Nabii Askofu Mwingira agoma Kupima DNA, ni katika kesi ya kuzaa na mke wa mtu

Ni watumishi wangapi wamezaa na waamini wao na haikuleta noma?

Huyu Mwingira aongee na huyo Dr Moris issue ipotezewe. Haya mambo ya kuanikana mahakamani ni aibu.

Halafu nyie wamama/wadada mbona mnawasumbua hawa watumishi? Mtu unakuja church au vipindi vya maombi matiti chuchu saa 6 yanaelea nje unategemea rijali asikubutue?

Mara mkikaa mbele miguu mnapanua, mapaja yote nje huku chupi zenu za strings zinaonekana zikichora mstari kwenye kitumbua na kuacha milima miwili pembeni...mnategemea watumishi wasijisevie? Acheni hizo bana, ona sasa mnamtesa Nabii wa watu!!!
 
View attachment 655331
Heshima kwenu wakuu, Mahakani Kisutu: Askofu wa Makanisa ya Efatha Josephat Mwingira, amekataa katakata kupima DNA ili kutambua mtoto wa Dk. Phillis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. William Morris ni wa nani. Amedai hawezi kupima DNA wakati mtoto si wake.

Huyu Mwingira si ndio huyo huyo alikuwa na kesi ya kutembea na mke wa wakili mmoja maarufu hapa Dar aliyetaka kumnyang'anya zawadi ya kiwanja aliyompa kwa ajili ya kanisa baada ya kugundua kuwa alikuwa anatembea na mke wake? Nilisikitika kusikia kuwa yule wakili alishindwa ile kesi. Kiwanja alichotoa akakosa na mke akaliwa. Kweli si wote wasemao Bwana, Bwana....!
 
Unasema kweli mkuu !!!
1091410
 
View attachment 655331
Heshima kwenu wakuu,

Mahakani Kisutu: Askofu wa Makanisa ya Efatha Josephat Mwingira, amekataa katakata kupima DNA ili kutambua mtoto wa Dk. Phillis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. William Morris ni wa nani.

Amedai hawezi kupima DNA wakati mtoto si wake.

Baada ya Usikilizwaji wa kesi hiyo, Askofu Mwingira alipitishwa Mlango wa Nyuma kukwepa Kamera za Waandishi wa habari kinyume na Washitakiwa wengine ambao hupigishwa magoti mbele ya Camera.

Hapa ndo nashindwa kuelewa kwanini Mahakamani wanafanya mambo ya Upendeleo. Wengine Wanaruhusu wapigwe picha wengine wanakataza.

Ijumaa ya tarehe 15Dec 2017, Huyo mwanamke anayedaiwa kuzaa na Mwingira alitoa ushahidi wake. Alisema hajazaa na Mwingira wa Moris, bali alizaa na mfanyabiashara Mwingine tu.

MKE wa Dk. William Morris, Dk. Philis Nyimbi, anayedaiwa kuzaa na Nabii Josephat Mwingira, alikana mahakamani kwamba haujui mwili wa nabii huyo wala hajawahi kuzaa naye.

Anadai aliamua mwenyewe kuzaa mtoto na mfanyabiashara ambaye sasa ni marehemu na kwamba mtoto huyo si wa Nabii Mwingira wala Dk. Morris.

Dk. Nyimbi alitoa utetezi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini, kwa kuongozwa na Wakili wake, Peter Swai.

Alidai mwaka 2001 alifunga ndoa na Dk. Morris katika Kanisa la Mtakatifu Albano na walikaa mapumziko ya siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili alikoishi katika chumba kimoja akiwa kwenye mafunzo ya vitendo.

“Niliishi naye katika chumba kimoja kwa miezi mitatu, aliniahidi tutaenda kuishi Marekani lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda hakukuwa na safari, mwishowe nikaanza kuona aibu kwa madaktari wenzangu, kila wakikaa walikuwa wananiuliza naondoka lini.

“Nilipoona hatuondoki nikaona nimuulize safari yake ina tatizo gani akanieleza kuna tatizo la tiketi, nikamsaidia kumaliza tatizo hilo akafanikiwa kuondoka peke yake Februari, 2002, mimi nikabakia akasema nitamfuata tukaishi huko.

“Mawasiliano yalikuwa ya shida, nilichanganyikiwa sana, madaktari wenzangu walikuwa wakinihoji naondoka lini, nilikuwa nalia tu. Nmelinukuu Gazeti la Mtanzania

My Take:

Kama kweli Askofu hahusiki na kuzalisha Mke wa mtu, kwanini akatae kupima DNA? Mimi napendekeza apime ili kuondoa utata na kujisafisha kwenye Jamii inayomzunguka.

Habari zaidi soma=> Mchungaji Mwingira ashtakiwa, adaiwa kuzaa na mke wa raia wa Marekani

=======

NABII Josephat Mwingira amedai mahakamani kwamba hayuko tayari kupima kipimo cha DNA na hawezi kulipa fidia ya Sh bilioni saba kwa sababu hajawahi kuzaa wala kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Dk. William Morris.

Nabii Mwingira alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini alipokuwa akijitetea kuhusu madai dhidi yake kwamba alizini na kuzaa na Dk. Philis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. Morris.

“Sifanyi vitu ambavyo sihusiki, aliyebeba mimba ndiye anajua mtoto wa nani, amuulize mkewe mtoto kazaa na nani, uchungaji wangu ni wa Mungu, siwezi kusafishwa kwa DNA,” alidai.

Mahojiano ya Nabii Mwingira na Wakili Peter Swai aliyekuwa akimuongoza kutoa utetezi wake yalikuwa kama ifuatavyo:

Swali: Tuambie cheo chako ni nani?

Jibu: Cheo cha kiroho ni Nabii na Mtume.

Swali: Unafanya mahuburi wapi?

Jibu: Efatha.

Swali: Unamfahamu Dk. Philis na Dk. Morris?

Jibu: Nawahafamu wote, ni mtu na muewe, walikuwa washiriki wa kituoni kwangu Efatha, Dk. Nyimbi ni mtoto wa nyumbani, nilisoma na kaka zake, majirani kijijini kwetu.

Swali: Mnatokea kijiji gani?

Jibu: Tunatokea Kijiji cha Mbaha wilayani Nyasa.

Swali: Kuna siku ambayo Dk. Morris alikuwa na ombi lolote kwako?

Jibu: Walikuja na mkewe kuomba msaada wa fedha kwa ajili ya kununua vitu katika mnada bandarini?

Swali: Shilingi ngapi?

Jibu: Ni zaidi ya Sh milioni 16, niliwapa kutoka katika akaunti ya Efatha, lakini mpaka leo hawajarudisha.

Swali: Hivyo vitu uliviona?

Jibu: Niliviona, ni kama vile vitu vinavyookotwa Marekani, nilishangaa anasafirisha takataka kutoka Marekani mpaka huku.

Swali: Ulishawahi kufuatwa na Morris kukulalamikia kwamba una mahusiano ya kimapenzi na mkewe?

Jibu: Ha ha ha ha, hapana.

Swali: Unafahamu kwamba Dk. Nyimbi ana mtoto?

Jibu: Nafahamu.

Swali: Kuna siku hata moja aliwahi kukwambia baba wa huyo mtoto?

Jibu: Hapana hatujawahi kuongelea kitu kama hicho.

Swali: Ulishawahi kuhusishwa katika mgogoro wa mtoto wa Dk. Nyimbi?

Jibu: Kwani Morris anasema mtoto sio wake?

Swali: Kuna tuhuma hapa, Morris anadai yule mtoto umezaa na Dk. Nyimbi.

Jibu: Niliwahi kusoma katika magazeti, sijawahi kuletewa mtoto, lakini nikiletewa nitalea.

Swali: Inasemekena wewe ulishiriki katika kikao cha familia kilichotambua mtoto ni wako.

Jibu: Hapana.

Swali: Kuna madai hapa mahakamani, Morris anaomba umlipe fidia ya Sh bilioni saba kwa kuwa na mahusiano na mkewe, unasemaje?

Jibu: Tunaanzaje? Unapolipa lazima uwe umetumia kile kitu, hilo jambo halipo.

Swali: Unazungumziaje madai yaliyopo mahakamani?

Jibu: Kama hii mahakama inatenda haki, itaangalia kwa haki, Dk Morris atalipa gharama za kunisumbua.

Swai alimaliza kumwongoza mteja wake na mahakama ikatoa nafasi kwa Wakili wa mlalamikaji, Respicius Ishengoma kumuhoji maswali.

Swali: Naomba nikuite Mchungaji?

Jibu: Umetoa wapi hilo jina?

Swali: Nini tofauti ya Mchungaji na Nabii?

Jibu: Mchungaji na Nabii ni tofauti sana, kama ukisema hakimu na wakili, huoni tofauti? Kila mmoja ana kazi yake.

Swali: Ndiyo maana nimekuuliza kutaka kujua tofauti.

Jibu: Mimi nahubiri injili, sifanyi kazi moja tu ya kuchunga, ila nina wachungaji chini yangu.

Swali: Una watoto wangapi?

Jibu: Nina watoto sita, lakini mmoja marehemu.

Swali: Wataja majina.

Jibu: Lucy, Joshua, Anna, Jonath na Glory.

Swali: Glory alizaliwa lini?

Jibu: Alizaliwa 2007.

Swali: Nikisema kazaliwa Mei 22 mwaka 2007 utakubaliana na mimi?

Jibu: Mimi niliyemzaa sikumbuki, wewe unatoa wapi? Alikuambia nani? Mimi siwezi kusema nakubaliana na wewe.

Swali: Unakumbuka mlifanya sherehe ya kupongeza kuzaliwa kwa Glory Mei 22 mwaka huo na ukampeleka Dk. Nyimbi Hoteli ya Millenium Tower?

Chanzo: Mtanzania

Ile bank ya Efatha iliishia wapi? Waliowekeza amewarudishia hela zao?

Hizo mali za bilioni 10 anaweza kuonyesha zimepatikanaje?
 
wewe nabii wewe!!si ukubali kupima umalize utata!!?Kama unagoma basi ni kweli ulimtafuna mke wa mtu!!!
 
Kampiga Mchungaji Kondoo wametawanyika.
Kamwaga petrol kwenye shimo vitoto vya Nyoka vinakimbia bila uelekeo.
Injili ni kitu cha ajabu sana. Nobody in this world can compromise. Mtu muongo ndio atoe laana? Si ndio uongo huo huo?
 
Back
Top Bottom