Naanza kutumia huu msemo wa kiswahili kwa fujo niwe milionea

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,183
13,611
Mzuqa

Huu msemo wa kiswahili maneno huumba nataka sasa hivi nijikite nao katika harakati zangu za kutafuta hela ndefu sana ili kuleta heshima kwenye jamii and to leave an everlasting legacy.

Japo huu msemo umejikita zaidi kwenye mambo hasi ila nitaulazimisha tu ulete mambo chanya.

Sasa kwaanzia sasa iwe kwa sauti ama kimoyomoyo nitakuwa kila wakati natamka nataka kuwa milionea nataka kuwa milionea nataka kuwa milionea hadi kitu kieleweke maamaee.

Nitatumia mbinu zote hadi njozi zangu za ushindi zitimie.

Wanaume tutafute hela tuu hamna namna.

MANENO HUUMBA!
 
Maneno Pekee bila kuchukua hatua madhubuti za kukufikisha unakotaka kwenda UTASUBIRI SANA sheikh wangu..nikushauri tu kama una shughuli zozote za kufanya ww uendelee nazo vinginevyo ni sawa na kusubiri treni sheli...

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
 
Usikate tamaa pambana utatoboa
Namimi nafuata nyayo zako

Kwenye safari ya mafanikio
 
Naona umeshiba dona na mlenda uliochacha sasa unaanza kuota ndoto nyevu.
Vip jackpot inasemaje?
Aiseee chalii yangu hapana nashindiliaga tu kiporo cha kande iliyochacha na chapati za msituni.

Jackpot bado ipo ila siyo kwa sana pamoja na mbinu zingine za kutafuta hela ndefu kuroga, kuiba, kufisidi, kutapeli, kuhadaa, maombi ya kujiunga na Freemason (application still pending) , kudanganya, kufuja, kughushi na kufanya kazi.

Sasa leo nimeanza na hii maneno huumba, kila siku nakuja na mbinu mpya hadi kieleweke maamaee!
 
Fanya kazi kwa bidii dingilai halafu punguza kula totoz.
ONE DAY YES.
 
Mzuqa

Huu msemo wa kiswahili maneno huumba nataka sasa hivi nijikite nao katika harakati zangu za kutafuta hela ndefu sana ili kuleta heshima kwenye jamii and to leave an everlasting legacy.

Japo huu msemo umejikita zaidi kwenye mambo hasi ila nitaulazimisha tu ulete mambo chanya.

Sasa kwaanzia sasa iwe kwa sauti ama kimoyomoyo nitakuwa kila wakati natamka nataka kuwa milionea nataka kuwa milionea nataka kuwa milionea hadi kitu kieleweke maamaee.

Nitatumia mbinu zote hadi njozi zangu za ushindi zitimie.

Wanaume tutafute hela tuu hamna namna.

MANENO HUUMBA!
Utaishia jela Tena segerea, Kaka magu Yuko madarakani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom