Nabii Frola bado unaendelea kuwatapeli watu? Sitasahau 1-Aug-2014 ulivyotaka kunitapeli mchana kweupe

Wazee kumekucha?

Wakati nakuja Dar rasmi kwa ajili ya kuanza makazi ya kudumu nikajisogeza kwa nabii Frola ili nisogeze shida zangu za kiuchumi. Pia nilikwenda nijifunze utumishi wa Mungu maana nilipokuwa mkoani tuliwahi kuwasiliana na kupanga hayo. Nilipokuja Dar sikumtaarifu kuwa nimekuja nikajipenyeza tu na nilienda kanisani kwake. Niliona mifumo ya kiutofauti katika ibada kwa Jumapili 2. Nikajipa moyo huenda ni mafunuo tu.

Jumatatu tar 1,Septemba 2014 nikaenda kwenye ibada, ibada ambayo pia hukutana na mtu mmojammoja na kumweleza yaliyo sirini. Sasa huku tukiwa foleni wale wapambe kazi yao ni kutoa shuhuda za uongo ili kutuandaa kisaikolojia huku wakisisitiza mara tutakapoonana na Nabii tutoe kiasi kikubwa maana nabii anajua mpaka kilicho mfukoni au benki.

Mara nabii akaenda mapumziko ya lunch kwa nusu saa hivi. Aliporudi akafanya ibada ya pamoja iitwayo ya unabii. Akamtabiria wa kwanza, wa pili na Mimi nikawa wa tatu. Nabii alikuwa hanijui licha ya kwamba tumewahi kuwasiliana mara kadhaa. Ile siku nilivaa suti nyeupe, kuanzia viatu, soksi mpaka shati juu. Akaniambia pita mbele nikapita. Akaanza "Wewe una kiwanja na unahangaika kutafuta wateja kwa muda mwingi lakini imekuwa ngumu, Mungu ananiambia anakwenda kukuinua sana na hata kiwanja utakiuza kwa fedha nyingi" kweli si kweli? Nikamjibu kweli .

Akaniambia toa sadaka ya shukrani na wenzako wakuunge mkono. Nilikuwa na kahela kidogo ila nikagoma kutoa maana wakati huo sikuwa hata na kiwanja, nikarudi kwenye kiti nilichokalia nikakusanya vitu vyangu nikaondoka huku ibada inaendelea.

Nabii Frola ni tapeli na muhuni tu. Hawa manabii wote ni wahuni na wezi, zama za manabii zimepita, Nimewafanyia tafiti wengi na kubaini ni wezi wanaotumia ujinga wa waumini.

Dawa ya kufanikiwa ni kufanya kazi kwa juhudi na kumtegemea Mungu pekee.
Samahani heading nimekosea ni September mosi na si Agosti.[/QUOTE
Nenda kwa kwa kakobe. Ndie mtumishi wakweli aliyesalia hapa 🇹🇿 tz
 
Wengi walianza kwa majina ya mchungaji, ila walipoona majina haya hayana nguvu ya kimvuto wakajipachika majina ya nabii na wengine mtume. Wengine mtume na nabii

Nimejaribu kuwaza kwa trend hii je wanaweza siku moja kufikia kujiita Papa au Kardinali?
 
Namfahamu,niliwahi kufika kwake mwaka 2012, alikuwa anajirembaa halafu akianza kuhubiri mijasho inamrudisha kama katoka kuoga. Nilipelekwa na mtu, sijawahi kuenda tena akiwa kwenye banda pale tangbovu.
 
Mie niliambiwa mke wangu ananifunga nisiendelee, wakati sijawahi oa, sina mwanamke mwenye lengo nae mie chapa ilale.

nikauliza mara 2 akaanza porojo nikasema sawa sawa
 
Back
Top Bottom