Nachukia sehemu hizi tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nachukia sehemu hizi tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ULUMI, Jun 2, 2011.

 1. ULUMI

  ULUMI Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1.Kituo cha Polisi

  2.Hospitali za serikali

  3.Mahakama zote

  Sababu haki haipo rushwa imeshika kasi Wandugu wa JF mnasemaje nyie?
   
 2. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe lkh hatuna jinsi lazima tukimbilie huko au tuhame nchi make hata makampuni binafsi ni yanayotoa huduma kama hizo nchini ni machache sana,ldb semina elekezi waliyopata viongozi wetu itasaidia make nasikia walikuwa wanaongelea mambo ya uadilifu kazin lbd wanaweza kubadilika
   
 3. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Ama kweli sehemu hizi ni kero la Kitaifa, Nani wa kutuokoa mahali hapa!!Utumishi wa Umma au tabia zetu binafsi watanzania??
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  4. Kuendesha gari barabarani hasa dar.
   
 5. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nazichukia kupindukia!!
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hivi kwanini kisianzishwe kituo cha polisi za watu binafsi kama hospital?
   
 7. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,283
  Trophy Points: 280
  Kunani huku? mbona mimi sina shida napo kabisa yani...ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndo watu wanavyozidi kuweka posts in diferent titles za kuchukia hii sehemu! what is not hapenning!??
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nenda Tanesco uombe kuunganishiwa service line nyumbani kwako! Jinsi utakavyoonyeshwa orodha ndefu ya wanaosubiri hiyo huduma, utakata tamaa kabisa na kwamba nyumba yako haitakuwa na umeme kamwe!! Kumbe list hiyo ni feki ili ufanye malipo haramu yasiyo na risiti. Afadhali iruhusiwe kuwa na private investors kwenye umeme kama ilivyo kwa makampuni ya simu. TTCL wanaelewa vizuri utamu wa kuondolewa monopoly. Zamani ilikuwa shida kwelikweli kupata land line. sasa hivi unabembelezwa uwekewe line bure wewe ni kulipia matumizi tu.
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Mahakamani unaulizwa unataka kesi yako iishe lini...leo au siku nyingine....maanake kata kitu kesi iishe leo...usikate ukae nayo miaka. Nchi imeoza...Haki za msingi hazpatikani bila hongo!
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Zingine badala ya kuzichukia unazisikitia kama shule za kata.
   
 11. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni afisa wa serikali ama influential figure katika eneo lako huwezi jua usumbufu waupatao watu wa kawaida sehemu hizo tajwa. Aisee kuna kero si mchezo
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,283
  Trophy Points: 280
  Wala sio afande wala afisa anywhere in the government, I am actually an employee in the private sector..but nahisi kama hawa watu wanaonewa sana...ni nani Tanzania hii hatumiwi na mafisadi?? Nani!?? Hata huyo Slaa mwenyewe siku hizi kwangu namuona mizinguo tu (no pun intended!) sasa iweje polisi tu ndo waonekane wana makosa? ama koz yao yanaonekana vividly? i think tunawaonea sana..
  hebu re-evaluate again hiyo list yako uangalie kama bado itakuwa ndivyo...look at the society around you:
  1. Pita moshi mjini kwenye vibaraza vyote ni ombaomba...unapenda sehemu hizi sana? Huku Dar ndo kila uitwao mlango, utwakakuta nje kama walinzi..

  2. Unafurahia sana kupanda daladala mmejazana kama mambuzi? kama zile za milango miwili za mbagala,damn! nishaapa sipandi hizo kamwe..wacha nichelewe kazini!

  3. Unapenda, sana ukienda mikoani ukapita pale highway ama liverpool (na sehemu nyingine nyingi ambazo sijapita bado) baada ya kula watu wanatupa taka hovyo njia nzima?

  4. Unapenda sana wanasiasa wetu wanavyotupumbaza na kelele nyingi bila matendo (ambayo fyi, ndo yanayoleta matukio yote yanayomulikwa polisi!??)

  5. Why the police? do they really rank number 1 in your list!??
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hizi ndizo sehemu sumbufu kuliko zote maanake hata rushwa huku ndiko zina rank high.
  Naomba niongeze nyingine: Ofisi za manispaa au halmashauri za miji na wilaya
   
 14. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  nimetoka hospital ya serikali nimezidiwa zaid ya nlivyoenda haaa bora niende za binafsi
   
 15. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  kiukweli ofisi zooote za sirikali wanafanya kazi wanavyotaka nimeenda zahanati moja hapa kwetu tabata!yani leo asubuhi kuna doctor anamjibu mgonjwa km mbwa,mama wa watu hata kiswahili shida anajieleza jambo anaambiwa sooo what?.karibia nimchape kibao yule doctor,nimetoka hapo bila kumaliza vipimo vyote make wanazunguuka tu ili tuwape hongo.khaaa na kwingine koote ndo hivyo2.polisi pale hawajui tu uniform c ishu hata za bar pia ni uniform alaa kazi yao ni kutoa huduma na si vinginevyo
   
 16. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  4. Uhamiaji.
   
 17. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  4.bandari hasa ya dar
  5.ukumbi wa chawino dodoma
  6.chumba cha mtihani
  7.
   
 18. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mentor
  Binafsi nadhani polisi wamekubuhu. Hii ni kwa kuwa endapo una tatizo lolote, kabla hujafika mahakamani utapitia polisi. Endapo wewe unafahamika huko ulipona polisi wanakutetemekea, si kwa watanzania wa kawaida. Isitoshe tafiti nyingi zimeonesha jinsi gani huduma bora kutoka polisi ni adimu siku hizi. Vile vile orodha unayoweka yenye kero kuilinganisha na mtoa hoja ...orodha yako nadhani ni tofauti kidogo kimantiki! Ukiangalia mpangilio wa orosha ya mwanzo, hivyo ni vituo vya huduma tunakolipia kodi, tunawalipa mishahara watu hao, na bado huduma zao si nzuri. Omba omba....yeye hata akiwa kero kwenye baraza ahusiki moja kwa moja na kodi yako, vinginevyo aletwe mkurugenzi na mwenyekiti/meya wa halmashauri/manispaa wawajibishwe. Lakini POLISI, MAHAKAMA ni vyombo vya kutoa haki pasipo kuleta mashaka...na kwa uhakika usio na walakini! Uzoefu ni kwamba ndizzo idara zinashikiria bendera ya huduma mbovu! Biansi nammunga mkono Urumi kwa hoja hii! Labda suala la msingi hapa si kuvichukua vituo/huduma za hao watu, kwa kuwa polisi na mahakama, na hosptali zitadumu kuwepo ilmradi tunaishi. Kwa hiyo ni ninikifanyike kuwafanya wahudumie jamii bila kuomba rushwa na kulazimisha udhia ili watu watie rupia
   
 19. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280

  Mkuu!

  Hizo sehemu zote ulizozitaja kweli nazo ni kero pia lakini kumbuka pia sehemu hizo zote, ZINATEGEMEA chombo kama Polisi ndio msingi wa kulinda na kutetea usalama na ndipo mwanzo wa kutenda haki unapoanzia endapo sehemu hizo nyingine zitakapo kuwa NDIVYO SIVYO. Polisi inapokuwa legelege basi usitegemee maadili na kutimiza wajibu katika sehemu nyingine utakuwepo.

  Nakupa mifano michache:
  1. Madereva wanaposumbuliwa na trafiki huwa wanatoa rushwa si kwasababu wanakiri kosa isipokua kama utaamua kwenda kituoni, huo usumbufu utakaoupata wa kuzungushwa na mwisho wa siku haki haitatendeka hivyo watu wanaona bora kutoa elfu 2 au 5 na zaidi wamalizane aendelee na shughuli zake kuliko kwenda polisi ukazuiliwe gari na shughuli zako zisimame hata wiki nzima na mwisho wa siku uishie kutoa hela zaidi ya hizo.
  2. Kuuwawa kwa wezi na wananchi, ni kutokana na vitendo vya Polisi kuwasumbua wananchi wanapomkamata mwizi lakini unapompeleka Polisi badala ya wao kukushukuru kwa kumfikisha kituoni, huanza kukusumbua wewe na tena kuomba fedha ili watekeleze wajibu wao. Hapa nina mfano hai: Mie nilikua naishi Morogoro eneo linaitwa vibandani, siku moja nilirudi nyumbani kama saa 4 usiku nikakuta wakazi wa mtaani kwangu wapo na Mwenyekiti wa mtaa wakiwa wamemkamata jamaa ambae alisadikika ni vibaka wanaokaba watu usiku kwani walimuona akiwa na kisu, bisibisi na akiwa anatembeatembea mtaani bila kueleweka ndipo walipomsimamisha kumuhoji akatimua mbio, basi alikimbizwa na alipokamatwa akapata kipondo na wakampeleka kwa M/kiti ili kupata muongozo, kwakuwa hali yake ilikua mbaya, nilikua na usafiri tukaondoka hadi polisi tukawakabidhi, polisi wakatuandikia pf3 na kutuambia tumpeleke hospitali bila kuwa na askari, basi tukaamua twende tu hospitali, huko nako tukakuta mtihani, reception wakadai tutoe malipo ya faili na kumuona daktari, kweli tulikua wakali, yaani mwizi alafu tumlipie, wakaona aibu wakafungua faili kutuambia tuende kwa daktali, ndugu yangu tulimsubiri huyo daktari kama masaa mawili bila kutokea, tukaona si vyema kumuacha pale maana yakitokea matatizo M/kiti wetu anaweza pata msukosuko maana alikwisha jiandikisha polisi ikabidi tumrudishe polisi, tulipofika polisi wakasema eti turudi tena hospitali na endapo kama atalazwa basi baadhi yetu tubaki hapo hospitali, kweli tuliona huo ni upuuzi uliopitiliza, ina maana ingefika asubuhi tungeambiwa tumpatie chai na hata chakula cha mchana? Tulichofanya ni kumuacha pale polisi tukaondoka maana tuliona hakuna haja ya kubanana zaidi maana hakuleta madhara bado mtaani. Mifano iko mingi lakini angalia mambo kama hayo kwanza kwanini polisi isiwe namba 1? Kama bado hukubaliani basi NDUGU ITAKUA HAYAJAKUFIKA BADO na MSHUKURU MOLA WAKO!
   
 20. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #20
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda waheshimiwa wetu wanaitwa wabunge wakalianzishe huko mjengoni....ha ha ha!
  Pia mahakama zianzishwe binafsi.
   
Loading...