Nabii Joshua Mbugua wa jijini Dar ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutapeli waumini wake

IMEANDIKWA( ITS WRITTEN)

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
2 Wathesalonike 2 :10

11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
2 Wathesalonike 2 :11

12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
2 Wathesalonike 2 :12

Mtu anapolikataa Neno la Mungu lililodhahili na kuchagua vifungu fulani na kuvitupa vingine kwa kisingizio agano limepitwa na wakati au kusema hilo limegongomelewa Msalabani basi ategemee hayo. Kuombewa Chupi zao mbele ya kanisa , Kutoa pesa , Kuliwa ile Tamu, n.k
 
nabii suguye wa wrm jamaa namkubali sna.huwa napenda sna kuangaliaga chanel yake wrm
 
Huyu
Baada ya nabii Issa(Yesu) kilipita kipind kirefu sana then akaletwa nabii Muhammad (mtume /nabii wa mwsho):

hao wengine wa sasa ni completely FAKE!
Huyu ndio yupi tena .au ni yule aliyeoa kitoto cha miaka tisa .
 
Kwenye huu uzi habari kwangu ni SAM MAHELA Kuhamia TBC ila huyo Nabii kutapeli waamini wake kwangu sio habari maana huwa Wanawatapeli kila siku.
 
Mungu anataka watu walioacha dhambi, watu nao wanataka miujiza tu ukiwaambia kuacha dhambi hawataki, Yesu alisema mtaomba kwa jina langu sio mtaweka maji wala mafuta wala kutembeza vitambaa, tusiwe wavivu wa kusoma Neno la Mungu, jihadharini *******nao watawadanganya wengi!
 
hapa ndipo nawakubaligi hawa ndugu zangu watoto wa mama mdogo, hawanaga ufala kama huu huyu asingefika kesho
 
habari wakuu,

Kwenye taarifa ya habari ya TBC leo usiku wametangaza habari ya nabii Mbugua wa kanisa la CAG kudaiwa kuwatapeli waumini wake. Mchungaji huyo anadaiwa kuagiza waumini wapeleke pesa ili aziombee ziwe nyingi kisha atawarudishia bila kuchukua hata shillingi.

kama mnavyojua ndugu zetu wapenda dini wana kitu kimoja in common (low thinking capacity) nabii kawapiga hela siku aliyowaambia wakachukua kawaambia hela zimungua mlimani alivyokuwa kwenye maombi.

kwa mara ya kwanza namuona huyu nabii kwenye channel ten nilijua tu ni tapeli jinsi anavyofundisha na mavazi yake kavaa kama shehe ana coach watu watoe ushuhuda,

Walokole amkeni mtapigwa na manabii feki mpaka lini acheni kuhangaika hakuna kitu kinachoitwa maombi na miujiza just live your faithful life, wenzenu waislamu wametulia na mtume wao wala hawatarajii hata kamuujiza kokote ni kupambana na maisha na huo ndio uhalisia.
Esa ziombewe ili ziongezeke? Jamaa wajinga mno.
 
Katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku TBC kutoka kwa reporter SAM MAHELA, kuwa nabii huyo anayepatikana DAR anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutapeli fedha waumini wake ambapo waumini wawili wamethibitisha hilo mmoja akitapeliwa laki 6 na mwingine laki 2 eti aliwashawishi wampelekee hela aziombee na baadaye akadai zimeungua na moto.

Binafsi ukiachilia mbali kutokuwakubali hawa wanaojiita manabii,lakini huyu alivuka kiwango cha kutokubalika maana hajui hata kuhubiri kazi yake ni kutoa matumaini tu mazurizuri kwa waumini na kisha kuombea watu na hata kuwataka walishike vazi lake ili kupata baraka kisha inafuata promo ya miujiza.

Nilishaona pale ni 0 lakini nikashangaa kuona watu wanamshangilia na wanajazana kanisani kwake ndipo nilipobaini shida kubwa ya sisi wabongo kwa kupigwa kijinga.

Hakuna cha nabii hapa wala BULLDOZER, MWAMPOSA, MITI MINGI n.k ijapo hawa kwangu wana unafuu kwenye mahubiri yao kwamba si haba wanajitahidi kuwa huwezi toka kapa ila sio mazingaombwe yao ya kuombea.

Mkome.
TBC, Sam Mahela?
 
Huko nyuma ķoote nimeunga mkono ukosoaji wenu kuhusu manabii wa uongo.ILA HILI LA KUMHUSISHA/KUMUUNGANISHA T.B.JOSHUA NA HAO MANABII FAKE, NASEMA NOOO! YES, BIG NOOO..
T B Joshua ndio tapeli la kutupwa...Serikali ya Cameroon wamepiga marufuku wananchi wake kwenda kwa tb joshua kutapeliwa...
 
Huko nyuma ķoote nimeunga mkono ukosoaji wenu kuhusu manabii wa uongo.ILA HILI LA KUMHUSISHA/KUMUUNGANISHA T.B.JOSHUA NA HAO MANABII FAKE, NASEMA NOOO! YES, BIG NOOO..


TB Joshua hana unabii wowote, he's as fake as fake can be. Anawalostisha tu wajinga. Manabii woooooote toka Nigeria ni fake na si watu wa kuwafuatilia hata kidogo.
 
Watu wamepiga kelele humu kuhusu hawa manabii, kuna watu wao wanawa support kinoma, tumesema hawa matapeli, lakini watu kutwa wanakesha huko, wengine hata wakidai kuwa huyu au yule afadhali...
Kifupi hakuna cha nabii wala nini, hakuna cha kutoa majini wala kuleta nyota, wote matapeli, kuanzia mama lwakatare mpaka tb joshua, ila watu wameingia kingi toka enzi hizo, wengine wakidai wako pale eti kibiashara!
Kutokana na hawa matapeli, ndoa zimevunjika, watoto yatima wametumiwa, watu wamefilisika, watu wameharibu uhusiano na marafiki, ndugu na wanafamilia...
Wacha waliwe tu hela zao, wala hatuwahurumii...
 
Back
Top Bottom