Ama kweli majirani zetu wa kenya wapo katika kipindi kigumu sana kuelekea uchaguzi mkuu, naangalia willium rutto aliyoingizwa mkenge na tajiri wa kutupwa uhuru kenyata na wao kutengeneza muungano wao.Ukiangalia sura ya kenyatta pale nakuru leo ni wazi kabisa na macho yake wanajiandaa kuififisha nyota ya kenya kwa ukabila.Sioni hoja yeyote wanayojenga zaidi ya maslahi ya kikabila.Kenya ikichafuka tena, Tanzania haitakuwa salama katika kuelekea 2015 na unaweza kuwa mwanzo wa machafuko ya kudumu katika eneo la Afrika mashariki ukizingatia kuwa wanaowania urais huko kenya wana mafungamano na viongozi kadhaa wa kisiasa hapa Tanzania katika vyama vyote vya siasa ( upinzani na chama tawala)