Naanza kuiona Tanzania iliyobadilika. Watanzania hawasikilizi propaganda za uongo za Wapinzani

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Watanzania sio wajinga, ukija na hoja za kitoto wanakusikiliza kisa wanapima unachosema.

Hakuna ubishi kuwa upinzani hapa Tanzani ulipata nguvu sababu ya makosa ya Ccm kama chama tawala kuruhusu ufisadi.

Nani asiyekumbuka kuwa Lyatonga Mrema alipata kiki baada ya kuibua ufisadi wa mfanyabiashara Chavda.Mrema akapata kick na kuwa kama mkombozi. Chadema ya Dk Slaa ilisifika kwa kuibua madudu ambayo ndio yamesababisha Ccm ijirekebishe.

Hivi yapata miaka 29 tangu tuingie kwenye siasa za vyama vingi,watanzania wanajua kupima hoja zipi zina mashiko na zipi hazina mashiko. Hivyo sio wakati wa kuburutwa na wapinzani kwa propaganda ambazo hazina mashiko.

Kipindi hiki ambacho ufisadi umebinywa na kila mtanzania anaona maendeleo yanavyofanyika nchini sio rahisi kumshawishi mtu kuwa diversification of economic development haifanyiki hapa Tanzania.

Hivi ninyi wapinzani mnaweza kushawishi umma kuwa sasa maendeleo yapo centralized eneo moja? Kwa kigezo kipi?

Mbona kila mtanzania anajua,sasa hamna hoja. Sababu hoja ya ufisadi iliyokuwa inawabeba haipo. Sasa mnataka kueneza uongo kuwa kuna upendeleo katika kutekeleza miradi ya kimkakati. Hivi mnadhani Watanzania watawaelewa?
 
20210114_095203.jpg

Tusio watanzania
 
Watanzania sio wajinga,ukija na hoja za kitoto wanakusikiliza kisa wanapima unachosema...
chagu wa malunde , CCM imeshinda kwa kumwaga damu, kura feki na kupindua matokeo.
Kama CCM inajiamini zile kauli za kwamba nitamfukuza kazi mkurugenzi atakaye tangaza Mshindi mtu wa upinzani zilitokea wapi?

Wekeni tume huru ya haki na wazi ya uchaguzi muone mnavyobwagwa mapemaaaaaaaa
 
chagu wa malunde , CCM imeshinda kwa kumwaga damu, kura feki na kupindua matokeo...
Inaingia akilini kudai tume sio huru? Hivi kama upinzani umeshinda unadhani kuna mtu wa kupindua matokeo mbele ya nguvu ya umma?

Hakuna hoka za msingi kuibana Ccm ili wananchi waikatae bali mmebakiza propaganda za kizushi kama mnazoeneza sasa hivi kuwa maendeleo yanapelekwa sehemu moja.
 
Kama maendeleo hayapelekwi sehemu moja, Basi linganisha maendeleo ya Kisarawe na yale ya ardhi takatifu Chato.

Kisarawe na Nairobi zote zilianzishwa siku moja, zote zikiwa wilaya.

Chato imeanzisha miaka ya katikati ya 90 lakini angalia maendeleo yake ya kuanzia 2015 hadi leo.
 
Uwezo mdogo wa kug'mua mambo. Kipi kimekutusha kuhusu Chato? Hii Hospital iliyojengwa?
Nairobi unaweka hadhi sawa na Kisarawe?
 
Uwezo mdogo wa kug'mua mambo. Kipi kimekutusha kuhusu Chato? Hii Hospital iliyojengwa?
Nairobi unaweka hadhi sawa na Kisarawe?

Airport kubwa kama ya Dar, kuwa kitovu cha utalii kanda ya ziwa, Mbuga ya wanayama ya kutengeneza, uwanja mkubwa wa mpira, chuo kikubwa cha ufundi cha veta, bohari kubwa ya dawa ya (MSD)
 
Kuna vituko duniani hapa!

Eti Lisu nae alitaka awe rais!

Kule Uganda nako eti Bob anataka kuwa rais,!
Ati raisi MAGUFULI aliwauzia nyumba za umma hawala zake kina KABULA yule wa kebys Nate leo anajiita mzalendo?
Ati MAGUFULI alinunua magorofa mawili ya NIC huko dodoma kwa ml 6 kila moja na kwa mkopo lakini hayaonekani popote kwenye Mali zake?
 
Mlituaminisha kuwa wapinzani wanachelewesha maendeleo, kwenye uchaguzi mkapindua meza mkajipa ushindi majimbo na kata zote. Ajabu miezi mitatu imepita bado mnawaota wapinzani. Tunataka maendeleo hatutaki porojo
 
Mvua zinanyesa huku wilayani Kakonko,tunakunywa tope si maji tena!

Tukisikia yanayofanyika Chato, hata yale yasiyo na umuhimu tunaona ni wazi watu wa Kigoma hatuna thamani kabisa!
 
Back
Top Bottom