Nachingwea kumchukulia fomu ya ubunge aliyewacharaza bakora walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nachingwea kumchukulia fomu ya ubunge aliyewacharaza bakora walimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Nov 7, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  KINYANG'ANYIRO cha Ubunge katikas Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi kimechukua sura mpya baada ya wananchi kujitokeza kueleza kuwa watamchukulia fomu ya ubunge aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali ili agombee nafasi hiyo.

  Wananchi hao wamesema kwamba wamechukua uamuazi hu baada ya kumwona Mnali kuwa ana uwezo wa kuwaletea maendeleo pamoja na kuthibiti uzembe miongoni mwa watumishi wa umma.

  Mmoja wa wananchi hao ni Costanine Makota ambaye aliiambia Mwananchi Jumapili kwamba yupo tayari kunchukulia fomu ya kugombea ubunge
  Mnali kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Hata hivyo, Mnali mwenyewe amethibitisha liliambia gazeti hili nyumbani kwake kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa na makundi mbalimbali ya wananchi wa jimbo hilo wakiwemo vijana na wazee.

  รข€œMwanzoni nilikataa kugombea nafasi hiyo lakini, wananchi wameniomba na kwa heshima sikutaka kuwavunja moyo, nikakubali,"alisema Mnali.

  Mnali ameeleza kuwa jimbo la Nachingwea linahitaji mbunge mwenye dhamira ya kweli kuwaletea wananchi maendeleo endelevu na anaamini yeye ndiye anayefaa.

  Mnali alikuwa mkuu wa wilaya ya Bukoba, aliondolewa madarakani baada ya kuwachapa walimu viboko baada ya wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika mitihani ya darasa la saba mwaka juzi.

  Akizungumzia tukio hilo, alisema kuondolewa kwake madarakani kulitokana na kutekeleza wajibu wake kama mkuu wa wilaya. "Niliondolewa kazini baada ya kutoa dozi kwa walimu nikitekeleza kazi yangu kama mtuhumishi wa serikali lakini, nikiwa mbunge kazi yangu itakuwa kuihimiza serikali kudhibiti nidhamu ya walimu ambao wengi ni walevi.

  Source: Mwananchi
   
Loading...