Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

Mathayo 7
Msihukumu nanyi mtahukumiwa maana kiasi kilekile mnachohukumu ndicho kiasi hiko hiko nanyi mtapimiwa kuhukumiwa.

kuna laana katika
1.Kuhumu wenye haki
2.kunyooshea watumishi wa Mungu vidole
3.Mungu anamwita mtumishi wake katika hali yoyote
4.Mungu usifikiri hakuoni maovu yako, usifikiri hakujui anakujua lakini wewe hajakuhukumu lakini wewe unamuhukumu binadamu mwingine, unamfanya Mungu hana akili? hajui analolifanya?
5.Mungu kamwita jinsi alivyo ili Mungu ajitwalie utukufu wake. Yesu akasema sijaja kwa ajili ya wenye haki nimekuja kwa kwa ajili ya waliopotea ili wapate uzima na uzima tele! Mungu anaweza kukupa maradhi ya cancer ya ngozi ili ujue hapendi dhambi unayofanya. Mungu anaweza kukuparalizisha mkono wako unaoandika hapa. Mungu anaweza kukupa maradhi ya kujinyea na kujikojolea anaweza kuuwa anaweza kufufua! wewe ni nani binadamu unayejihesabia haki mbela ya Mungu? wewe ni mkuu kuliko Mungu wa majeshi? wewe ulimuumba Mungu au yeye alikuumba wewe? na unamhukumu binadamu mwenzako? unamfanya Mungu mjinga? Mungu alikosea kuumba? iyo akili nani kakupa? iyo afya unayoringia mpaka unamhukumu mwingine? unampangia Mungu nani amfanye mtumishi? mbona wewe mzima Mungu kakuruka kamfuata mtumishi wa Mungu? angalia Mungu asije kukuangamiza! Mungu anaweza kukufanya ombaomba maisha yako yakawa magumu! Na akafanya mlangowako kwa Nabii flora alafu ndio wa kukuombea sijui utaenda au utaendelea kumsema? Mungu anaweza kukupiga wewe unayemsema mtumishi wa Mungu alafu kwa makusudi mlango wa wewe kufungulia akaufanya kwa uyu mtumishi. kila mahali unapoenda Mungu hakufungui mpaka kwa uyu nabii sijui utafanyaje? Mungu anaweza kukuletea msiba kwako! anaweza kukutesa! ila anakuangalia tuu unahukumu binadamu mwenzako alafu unamtukana mtumishi wa Mungu. Goliath alikuwa na kiburi zaidi yako lakini Bwana wa majeshi alimpoteza kwa jiwe moja tuu, alijitapa kama wewe! alitukana kama wewe! alijiinua kama wewe! angalia hasira ya Mungu isije kukuangukia. siandiki kukutisha ila nakueleza ya kuwa Mungu hataki na hapendezwi! kujihesabia haki! angalia Mungu asiruusu jiwe lililopiga Goliath likupige na wewe.

Hata utapeli wa wazi msiambiwe jamani? hapo mnatapeliw tu hamna kitu, nurudi ktk makanisa yenu na mtubu kabisa,
 
Wajinga ndiyo waliwao,Mungu hakua mjinga kutompa mwanamke unabii,hawa wa siku hizi sijui mtajibu nini siku ya kiama
GENTAMYCINE
unakosea. Mungu aliwapa wanawake unabii; ref. miriam, nabii debora. kasome kitabu cha wafalme kwa habari zake zaidi. ila huyu nabii wa gentamycine ni janga la kiroho. ni nabii ila ni nabii wa uongo.
 
Ni mikorogo kwa kwenda mbele...
????????????>..,,lljy@@2@@@@@@@!!!!!!!!!*********** Mungu neema yako baba
attachment.php
 
mimi haya mafundisho ya kusema fuata neno usifuate matendo ni ya kipuuzi maana Yesu alisema tutawatambua kwa matendo yao[/QU

nitonye;
Sikutaka kucomenti chochote lakini umenikuna. Hivi kweli, mtu na akili zako atokee mtu atii anakuambia; Fuata mimachokuambia usifuate ninacho tenda. Kesho utakwenda kwake??
Hivi kweli, mtu unayejikoboa kama mahindi ya sembe, utakapofika pale mbele za Mungu utasema nini? Mtu anauliza atii; Ni wapi pameandikwa usijikoboe!!!! Ni aibu kuuliza swali kama hili au sivyo?? Hujasoma neno la Mungu kuwa hata usijichore (Tatoo) mwili wako?? Iweje kujikoboa kuwe sawa??
Mnaniambia ati anatumia mafuta ya mzeituni kutoka Israel, nikitumia mafuta kutoka Supermarkiti kuna shida gani?? Hivi kinachotoka Israel ndiyo "Kitakatifu" saana au? Nasema; Hapo ni manyoya tuuuuu.
Hata angemfanya kuku akojoe, hanitishi huyooo

Ngoja nikujibu tu apo kwenye mafuta baaaas,supermarkiti ulosema apo ni nchi gani kwani
 
Mathayo 7

3.Mungu anamwita mtumishi wake katika hali yoyote
.

