Nachukia harusi/sherehe zinazohusiana na harusi. Hii ishawahi kukutokea hata wewe?

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,766
Habari za wakati huu wanaJF.

Acha niende kwenye maada husika..! Niko kwenye mahusiano serious kabisa na mtoto wa Watu. Tayari nimeshatoa mahali kiasi (50%) panapo majaliwa nitapeleka tena kiasi fulani huko ukweni kupunguza punguza hilo deni . Sasa kuna jambo ambalo mimi binafsi sipendi tu kabisa. Nalo ni Sherehe.

Niliwahi kuongea naye muhusika nikamwambia mimi sitaki mambo ya sherehe nataka nifanye taratibu za kimila ila mambo ya Sherehe sitaki kama ni Cheti tutaenda hata mahakamani tufunge ndoa mbele ya mashahidi wasio zidi wanne iishe.

Mrs mtarajiwa akasema mimi nahitaji harusi bhana* Nikqmwambia mie sipendi sherehe na hata sasa sherehe nikizohudhuria mpaka nimefika umri huu haziwezi fika 3 ukiondoa graduations za O level, A level na Chuoni.

Mimi sio mtu wa sherehe ila mama lao anataka sherehe japo yeye alisema hata isiwe ya watu wengi ila watu hamsini inatosha na mimi natamani tufanye maisha yetu Bila hizi mambo za masherehe.!

Nisaidie nifanyeje kutatua hili suala.! I am simply an introvert kind of.! Sijui asee nifanyeje.!
 
mi mwenyewe sipendi kabisa siku ya kuoa kwangu japo ndugu zangu wanataman nioe hata kesho ili wanichangie ifanyike sherehe kubwa cjui hata nawakwepa vipi
 
Kuna jamaa Infantry Soldier alisema wale wanaopenda kuhudhuria graduation ni vilaza....

Sasa ndugu yangu wewe sherehe uklizohudhuria zote ni graduation. Kuna tatzo hapa.

 
Simple.

Mpe ruhusa ya kufanya send off halafu siku ya ndoa mnakutana mahali pa kula viapo na ndugu wa karibu tu na kila mtu kutawanyika kwake
 
Back
Top Bottom