa hawana sifa za kufanya mtihani wao wa mwisho ambao unatambuliwa na NACTE.

Sasa huu kama siyo utapeli ni nini:,yaani mtoto wa mtu unakaa naye chuoni anakulipa pesa unaweka mfukoni na mwisho wa siku unamwambia hana sifa?,nadhani NACTE mtaupata huu ujumbe na ikiwezekana mchukue hatua kali na kwa upande wa wazazi wa wanafunzi waliotapeliwa mna haki ya kwenda mahakamani kudai haki ya watoto wenu maana ninyi ndiyo mliokuwa mkilipa ada na mahitaji mengine kwa watoto wenu.

Kwa leo naomba niishie hapa,comment ziwe fupi fupi kuokoa muda
 
Unawezaje kuchukua pesa ya mtu Hali ya kuwa unajua hujakizi vigezo vya kutoa huduma staiki hili jambo litazamwe kwa mamlaka husika
 
Back
Top Bottom