NI kweli kabisa...lakini mtu huyo lazima abadilishwa auvae utu upya na kuachana na uzamani na tabia za zamani zisizompendeza Mungu na wanadamu.......mkorogo?
 
wewe unajuaje Mungu alimwita na mkorogo wake? Mungu anaweza kukuita na huku ulikuwa malaa unajiuza, anaweza kukuita na huku ulikuwa mlevi! mimi ndo nimeanzisha hii thread lakini daught zangu zimeisha huyu ni mtumishi wa Mungu aliye hai. sasa kama utaendelea kumnyooshea kidole mtumishi wa Mungu shori zako biblia inasema samweli-1 2-10 washindanao na Bwana watapondwa kabisa. ngoja niongee kitu kimoja kuusu watu wanaomtukana uyu mtumishi tena matusi ya nguoni! na kumdhiaki na kumbeza! Yesu alikaa na wanafunzi wake miaka ishiri na kitu! mpaka anaondoka na bado imani zao zilikuwa haba! sembuse wewe kwa binadamu mwenzako! kingine unaweza ukawa unafikiria ni sifa au mjanja kutukana watumishi wa Mungu kumbe....
 
kuwadhihaki kuwanyooshea kidole kumbe unatii mapepo ndani yako! binadamu yoyote bila ibilisi ameumbwa kumtii Mungu na sheria zake, wewe unafikiri ni wewe unayeongea kumbe ni mapepo ndani yako na wewe unafurahia! hujui ya kwamba icho kinachokuambia utukane au umseme mtumishi wa Mungu vibaya ni mapepo. ibilisi na wafuasi wake kasoro binadamu aliye hai wameshahukumia wanasubiri mda tuu wao hawana msamaha! ila binadamu anamsaha wa Mungu! ivyo wewe utahukumia na Mungu si sababu pepo limetukana ndani yako! au ibilisi ametumia mwili wako kutenda dhambi bali utahukumiwa sababu umemtii shetani! ivyo watch out vitu vya Mungu haviguswi wala havifanyiwi mzaha! ila kama bado unakiburi cha ibilisi wewe endelea litakalokukuta usirudi kuhadisia hapa!
 
unakosea. Mungu aliwapa wanawake unabii; ref. miriam, nabii debora. kasome kitabu cha wafalme kwa habari zake zaidi. ila huyu nabii wa gentamycine ni janga la kiroho. ni nabii ila ni nabii wa uongo.

Kwanini unasema ni nabii wa uongo? Any evidence?
 
"watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, wana masikio lkn hawasikii, macho lkn hawaoni, akili lkn hawafikiri' Kusema kweli nawaonea sana huruma hawa 'kondoo' wasiojua kuwa wao ni 'wateja'
 
Huwa najiuliza ni kwanini watu wapo so keen na kupata miujiza? Miujiza ipo ndani ya dhamira ya mtu , ukiomba na kuamini na kulifanyia kazi tatizo lako kwa udhati basi wewe mwenyewe utamualika Mungu kufanya miujiza kwako.

Sijui kizazi hiki kimekuwaje : Hamna tena mahubiri ya kukemea dhambi, kusisitiza utakatifu zaidi ni msusuru wa watu waliopata miujiza , magari, visa etc . Kila mtu na ajitafakari ni nini ultimate goal ya spiritual life yake? Hivi kweli na sober mind unaambiwa nunua stika weka chini ya mto , utafanikiwa? au watu wapo tooo desparate hata wakiambiwa lamba nyasi watafanya hivyo? Binafsi nadhani BAADHI ya wahubiri wana-take advantage ya desparation za watu +Ignorance na kujinufaisha wao.

Kwa huyu mama huitaji miwani kuona uchubuaji (japo sijasema ni dhambi) ila Biblia inatuonya Ole wao waletao makwazo kwa watu . Sasa kama watoto wetu tunawafundisha kutukuza uumbaji wa Mungu na kukubali rangi na ngozi zao leo si ni makwazo kuona muhubiri akiharibu hekalu la roho mt ambalo ni mwili wake? Kuna mtu kahoji umejuaje kama kajichubua? Seriously kwenye hizo picha hata kama si mwanasayansi huwezi kuona human intervention kwenye ngozi? au Mahaba yamezidi hadi kuleta upofu?

Mwisho: You and I have the power to create the miracles of our lives , its our decision whether we throw that power away or embrace it with Gods help.
 
Nakushauri uende mwenyewe ujionee..mengi yanaongewa kuhusu mausanii..ila wapo wanashuhuda..nakushauri popote utakapoenda kufuata maombezi..muombe mungu kwanza akuongoze na sio watu wakuongoze..na kama neno la mungu linavyosema amani ya kristo iamue ndani yenu..ukiona huna amani jua sio penyewe...angalizo ibada za kutumia maji, sabuni sijaona ufunuo ktt neno..ila mtu ukiamua kuamini hata udongo unafanya kazi ..kazi kwako!

Unajua tatizo watumishi wengi wamefikia hatua wanafanya Huduma km waganga wakienyeji....Hiyo habari yakufanya maombi kwa Simbo's ....ipo nainafanyakazi lkn Inatakiwa iwe kwa muongozo wa ROHO MTAKATIFU tuu...na Roho mtakatifu hawezi kukwambia ufanye jambo hilo hillo kila siku ....Kuna jamaa yangu alinialika kanisani kwake pale Sinza akaniambia Huyo mtumishi sio mchezo....Nikapata nafasi nikaenda hapo....Kilichonifanya nisitamani kurudi tena kule yule jamaa anatumia Mafuta kuwapaka....watu Usoni...pia kwenye Maombi anatumia Kuwamwagia watu Maji nilipowauliza waumini wa ile Huduma wanasema hiyo ndio style ya Kuomba kwa Huyo mtumishi....natena maji sio utoke nayo home Unayakuta pale kwakweli kwa namna nilivyofundishwa Roho Mtakatifu anavyofanyakazi Nimeamua kutokwenda kwenye hizo Huduma...za...watu..Tatizo kubwa watu wengi kwenye makanisa wanakotoka hawapati mafundisho yakutosha so wakiingia humo wanapokea bila kuzipima hizo Roho na tatizo kubwa watu wana matatizo mwakubwa yanayohusu Asili zakuzaliwa kwao so watu wanakwama sana
 
Neno langu likakaa kwa wingi ndani yenu ombeni chochote kwa jina langu nanyi mtapewa Tatizo watu hawataki kumtafuta Mungu wanatafuta miujiza mtaomba poo mtaangaika hadi mtaaingia mahali ambako si sahihi watumishi kumjua huyu ni wa MUngu au huyu msanii lazima uwe na macho ya rohoni
 
Neno langu likakaa kwa wingi ndani yenu ombeni chochote kwa jina langu nanyi mtapewa Tatizo watu hawataki kumtafuta Mungu wanatafuta miujiza mtaomba poo mtaangaika hadi mtaaingia mahali ambako si sahihi watumishi kumjua huyu ni wa MUngu au huyu msanii lazima uwe na macho ya rohoni

Ndio maana inasisitizwa watu walijie Neno ili wajiombee wenyewe kuna nyakati nikawa siamini km Hata Wewe ukilijua neno la MUNGU ukimuita anajibu maombi.....Binafsi baada yakupat mafundisho yakutosha nimelazimika kuwa na madhabahu Nyumbani kwangu nakwenda Kanisani kwaajili yakuongeza Ufahamu zaidi wakulijua NENO la MUNGU lkn MAOMBI nafanyia Nyumba na uwepo wa MUNGU unashuka ananijibu bila shida sasa tatizo watu hawataki kujifunza Neno wanategemea wengine wasome then wao wakaririshwe Kwanini wasilishwe matango pori
 
Hapo lazima Wale watango Pole ukilijua neno hata mtumishi akichemka unajua kabisa huyu kachemka lasivyo kila siku ukisikia tangazo la maombezi utaenda mwisho wake ni kuanza kuponda makanisa ya kilokole kwa sababu ya kukosa maarifa ukimpenda MUngu na kumtafuta kwa bidii kupitia neno lake atakufunulia mengi
 
Ndio maana watu wengi wanakata tamaa na dini. Sasa wewe na uchafu wote unaoandika hapa forum eti unasali kwa nabii halafu tena amekusaidia? Basi atakuwa ni Lusifa mwenyewe na wewe ni ibilisi

wewe ni nani mpaka umhukumu mwenzio? Usihukumu nawe utahukumiwa.
 
Back
Top Bottom