Naanza kupata wasiwasi kwa kila rais wa Afrika anayeungwa mkono na nchi za magharibi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naanza kupata wasiwasi kwa kila rais wa Afrika anayeungwa mkono na nchi za magharibi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gosbertgoodluck, Mar 31, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nimeangalia kinachoendelea Libya nikalinganisha na Ivory Coast, Somalia na maeneo mengine ya Afrika na kubaini namna nchi za magharibi zilivyo substandard katika kushughulikia migogolo ya nchi. Inavyoonekana, kinachotazamwa na hawa wababe wa Dunia siyo usalama wa raia wa nchi husika bali ni usalama wa raia wao kiuchumi. Kwa maneno mengine, kiongozi yeyote anayeungwa mkono na wababe hao lazima watakuwa na uhakika nae kuwa atawapatia ushirikiano katika jitihada zao za kupata maslahi kwa ajili ya ustawi wa nchi zao. Waafrika tuwe macho. Vinginevyo, tutaangamizwa na viongozi vibaraka wanaozipigia magoti nchi za magharibi.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  Nani anasema wazungu wapo kwa ajiri ya kuwasaidia waafrika? Katu ,na wala haitatokea, kama anakusaidia basi ujue zaidi ya 65% inakuwa ni kwa masrahi yake binafsi kwenye ilo jambo husika ...in a capitalist world there is no free service at all,every single coin counts..!
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu vizuri kama umelitambua hilo, nadhani uchangiaji wako wa kama siku tano au nne zimepita ulikuwa mstari wa mbele kushangilia, Marekani na Ufaransa kuipiga Libya. ni vizuri kama umetambua hilo. nchi za Ulaya na Marekani huwa zipo kimaslahi zaidi
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ndugu ulikuwa hujui kuwa hao mabeberu huwa hawana permanent friends but they have permanent allies? Ukiona wanamshangilia kiongozi yeyote wa Afrika ujue kama si kuhomola madini ya nchi husika basi ni mafuta na kama si hayo basi ujue ni misitu. Mabeberu siku zote wanaangalia maliasili ya Afrika kama Urani, dhahabu, almasi, magogo ya mbao, n.k. Kiongozi akionyesha dalili za kujikomboa kutoka katika makucha yao basi anaonekana audi mara moja. Utasikia wanaenda UN kuomba Azimio ili kuitumia UN kama kichaka cha kutekeleza maovu yao ili wamuangamize huyo kiongozi na kuweka vibaraka wao.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  R U serious about Libya? that the president is good? what Somalia western world support? oh yeah Qattara won
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Una ujumbe sawa na huyu muzee hapa.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ifike wakati tuache kuwalaumu ulaya na USA, na kabla hatujafika huko, hivi viongozi wa Afrika wanafanya nini cha maana kutatua migogoro hii, kuanzia Sudan, somalia Ivory Coast, Libua n.k? Hawa jamaa wataendelea kututia adabu huku tena wakifurahia ili WAHOMoLE madini na mafuta yetu, si wanatufanyia majukumu yetu ya AU, na wanaangalia na maslahi kudadadeki! Tatizo letu Afrika hatuach ujinga wetu wa utawala mbovu yaani viongozi wote wanaoneana noma maana kiLa mmoja ana uchafu wake, tena itafika siku wazungu watasema kwa kuwa waafrika mnaonekana kujitawala hamuwezi hebu tuachieni nchi zenu tuwatawale hadi mtakapoweza kujitawala wenyewe!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni Vizuri Kesi Zote Zitaletwa Mjini Arusha, Tanzania - kwahiyo tuna Uwezo wa kuangalia Usawa wake

  1. Ghadaffi anauwa Wananchi Wa Libya -- Kesi Itasikilizwa Mjini Arusha - Makao ya African Court
  2. Gagbo kesi ya kung'ang'ania Madaraka -- bado haijaamuliwa lakini wanaelekea kuipeleka Arusha
  3. Kesi ya Uchaguzi na Uuaji Kenya--- Kesi inakwenda Mjini Arusha
  4. Maaramia wa Kisomali baharini --- kesi inakwenda Mjini Arusha

  Kwahiyo Mtaona hii ni faida ya Mataifa ya Magharibi au Ni faida ya Damu zinazouawa na Marais wanaopenda Madaraka wa Kiafrika
  Aibu naona wote nyie mtapenda CCM ikao kwa Karne na Ufisadi.
   
Loading...