NACTE ichunguzwe. Imeshindwa kutoa Vyeti kwa wakati vya Wahitimu wa LITA. Wanaenda kukosa ajira zilizotangazwa na Serikali

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Serikali yetu makini hivi karibuni imetangaza nafasi za ajira lukuki kwa vijana waliohitimu Mafunzo ya mifugo sehemu mbalimbali.

LITA kama Taasisi ya Serikali yenye ithibati ya kutoa mafunzo hayo ikisimamiwa na NACTE imekuwa ikitoa wanafunzi lukuki kila mwaka.

Ili uweze kutambulika kifani ni lazima uwe na cheti cha uhitimu ambacho hutolewa na NACTE. Cha ajabu na kusikitisha vijana waliohitimu mwaka jana hawajapata vyeti vyao hadi sasa.

Wengi wao wanaelekea kukosa nafasi za ajira zilizotangazwa majuzi kwa kukosa vyeti vya uhitimu huku wakiwa wamafaulu masomo yao.

Mwisho wa kutuma maombi ni 7, Juni,2022. Ni vyema Wizara husika kuingilia kati,vijana wapate vyeti vyao kwani ni haki yao.

Taarifa zisizo rasmi ni kuwa sababu za ucheleweshaji wa vyeti zilizotolewa na NACTE ni uhaba wa watumishi.

Wizara husika ni vyema ikajiridhisha kwani yaweza kuwa ni uzembe wa kiutendaji na siyo sababu iliyotolewa.
 
Back
Top Bottom