Nachelea kukubali Udaktari uliopo ndani ya Hamis Kigwangalla

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Zamani tuliamini na kunasibisha matendo ya wasomi na tabia zao. Ila naangalia mwenendo, matendo na maisha ya Hamis Kigwangala yananifanya nijiulize kuwa Daktari ni uwezo wa akili kupambanua mambo au inategemea na kufanya mitihani ya darasani?

Unapokuwa na Daktari ambaye kila jukumu analokabidhiwa anafeli na ajui kama anafeli ili ajirekebishe unajiuliza reasoning capacity ya huyu mtu ipo sawa?

Ni kweli hadhi ya Uwaziri imeshuka kiasi cha kumfanya Kigwangalla kuishi mitandaoni akitukanana na watu wa mitandao? Nini makatazo kwa viongozi waandamizi wa Taifa letu? Kwamba kesho mtu wa tabia hii Hana waangaliz huko CCM wakumwelekeza aishi vipi baada yakunyimwa Uwaziri? Elimu yetu imeshuka kwa Kasi hii au watu wanapata madaraka kwa ngekewa?

Pls Kigwangalla tulitegemea uheshimishe hadhi ya madaraka lakini siyo kama unavyoishi nakuandika mitandaoni. Kwanini unadhiirisha una msongo wa mawazo kwa kukosa uwaziri? Haiwezekani ukaa kimya na stress zako? Je, hata mke na marafiki awakusaidii kukuelimisha namna yakuiishi na msongo wa mawazo?

Jaribu kujikubali mdogo wetu ufanye kazi za msingi kuliko kukesha mitandaoni huku ukidhalilishwa. Kimya kitakusaidia
 
Ni kweli hadhi ya Uwaziri imeshuka kiasi Cha kumfanya Kigwangala kuishi mitandaoni akitukanana na watu wa mitandao? Nini makatazo kwa viongozi waandamizi wa Taifa letu? Kwamba kesho mtu wa tabia hii Hana waangaliz huko CCM wakumwelekeza aishi vipi baada yakunyimwa Uwaziri? Elimu yetu imeshuka kwa Kasi hii au watu wanapata madaraka kwa ngekewa?
Kwa ujumla ni kushuka kwa maadili na haiba ya uongozi ktk nchi yetu.

Siyo Kigwa peke yake, kuna mtu aligombea urais kabisa, anaongoza kwa kutukana huko mitandaoni, anatukana mpaka maiti.

Now you can imagine, huyo ntu ndiye alitaka kuwa rais wetu! Tungepata rais wa hivyo sijui nchi ingekuwaje?

Nadhani salamu zetu zingeanza na matusi:
Msalimiaji: "nyie wangese peoples "
Waitikiaji: "power kudadeki zako"
 
Kubali kuwa ana digrii ya udaktari ingawa hana ujuzi wa udaktari kwa vile hajawahi kufanya kazi hiyo.

Mimi bado nina leseni yangu ya ya kuendesha pikipiki (of course inahitaji kuwa renewed) na hivyo nina tambuliwa kama mmoja wa wenye kuwa na leseni za kuendesha pikipiki -kwa namna fualni.

Lakini sijaendesha pikipiki kwa miaka takriban 30 na wala sikumbuki jinsi ya kuendesha pikipiki tena. Kigwangwala pia ni vivyo hivyo, ana leseni halali lakini huenda anahitaji renew.

Kutokuwa na uzoefu wa uganga hakumzuii kutambulika kwa digrii zake.
 
Chunguza hili kwa muda wako binafsi Binadamu wengi wapenda na waamini ' Ushirikina ' baadae huja kuwa ni Wapumbavu ( Mapopoma ) sana halafu hata ' Utahaira ' nao huanza kuwaingia taratibu na huja Kufa Vifo vibaya, vya ajabu na vya ' Kushtukiza ' pia kama cha Mwezi Machi, 2021 ila tarehe ndiyo nimeisahau tu kwa sasa.
 
... tumsome "mzalendo" anayeomba kuungwa mkono na watanzania na ujumbe wake murua ... "piga risasi"

Magufuli baba lao, Makonda baba lao...
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!
 
Chunguza hili kwa muda wako binafsi Binadamu wengi wapenda na waamini ' Ushirikina ' baadae huja kuwa ni Wapumbavu ( Mapopoma ) sana halafu hata ' Utahaira ' nao huanza kuwaingia taratibu na huja Kufa Vifo vibaya, vya ajabu na vya ' Kushtukiza ' pia cha Mwezi Machi, 2021 ila tarehe ndiyo nimeisahau tu kwa sasa.
Yale maimani hayawezi kuacha salama
 
Zamani tuliamini nakunasibisha matendo ya wasomi na tabia zao. Ila naangalia mwenendo,matendo na maisha ya Hamis Kigwangala yananifanya nijiulize kuwa Daktari ni uwezo wa akili kupambanua mambo au inategemea na kufanya mitihani ya darasani?..

Ukishaingia ccm lazima fuse na ubongo ziondolewe kichwani
 
Back
Top Bottom