NACTE: IFM, CBE na Arusha Tech siyo Vyuo Vikuu bali ni Taasisi za Elimu

Engineer wa CBE

Nafurahi umeandika neno Engineer kama inavyotakiwa,nawapa tu moyo watoto wa cbe...Mimi nimesoma zangu mbele huko...Sidhani kama Cbe wanasolve fourier series na advanced calculus au differential equations au laplace equations
 
That is well known. Wasiyojua hilo hawana hata interest na hayo maelezo, so hakuna haja ya kufafanua.
 
Ilitakiwa atuelezee sifa na tofauti kati ya chuo kikuu na Taasisi ya elimu

Sidhani kama Kuna tofauti ya kiubora maana ametoa mfano wa Taasisi inayotoa cheti mpaka masters so naona bado hajaeleweka naona ameeleza kiushabiki zaidi kuliko uhalisia
Hata Universities wanatoa astashahada, stashabada na kuendelea
 
Mkuu, chuo kutoa degree sio kigezo kua chuo kikuu. Yuko sawa kabisa hivyo sio vyuo vikuu bali ni vyuo vya kati.

Kwa kuelewa zaidi tafuta guide books za tcu ili uongeze maarifa.

Respect...
Kwahiyo hata vikitoa elimu Hadi ngazi ya PhD bado vitaitwa vyuo vya kati au?
 
Halaf mim kuna siku nilijiulizaga hili swali
Ifm na comp sci wapi na wapi😄😄😄
Itakua bodi imekaa ikaona itafute vyanzo vingine vya mapato 😄😄😄
Shangaa unakuta kijana anatoka IFM au DIT ni programmer mzuri ( wapo wengi tu wameajiriwa na makampuni ya IT) wanakuacha wewe na raba zako za aadidas + flana za Arsenal au Manchester United hapo Unapopaita University of Africa
 
Tazama rankings ya vyuo vikuu bora duniani.

Utakutana na MIT, California institute of technology, Georgia institute of technology.

Hapo huwa sielewi kwa nini wanaingiza taasisi ziwemo katika 10 bora ya vyuo vikuu duniani
Elimu ya kiwango cha chuo kikuu.
 
Wale Mliosoma IFm,Cbe na Arusha Tech Pokeeni Hii Taarifa Wakuu.

----
Dkt. Geofey Oleke - Mkurugenzi wa Udhibiti, Tathmini na Ufuatiliaji NACTE amesema haya

Watu huwa wanachanganya kati ya NECTA Na NACTE kwa sababu ya maneno kushabihiana NACTE ni baraza la Taifa la elimu ya Ufundi wakati NECTA ni baraza la Mitihani la Taifa. Sisi kazi yetu ni kusajili vyuo na kuangalia ubora katika vyuo vya elimu ya kati, ni vyuo ambayo sio vyuo vikuu ambayo vinatoa ngazi ya cheti, diploma, degree mpaka degree za juu.

Vyuo ambayo sio vyuo Vikuu ni IFM, CBE, Arusha Tech., hizi ni taasisi za elimu zinatoa ngazi ya cheti hadi Masters vyote vipo chini na NACTE.

Vyuo vikuu vyote vipo chini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kama UDSM, UDOM na vingine.

Tupo kwenye msimu wa Udahili na kawaida kabla ya wanafunzi kwenye vyuoni kuripoti wanafanyiwa uhakiki.

Wanafanya maombi kwenye vyuo vyao halafu baadaye vyuo vinaleta majina ya wanafunzi wote wanaotakiwa kusajiliwa ili sifa zao zifanyiwe uhakiki kwa mfano unataka kusoma program ya afya kumbe hauna vigezo vya kusoma kazi yetu kubwa kama baraza ni kuangalia ubora tumeshafanya kwenye program ya afya kwenye vyuo vya Serikali kwenye vyuo vingine mchakato unaendelea umeanza tarehe 5 kuangalia sifa za wanafunzi vyuo vyote vimeleta majina ya wanafunzi wao. Hii kazi itakwenda mpaka tarehe 15 September

Ni kwamba hii ilikuwa haieleweki? Tangu miaka ya 70 vilipoanzishwa ilikuwa ikujulikana hivyo, IFM inaitwa Chuo tu (Institute) na sio Chuo Kikuu (university)
 
Halaf mim kuna siku nilijiulizaga hili swali
Ifm na comp sci wapi na wapi😄😄😄
Itakua bodi imekaa ikaona itafute vyanzo vingine vya mapato 😄😄😄
True bro wanatafutaga kozi nyingne ambazo hazina hata uhusiano ili wapate fedha tuu, hawafwati protocol
 
Mkuu, chuo kutoa degree sio kigezo kua chuo kikuu. Yuko sawa kabisa hivyo sio vyuo vikuu bali ni vyuo vya kati.

Kwa kuelewa zaidi tafuta guide books za tcu ili uongeze maarifa.

Respect...

Nakubaliana kuwa kweli CBE au IFM nk vyote vilivyoko chini ya NACTE siyo vyuo vikuu bali ni vyuo vya Elimu ya Juu ambayo hupatikana pia vyuo vikuu. Muumganiko wa Taasisi nyingi na vyuo vingi na Faculty huunda Chuo Kikuu ambacho utakuta kuna Elimu, Uhandisi, Udaktari, Lugha, nk. Wakati Taaisisi za Elimu ya juu ni mahsusi kwa fani fulani kama ilivyo DIT au Arusha Tech ni mahiri kwa Uhandisi sawa na CoET ambayo ni Chuo au Taasisi inayounda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa hiyo Chuo Kikuu ni Mkusanyiko wa Taasisi au Colleges kwa fani mbalimbali kwa pamoja na huwa na uwezo wa kutoa elimu kuanzia Diploma hadi PhD, wakati taasisi nyigi za Elimu huishia mara nyingi kiwango cha Uzamili(Masters Degree).
Kwa sasa kuna TCU na NACTE, zamani ilikua ni Higher Education Accreditation Council kwa watu wote bila kujali aina ya Chuo.
 
Muhimu ni OUTPUT tu, kama cheti cha Ifm kinakupa fursa sawa na cha Udsm basi hiyo tofauti ya majina isikupe shida
 
The simple difference between the two is, Institutes are focused on acquiring a specialization on industry-related topics (Profession) while Universities are devoted on education and research(Academic).
Ingawa kuna baadhi ya universities wana institute like categories kwa ajili ya proffesional courses refers UDSM, wana College of Engineering, College of Business, College of Health etc.
Ni kama ilivyo tofaut kati ya CV na Resume, watu wengi huwa wanashindwa kutofautisha.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom