Nabii wa Ishara Tanzania: CCM wataomboleza, Zanzibar kuna mgogoro na kifo cha mtu mkubwa 2021

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,406


Tizama mwenywe dakika ya 32 - 37 na 47- 49:30 ama kama unaweza tazama yote.

Katabiri mengi yatakayojiri 2021, lkn mm nimechukua ya kisiasa tu.
1. Wakuu wa mihimili 3 mmojawapo atapata shida kubwa ya kiafya na kupelekea ku-rest in peace.

2. Mmojawapo wa viongozi wakubwa wa ccm ataingia kwenye mgogoro wa kiafya. Na kwa mujibu wa nabii anawaona ccm wakiomboleza (maana yake ata-rest in peace.

3. Anaona ajali mbaya Zanzibar itakayohusisha mtu/kundi la watu itakayogharimu maisha ya kiongozi mkubwa.

4 . Anaona mgogoro mzito utakaosababisha mgawanyiko mkubwa Zanzibar.

5. Anaona kiongozi mkubwa wa chama (yaweza kuwa toka upinzani ama tawala) akipewa majukumu makubwa ya kimataifa.

Ni hayo tu niliyoweza kuyanyaka.
https://uc.xyz/MovvM?pub=link Share File
 
Toka awamu ya 5 imekalia kiti na maisha kuwa magumu, watabiri wengi sana wamejitokeza na kunena kwa lugha zote. Lakini hadi muda huu nachapisha namba za kila rangi tumezisoma. Vyovyote itakavyokuwa watu tumeteseka hadi tumezoea mateso.

Nasemaje, Mitano tena na iwe milele na milele hadi wanalumumba akili ziwarejee ndiyo ukombozi wa kweli utakuja.

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Toka awamu ya 5 imekalia kiti na maisha kuwa magumu, watabiri wengi sana wamejitokeza na kunena kwa lugha zote. Lakini hadi muda huu nachapisha namba za kila rangi tumezisoma. Vyovyote itakavyokuwa watu tumeteseka hadi tumezoea mateso...
Kwahiyo wanalumumba ndo wataisoma namba peke yao wewe hautahusika sio
 
Manabii walikuwepo zamani hawa wa sikuhizi ni wachumia tumbo. Wamefanya huduma hii kukosa heshima ktk kanisa na kwa kweli wanamdhalilisha Kristo!

1. Maunabii ya 2015 wakati wa Uchaguzi yote yalikuwa null and void
2. Maunabii ya Uchaguzi 2020 yote yamekuwa null and void
3. Maunabii ya Lema yamegoma kutimia akakimbia nchi!
Ongezea mwenyewe.....

Mungu anatuwazia mawazo mema tena ya Amani! Kutupa tumaini siku zetu za mbeleni!
Yeremia 29:11

Mungu huyabatilisha mashauri ya wwnadamu, huyatangua makusudi ya watu, shauri la Bwana lasimama milele! Makusudi yake vizazi na vizazi!
Zaburi 33:10-11

Queen Esther
 
Mhh, huyu ni mrengo gani wa kisiasa mbona utabiri wake umeegemea upande mmoja?
Anatabiri mawazo yake ya kichadema hakuna nabii hapo

kazi ya nabii wa agano jipya ni tofauti na manabii wa agano la kale wa agano jipya kazi yake ni kufariji na kujenga mwili wa Kristo

karama ya nabii ya agano jipya inajikita kwenye upendo sio hukumu sababu agano jipya linatamka wazi Mungu hafurahii kifo cha mwenyr dhambi

ukiona nabiii anatamka kuwa mtu fulani atakufa huyo ana mapepo sababu kazi ya shetani agano jipya ni kuua na kuharibu na kutabiri mabaya kwa nchi au kwa jamiii

huyo nabii ni nabii wa shetani baba wa kuwa na kuharibu a kutabiri mabaya

watoa pepo nendeni mkamtoe mapepo huyo nabii wa shetani
 
kazi ya nabii wa agano la kale na nabii wa agano jipya ziko tofauti kama mbingu na ardhi ukiona mtu anatoa matamko ya kiagano la manabii la kiagano la kale kama huyu nabii koko mwana wa Ibilisi anayetakiwa kukemrwa na kila mtoa mapepo pepo wamtoke kwa jina la Yesu
 
Back
Top Bottom