Naamini "waasi" ndio wanaopenya

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
762
Ni wazi katika maisha huwezi kuishi peke yako.
Lakini pamoja na kutegemeana huko, yapo mambo ambayo usipokuwa mwangalifu, yatakugharimu sana kimaisha.

Zipo imani na mitazamo mbalimbali ya kijamii ambayo ina nguvu sana lakini haina ukweli wowote.

Kwa mfano, mtu akikuambia "fulani amekusengenya" wakati kumbe hakufanya hivyo, ukiamini maneno hayo (japo hayana ukweli), athari yake itakuwa ni halisi kabisa katika maisha yako. Yatakusababishia chuki na yataongoza kabisa maisha yako in relation to mtu huyo.

Basi iko mifano mingi ya namna hiyo ambayo inaongoza maisha ya wengi lakini kumbe haina ukweli wowote. Ifuatayo ni baadhi:

1. Maisha ya sasa ni magumu sana.
2. Hakuna mwanamume mwaminifu siku hizi.
3. Siku hizi wanawake wanapenda tu pesa.
4. Siku hizi hakuna cha ndoa wala nini?
5. Wanasiasa wote ni waongo.
6. Huwezi kuajiriwa bila kuwa na refa.
7. Polisi wote ni wala rushwa.

Unaweza kuongeza mengi tu.
Cha msingi cha kujiuliza ni kuwa, je, umechunguza mitazamo ya kijamii inayoongoza maisha yako? - maana ipo hata kama huijui. Ipo.

Only those who are rebellious against such view have a greater chance of making it to the top of whatever field of life.
 
Nikadhani labda unamaanisha ule uasi tuliouzoea!...
 
Ndivyo unavyoamini, binadamu hatuez kua na mawazo na imani kuhusu mambo mbalimbali yakafanana hata siku moja
Mimi siamini, wewe unaamini hivo, wengine hawaamini na wengine wanaamini,
maisha yanasonga mbele.
 
ni uasi halisi

kwamba kiongozi anaweza kuasi kundi lake
Kama kundi linashikilia social views ambazo ana uhakika hazisongeshi mambo mbele, dawa nzuri ni kuwa rebellious tu - sio in a negative way lakini in a positive way.
 
Ndivyo unavyoamini, binadamu hatuez kua na mawazo na imani kuhusu mambo mbalimbali yakafanana hata siku moja
Mimi siamini, wewe unaamini hivo, wengine hawaamini na wengine wanaamini,
maisha yanasonga mbele.
Hiyo ni sawa kabisa. Ndio maana ya michango ya mawazo mkuu. Ukichangia hili, huyu litamfaa; huyu halitamfaa. Ndio part ya maisha. nakubaliana na wewe kabisa.
 
Kama kundi linashikilia social views ambazo ana uhakika hazisongeshi mambo mbele, dawa nzuri ni kuwa rebellious tu - sio in a negative way lakini in a positive way.
hahahaaa

zanzibar=sichagui wale wa kushoto
magogoni=anaapisha wa kushoto

wa kulia washazingua tena...ukiona hivyo
 
Ndivyo unavyoamini, binadamu hatuez kua na mawazo na imani kuhusu mambo mbalimbali yakafanana hata siku moja
Mimi siamini, wewe unaamini hivo, wengine hawaamini na wengine wanaamini,
maisha yanasonga mbele
.
Ndio maana huwa sipendi kumwambia mtu "una fikra potofu", kwa kuwa zinaonekana potofu kwako lunayesema akini kwake na wengine ni sahihi. Kuna watu huwa wanapenda kulazimisha wengine waamini kile wanachokiamini wao, na kama hutokubaliana nao utaambiwa una fikra potofu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom