Naapa kuwa sirudii tena kumsaidia Mtanzania -- never!

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,800
2,000
Habar zenu ndugu zangu. Ama baada ya salam ningependa kuendelea na kile kilichonifanya niandike uzi huu. Ndugu zangu kama ilivyo ada au kama tulivyofunzwa na misingi yetu ya Taifa kwamba watanzania popote tulipo haijalishi ni ndani au nje ya nchi, sisi ni watu wamoja. Kwahiyo kwa misingi hiyo sisi tulio nje huwa na desturi au utamaduni wa kusaidiana bila kujali tofauti zetu za kikabila, dini, rangi, jinsia au kanda ya mtu anayotokea ilimradi sote ni watanzania na tunatokea kwenye ardhi ya Tanzania basi ni ndugu.

Sasa basi miezi 3 iliyopita kuna kijana aliingia Kaburu akitokea bongo kwa lengo la kuja kutafuta maisha. Kijana anadai kuna rafiki yake wa kitaa, kwa sasa anaeishi Capetown ndio alimshawishi kuja maisha haya, lkn alipoingia tu "Kaburu" yule rafiki yake akamzimia simu na kumkosa kabisa online.

Kijana akachanganyikiwa asijue wapi pakwenda wala nini cha kufanya. Nikiwa katika mizunguko yangu mitaa ya park station Johannesburg, ghafla nikapita sehem na kumuona kijana akiwa kajiinamia na begi lake huku machozi yakimtoka. Nikamsogelea taratibu na kujaribu kumuuliza kwa lugha ya wenyeji, ghafla nikasikia jamaa akiongea kiswahili, hii ikanipa nguvu ya kumsogelea na kumuuliza zaidi baada ya kugundua kuwa naongea na mtu anaetoka nchini kwetu. Baada ya maongezi ya hapa na pale nikagundua kuwa jamaa ameingizwa cha kike na mwenyeji wake, kwahiyo nikachukua jukumu la kumsaidia.

Nikaondoka na jamaa hadi nyumban, akaoga, akala, baada ya kula nikampa sehem ya kupumzika akalala. Kwa kuwa mimi nina familia ikanibidi niende kuongea na homeboy fulan ambae ni single ili ampe hifadhi ya miezi kadhaa wakati nikiendelea na mchakato wa kumtafutia shughuli ya kufanya, mshikaji akakubali lkn kwa masharti ya kumsaidia kulipa rent.

Kwa kuwa nilikuwa nimeamua kumsaidia kijana, basi nikaona poa tu acha nimsadie kulipa rent ili aweze kuishi nae. Kijana tumekaa nae mwezi wa kwanza, wa pili na sometimes nilikuwa naenda nae kwenye mishe zangu ili kumzoesha mazingira ya nchi, na mishe za hapa na pale. Mwezi mmoja uliopita kuna rafiki angu Mkenya ambae tuliwahi kufanya nae kazi huko Gezina, Pretoria.

Mkenya alikuwa anatafuta mtu wa kumuachia saluni yake kubwa na ya kisasa iliyopo nje kidogo ya jiji la Pretoria huko Nellmapius, kwa malipo ya R600 kwa week (sawa na sh elfu 85 au elf 90) kula na kulala bure. Kwa vile nilikuwa na kijana na tayari alishanambia kuwa bongo kazi yake kubwa ilikuwa ni ukinyozi, nikaona YES maji ya mvua yameangukia juu ya mgongo wa bata. Nikampanga kijana, kesho yake mapema nikampeleka mpaka Pretoria kwa yule Mkenya na kumkabidhi.

Kweli bwana baada ya siku mbili kijana akaanza kazi huku Mkenya akiniomba nimtafutie vijana wengine ambao wataenda kusaidizana nae, maana saluni ni kubwa ilihitaji vinyozi zaidi ya watano, lkn pia kijana lugha ni tatizo, so alitaka ambao wangeweza pia kusaidiana hata katika mambo ya lugha za wenyeji ili kuwateka vizuri wateja wa kizawa.

Nikamuahidi jamaa kumtafutia hao vijana. Wakati namuacha kwa yule Mkenya kijana wang nilimuachia sim kwa ajili ya mawasiliano yetu, au ndugu zake wa bongo, au boss wake (Mkenya). Dogo tukawa tunawasiliana ananipa taarifa za kazi na mimi nampa mpa moyo kuwa akomae ili atimize malengo ya kile kilichomleta hapa nk. Siku tatu zilizopita sikumpata online, nikajua labda simu imepata tatizo ghafla.

Sasa jana yule rafiki angu Mkenya amenipigia simu na kuniambia kuwa jamaa amemuibia kila kitu cha saluni, na hela ambazo yule Mkenya anaendaga kuzichukua kwa week jamaa katimka nazo. Simu yake haipiti na hatujui tutamtoa wapi. Nilipotaka kumlipa yule Mkenya nusu ya hasara ya vitu alivyoiba jamaa, Mkenya amkataa amesema nisijali kwa vile sio kosa langu ni kosa la mtu mungine kwahiyo mimi sistahili kumlipa na ukizingatia na rafiki yangu.

Hiki kitendo cha huyu jamaa kimenisononesha na kunivunja nguvu. Imenifanya sasa niwachukie wabongo wenzangu, maana hii ni mara pili sasa nawasaidia wabongo afu wanaharibu na kutimkia kusikojulikana, japo kwa huyu sikutegemea hata kidogo kutokana na upole na muonekano wake.

Najua binadamu tunatakiwa tusamehe, lkn kwa mikasa hii sioni sababu ya kusamehe kwa lengo la kurudi kumsaidia mungine labda yule nimjuae A to Z. Ndugu zangu wabongo tubadilike, hii dunia tunapita tu. Kumuharibia mtu anaekusaidia sio ujanja bali ni ujinga wa mwisho. Hii ni tahadhari nimetoa kwa vijana wengine kuwa makini sana. Asanteni
 

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,932
2,000
Honestly speaking waTanzania wengi wanapenda shortcut

Siyo kwenye kazi
Kwenye biashara
Mpaka kwenye mambo ya kijamii

Kuna mmoja nilimpeleka godown fulani akapiga mzigo imekuja julikana too late na deni nikalibeba

Mimi nikisikia opportunity nakausha tu kuepuka lawama. Kisha utasikia waTanzania hatupendani.
 

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,197
2,000
Pole sana mkuu. Ndiyo maana hata nyumbani huku tunaambiwa hatuaminiki kwasababu ya wachache kama hao.

Unaweza kusaidia ila kwa namna ambayo haitokuathiri wewe ikitokea kama hivi.

Yaani rafiki yako wa karibu, ndugu au mtu wako uliye na ukaribu naye sana usimkabidhi mtu usiyemfahamu kiundani kwa lengo la kumsaidia ili ikitokea kama hivi unaelewa ni wapi pa kuanzia.
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,816
2,000
Imagine, wakenya ni mabingwa wa wizi lakini wakimwona mbongo huko Kenya hasa wachagga wanamwogopa balaa maana wanajua kupigwa ni nje nje.
Mkuu hivi Mbowe, Chadema na wachaga waliwakosea nini? Umetoka kula ban kwa huu huu upuuz wako. Tena unarudia. Hizi viporo vya kande iliyochacha unavyofakamia na kuparamia utaacha lini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom