Naamini wapo Watanzania wameenda kuchanjwa au wamechanjwa kimyakimya maana uhai Ni suala binafsi.

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mjadala wa chanjo ya Corona una msimamo wa nchi na msimamo wa mtu binafsi.

Nchi haifi lakini mtu mmoja mmoja anakufa aidha kwa mapenzi ya Mwenyenzi MUngu au kwa kutotimia maarifa aliyopewa na Mwenyenzi MUngu.

Kama chanjo hiyo inaonekana inafanya kazi na watu wanaamini inafanya kazi haiwekani ikawa baadhi ya watu hasa wenye uwezo au wanaosafiri nje wakawa wanajichanja bila kuutangazia umma?

Lakini pia ugonjwa huu unagusa zaidi uhai wa watu wenye umri mkubwa na wale wenye changamoto za kiafya, kundi hili litaathirikaje na chanjo hiyo wakati wapo kwenye risk tayari?

Haiwezekani viongozi wengine wanaopuuza kuvaa barakoa na kukataa kuchukua taadhari wakawa wameshachanjwa?

Uhai siku zote ni Jambo binafsi hivyo nafungua mjadala binafsi baada ya mjadala wakitaifa kufungwa kwamba nchi yetu haikubaliani na chanjo ya Corona.
 
Ile ya Astrazeneca, ile ya urusi labda na ile ya china ndo naweza kusema ni chanjo kutokana na aina ta teknolojia iliyotumika kutengeza hizo chanjo, lakini hizi wanazoita Pfizer na Moderna ambazo zinaitwa mRNA vaccines bado hawajanishawishi kuanza kutumika haraka namna hiyo, bado zitahitaji utafiti na majaribio ya muda mrefu...
 
Duh... Kumbe tuna wataalam hapa Bongo. Kwanini tusitengeneze zakwetu.
 
1613756066605.png
 
Fanya utafiti halafu lete taarifa za kueleweka, sio kujaza nyuzi zisizo na kichwa.
 
Back
Top Bottom