Naanza kugundua kwanini nchi nyingi walipata marais mwanzoni wakawashangilia, ila muda ulivyopita wakaanza kupingwa na kuwa madikteta

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,635
29,967
Nikiagalia pale Rwanda pale, walimshangilia Kagame kwa kupata mkombozi safi,
Uganda wakafika hatua wakasema Hakuna kama Mseveni kwa meizi ile 50 ya mwanzo lakin muda huu unaoana kinachoendelea,

Nikagundua kwamba mara nyingi wapiga kura tunakuwa hatujapata muda wa kutosha wa kudadisi anayoyasema mgombea,
Pili tunakua hatujajua sana tabia yake ya binafsi nje ya uongozi,
Tatu tunashindwaga kuukemea unafiki wa wenzetu wapiga kura kwa kuwa ama ni wanufaika wa mfumo au ni wale wanaoogopa kwa uoga tu,

Juzi Algeria wananchi waliandamana mtaani kumpiga rais yule yule ambaye waliwahi kumuona mkombozi wao mwanzoni anaingia, na mbaya zaid pamoja na kwamba kuna uchaguzi huko Algeria wananchi hawana imani na tume ya uchaguzi , jana wameendelea kuandamana wakishinikiza jina la Rais wa sasa lisiendelee kuwapo katika lista ya wagombea, hii imenifikirisha sana kwamba kumbe nao wanakuwa hawana imani sana na tume yao ya uchaguzi maana wangekuwa na imani nayo si wangesubiri siku ya kupiga kura wasimpigie?

Matatizo au dalili ambazo upekekea wananchi waanze kuichoka serikali au rais waliyemwamini ni hizi
1.Kukosa ajira na huku waliahidiwa ajira, tunajua ajira si lazima zitolewe na serikali, ila serikali iweke utaratibu bora wa kuwezesha ajira za kuajiriwa na ajira binafsi,

2.Kukamuliwa sana wananchi kupitia kodi zisizo kuwa na mpangilio,

3.Kuona mauaji na upoteaji wa wenzao kwa kutekwa bila majibu ya kuridhisha

4. Chuki binafsi ya serikali dhidi ya wawekezaji wa mashirika binafsi na kuwakomoa

5.Kutunga tunga sheria ambazo hazina mpangilio kila siku ni kumtisha mwananchi wa kawaida badala ya kumfariji

NAWATAKIA UBEBAJI MWEMA WA MABOX VICHWANI MUWAPO KWENYE MABASI YA USAFIRI

USIKOSE KUFUATA MAAGIZO YA SERIKALI KWENYE KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI,

USIJE UKAMPA TENDA MTU AMBAYE SI WAKALA WA SERIKALI
 
Duuuuu!! Naona leo kinyonga umerudi kwenye akili iliyotulia.....

Kwa kifupi hilo ulilosema linaikumba nchi nyingi za kiafrica hata hao akina museven uliowataja walichokwa na wananchi baada ya miaka 10 ya uongozi wao lakini huyu wa kwetu ndani ya miaka 3 wananchi hawamtaki hata kumsikia,
Kila siku zinatungwa sheria ili kumkandamiza mwananchi je ndani ya miaka 5 ijayo TANZANIA hii itakuaje??
 
Ilivyo ni kwamba hata dikteta hua na watu wanaomsapoti anachokifanya. Watu wengine kwa kutaka kujipendekeza hutunga sheria au taratibu ambazo humtukuza zaidi kiongozi husika.

Wakati mwingine utakuta hata huyo kiongozi hajui na wala hakutaka ziwekwe taratibu za kumfanya awe Mungu Mtu hua anashtuka tu kujua kua siku hizi watu wanatakiwa kupiga magoti wakiongea naye.

Mfano Hitler, afisa mmoja kwa kutaka kujipendekeza akabadili kiapo cha wafanyakazi wa Umma badala ya kuapa kuitumikia Ujerumani wakawa wanaapa kua watamtumikia Hitler. Na Hitler hakujua kama kuna huu mpango.
 
Hapo namba 1 na 2 ni hatari zaidi, lakini nadhani ni mfumo uliopo katika vyama cha siasa, yaan wao wanatuletea mtu ili tumchague hivyo hakuna namna kwamba wale waliongia katika kinyanganyiro lazima mmoja wapo achagulie
Wananchi wananyima fursa ya kumjua mtu huyo, akiingia madarakani ndo tunajua ana rangi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu umeona dalili gani za kulegea kwangu?
Uzi wako unaeleza taabu tunazozipata kutokana na kukosekana kwa tume huru. Pia umegusia misingi ya utawara bora has a katika mgawanyo wa majukumu kati ya serikali, bunge na mahakama. Nimeona umelegea kwa kuona ni sawa na bure kuunga mkono juhudi katika hari yetu ya umateka chini ya wanasiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YES

Sure
Hapo namba 1 na 2 ni hatari zaidi, lakini nadhani ni mfumo uliopo katika vyama cha siasa, yaan wao wanatuletea mtu ili tumchague hivyo hakuna namna kwamba wale waliongia katika kinyanganyiro lazima mmoja wapo achagulie
Wananchi wananyima fursa ya kumjua mtu huyo, akiingia madarakani ndo tunajua ana rangi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe Britanicca ni moja kati ya hazina muhimu sana pale Lumumba. Siku za karibuni umekua na mada zenye mashiko tofauti na pale mwanzo, kiasi kwamba baadhi ya wenzako watahisi umenunuliwa na mabeberu.

Hebu utuambie, umepatwa na nini hadi kuwa critical kiasi hiki? wakati ndugu zako akina Jingalao, Magonjwa Mtambuka, et al; bado wanaendelea kuzipongeza, kuzitukuza na kuzienzi juhudi? Hongera sana kwa kuwa muwazi na mkweli.
 
mkuu unajua tatizo mtu asiamamye kwenye ukweli utukanwa hadi saa nyigine uonekana mpuuzi, kuna kipindi CHADEMA wakifanya mafyongo tunaongea kweli kabisa bila kupepesa macho sasa wale wafuasi wa CHADEMA Wa ufipa waanza mambo ya umeshachukua buku saba yako, sijui nini, wakati unausema ukweli,

Ukiusema upande wa chama tawala utaambiwa nyie ndo mmetumbuliwa, mara mianya imezibwa nakaa kucheka tu
 
Africans politicians

1.Wote wana lugha moja tu
2.Wanatumia shida za watu kupata madaraka
3.Wote si wazalendo kama wanavyojinasibu iwe ni toka vyama tawala au upinzani,wote nikwamaslahi binafsi
4.Wanabadirika soon baada ya kupata madaraka
5.Divide rule kama wakoloni tu
6.Hawapendi kukosolewa
7.Wanafiki
 
Sisi tulioishi kipindi cha utawala wa Stalin, tuliona mengi katika kipindi kile cha 'THE GREAT PURGE' tunaomba hayo tuliyoyapitia kipindi hicho yasijitokeze hapa. Nyi puha nyi pera k chortu.
 
Nikiagalia pale Rwanda pale, walimshangilia Kagame kwa kupata mkombozi safi,
Uganda wakafika hatua wakasema Hakuna kama Mseveni kwa meizi ile 50 ya mwanzo lakin muda huu unaoana kinachoendelea,

Nikagundua kwamba mara nyingi wapiga kura tunakuwa hatujapata muda wa kutosha wa kudadisi anayoyasema mgombea,
Pili tunakua hatujajua sana tabia yake ya binafsi nje ya uongozi,
Tatu tunashindwaga kuukemea unafiki wa wenzetu wapiga kura kwa kuwa ama ni wanufaika wa mfumo au ni wale wanaoogopa kwa uoga tu,

Juzi Algeria wananchi waliandamana mtaani kumpiga rais yule yule ambaye waliwahi kumuona mkombozi wao mwanzoni anaingia, na mbaya zaid pamoja na kwamba kuna uchaguzi huko Algeria wananchi hawana imani na tume ya uchaguzi , jana wameendelea kuandamana wakishinikiza jina la Rais wa sasa lisiendelee kuwapo katika lista ya wagombea, hii imenifikirisha sana kwamba kumbe nao wanakuwa hawana imani sana na tume yao ya uchaguzi maana wangekuwa na imani nayo si wangesubiri siku ya kupiga kura wasimpigie?

Matatizo au dalili ambazo upekekea wananchi waanze kuichoka serikali au rais waliyemwamini ni hizi
1.Kukosa ajira na huku waliahidiwa ajira, tunajua ajira si lazima zitolewe na serikali, ila serikali iweke utaratibu bora wa kuwezesha ajira za kuajiriwa na ajira binafsi,

2.Kukamuliwa sana wananchi kupitia kodi zisizo kuwa na mpangilio,

3.Kuona mauaji na upoteaji wa wenzao kwa kutekwa bila majibu ya kuridhisha

4. Chuki binafsi ya serikali dhidi ya wawekezaji wa mashirika binafsi na kuwakomoa

5.Kutunga tunga sheria ambazo hazina mpangilio kila siku ni kumtisha mwananchi wa kawaida badala ya kumfariji

NAWATAKIA UBEBAJI MWEMA WA MABOX VICHWANI MUWAPO KWENYE MABASI YA USAFIRI

USIKOSE KUFUATA MAAGIZO YA SERIKALI KWENYE KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI,

USIJE UKAMPA TENDA MTU AMBAYE SI WAKALA WA SERIKALI
Mkuu kwa comment zako za nyuma inaonekana kama vile ulikuwa UNAUNGA MKONO JUHUDI, lakini kwa comment zako za hivi karibuni, naona UNAPINGA JUHUDI ZA MHESHIMIWA SANA HIS EXCELLENCY HIS MAJESTY THE MOST DISTINGUISHED LEARNED BROTHER LEADER DR PROFESSOR ENGINEER ASTRONAUT FIELD MARSHALL JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI ESQUIRE?
chunga sana!!
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom