Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Siamini mungu sio kwa sababu ya corona, mimi nina uhakika mungu hayupo, hajawahi kuwepo na wala hajawahi kufanya chochote. Corona ni mfano tu. Sasa nyie mnaoamini ma mnaoomba Mumgu asie na uwezo wala msaada wowote, miaka na miaka mnamuomba, ukimwi, kansa, ebola, nk ni magonjwa yapo miaka na miaka, je Mungu wenu bado hajasikia maombi yetu aondoe hayo magonjwa au mambi hayajamfikia? Endeleeni kupiga kelele labda amelala, kelele inaweza kumuamsha.
Brother, angalia sana. Wapo wengi tu waliosema kama wewe, kumhusu Mungu, na walikiona cha mtema kuni. Kati yao ni hawa:- Actress/actor Marylyn Monroe, Beetles singer John Lennon, na engineer aliyetengeneza meli ya Titanic . Tena huyu alisema kuwa "Titanic, imetengenezwa imara zaidi ya meli zote, hakuna dhoruba itakayoizamisha na hata Mungu hawezi kuizamisha".
Si unajua kilichoipata meli hiyo?.
Nakuombea msamaha Mungu akusamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kweli mkuu Pascally umeoa katoto mpaka kanakushawishi uangalie wasaf tv? hiv kumbe hiv vitoto vina influence? yani kweli mtu mbishi kama wewe pascally mpka rais unamhojig maswali mazito leo hii umeekewa wasafi tv hata huuuliz kumbe tutoto tuna nguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Update
Na leo tena Nabii Malisa yuko live ndani ya nyumba Wasafi TV.

Leo Studio wamealikwa Emanuel Mbasha na Martha Mwaipaja hivyo hakuna msongamano, ila social distancing bado ni zero.
P
 
Nabii Malisa anasema Mungu amesema na Tanzania kupitia rais Magufuli na kutuhimiza Watanzania tufuate ushauri wa rais Magufuli wa kumtegemea Mungu!. Ni Mungu pekee ndiye anaweza kutuokoa kwenye hili janga la Corona.
P
 
hivi kweli mkuu Pascally umeoa katoto mpaka kanakushawishi uangalie wasaf tv? hiv kumbe hiv vitoto vina influence? yani kweli mtu mbishi kama wewe pascally mpka rais unamhojig maswali mazito leo hii umeekewa wasafi tv hata huuuliz kumbe tutoto tuna nguvu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hufi leo, hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
P
 
Leo kwenye utabiri, Nabii Malisa amesema wanawake wote wenye jina la Diana, jina hilo lina majanga kwenye mahusiano, mapenzi na ndoa.

Kuna Diana mmoja akapiga siku na miongoni mwa matatizo yake ni kukoma kwa siku zake 4 years ago. Nabii akamuombea, na kumwambia alifungwa na shetani, amemfungulia na saa hii hii siku zake zitaanza instantly.

Nabii akamwambia huyo Diana ajicheki kama zimeanza siku zake na atangaze live... hivi ndio vitu gani vya kuuliza live?. Kuna mambo fulani ya wanawake yanahitaji staha fulani, mwanamke anayejiheshimu, huwezi kumwambia ajicheki na kutangaza live "nimeanza"!, thanks God huyo Diana anajitambua, hakujibu.

Naendeleza ule wito Kamati ya Maudhui ya TCRA wawangazie hawa TV na Redio kwenye hizi live zao za mahubiri, kiukweli kuna udhalilishaji mwingi wa the right to privacy za watu.

Redio au TV zikiamua kuwatumia hawa Manabii ma dogo, wapewe abc za miiko ya utangazaji sio wanasema tuu faragha za watu, faragha nyingine ni udhalilishaji.
P
 
Kiukweli jina nilikuwa nalisikia leo ndio nimemuona, kiukweli yuko fit sana, kuna mdada mmoja Mwasha aliyekuwa na ile 8020 blog namfahamu.
P
Yule yuko ndani kwa ngada.....!! Huyu msanii mwingine ndio anaemlea Luvanda MC kelele zote analelewa huyo Dada bingwa kulea huyo
 
Yule yuko ndani kwa ngada.....!! Huyu msanii mwingine ndio anaemlea Luvanda MC kelele zote analelewa huyo Dada bingwa kulea huyo
Duh...!, hilo la MC kulelewa it's not true kwasababu MC Luvanda namfahamu vizuri, ni mmoja wa ma Top MC wa viwango hapa Bongo, hivyo hoja ya kulelewa haina mashiko, huyo dada ni mkewe wa ndoa sio haki kusema analelewa, ila pia inaruhusiwa kwa mke kumlea mume na mume kumlea mke.

P
 
Mafundisho mapya haya!!! Mkristo ni yule anaefuata mafundisho ya kristo.
Yesu katika kuikamilisha torati alikataa talaka, mke zaidi ya mmoja,kupigwa na mawe mpaka kufa mtu aliyefumaniwa kwa uzinzi na mengine mengi .Rejea mathayo 19:3-11. Pamoja na kuikamilisha bado hukubali yaliyokamilishwa, kuoa mke zaidi ya mmoja halipo kwa wakristo labda utupe mfano mmoja.

Swala la mavazi ni tamaduni za jamii mbalimbali na hijabu ni tamaduni za middle east mkuu,hilo huhitaji kulaumu wazungu unataka mimi mhadzabe nivae kanzu kisa yesu alivaa
 
Huwa sipendi sana kujadili mijadala inayohusu dini ya mtu au watu…. But kwa kusema kuwa wanaokufa kwa Corona ni watu wenye magonjwa mengine….So is UKIMWI.... upungufu wa kinga mwilini unaruhusu magonjwa mengine yashambulie..now Corona ni ugonjwa unaosindikiza wenye magonjwa what does it mean?
 
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Mkuu Paschal,

Kwanza nakupongeza kwa hii "follow up". Nadhani sisi kama members humu tunaoleta habar inabidi tulifanye hili jambo,litasaidia kuacha tabia ya mambo yapite tu.

Pili tutakuwa pamoja hiyo kesho.

Mwambie mh waziri ligi ya vodacom ianze trh 16.05.2020.

Lakini pia asisitize mashabiki tuende kwa ridhaa yetu,kusiwe na katazo,ka corona kameshasepa.

Jambo lingine mchomekee,lile suala la idadi ya wachezaji wa kigeni aliache nature ifanye kazi yake.

Tz tunavipaji sana,tutapambana wenyewe. Wao mbona kandarasi wanawapa wageni. Rejea SGR,BRT,Striglers gorge..etc.

Kuhusu uwekaji katika vilabu na ligi,aitishe mjadala mpana wa wadau ili tuweke sera kama serikali iwe muongozo kwa wawekezaji.

Kuhusu habari, bado tunahitaji uhuru wa kutosha,hii habar ya ukomo wa uhuru ni kichaka cha watu wasiowaadilifu. Anatuambia nini kuhusu utoaji,utafutaji na ulaji wa habar hasa wakati huu ambao karibu kila mtu ni mtoa habari,mtafuta habari.

Anajisikiaje anapoyafungia magazeti?

Sent using iphone pro max
 
Back
Top Bottom