Naamini sasa Magaidi hutengenezwa na Serikali kote duniani kwa utawala usio haki na kandamizi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
Wanajamii kipindi cha nyuma nilikuwa nashangaa inakuwaje mtu anajitoa mhanga kwa kujilipua na bomu na kuuwa watu, nilikuwa sipati jibu kama ni uendewazimu au ni imani kali za dini?

Lakini kwa fikra zangu siaamini kama wote ni watu waliorukwa na akili, na amini kabisa uonevu unapovuka mipaka na watu wakakosa namna ya kuukabili kwa njia ya amani, namna inayobaki ni kupandwa na hasira na kuwa na kisasi cha kupitiliza, na ndio matokeo ya machafuko mengi duniani.

Siungi mkono mauaji ya aina yoyote ile lakini pia siungi mkono uonevu wowote pia, na ukweli toka kwenye nafsi yangu nimeanza kuwa na mtazamo tofauti na watu wanaojitoa mhanga, inawezekana ni watu wanaojitambua kabisa na wanaopenda maisha ila wajinga wachache wanawafanya wafikie hapo.

Maana ikifika mahali uonevu unazidi hakuna jinsi, tukose wote au tupate wote. Huu ni mtazamo wangu, nakaribisha mawazo mengine.

hivi leo wakina Bashe, Lissu, Mbowe, Nape, Saanane, Lema nk wakipata nafasi hawawezi kuwa kundi hilo hapo juu na wananchi waliochoka na utawala wa kiimla?
 
Thats right... unajua watu huwa wanakandamizwa... inafikia stage wanaumia sana. Wanavulia.. lakin siku wakisema imetosha... ndio wanaanza kuitafuta haki yao kwa nguvu
 
Ile skendo mauaji ya polisi kule vikindu ni somo tosha...

Unachonga kinyago afu kinakutisha kweli...
 
Kwa kipindi hiki kuna wanaenufaika na hali ilivyo wengine twaumia, sisi ndio wakutafuta pori.
 
"Watu wanaandamana mioyoni iko siku wataandamana barabara bila kuambiwa na CDM, CUF na taifa litapasuka"

- Mheshimiwa Lema.

Haya ni maneno mazito si ya kupuuzia, serikali haina budi kujitafakari na kutafuta njia muafaka ya kuliepusha taifa na hali tete iliyopo
 
Kama wahenga walivyosema ...unaweza kuwadanganya watu kwa muda...., unaweza pia kuwakandamiza kwa muda....
 
tena haya mambo huwa yanaanza kama mzaha vile, watu ni kama hua wanapandwa na pepo,wakiamua kuuwasha moto serikali haitaamini kama hao ndio wananchi wao wa siku zote.
 
Nimeumia saaana aiseee, niko mahali hapa IPTL kuna magari kibao ya Polisi, najiuliza uchaguzi mdogo aiseee magari kibao, je ingekua uchaguzi Mkuu??
 
Hata hawa polisi wetu wanalijua sana hilo. Huko kwao makambini kuna wakati askari aliyeonewa sana huwa anaamua akipewa silaha kwenda lindo anaondoa maisha ya mkubwa wake anayemuonea na kujiondoa mwenyewe.
Kila jambo lina kipimo cha uvumilivu, Hapa Kleruu alivumiliwa kwa kiasi chake na Mwamwindi lakini dharau na manyanyaso yalipo zidi Mwamwindi alichukua hatua. Sasa yale ni manyanyaso tuu, jee hivi wanavyojeruhi na kuua kabisa watu watavumilia mpaka lini? Au tunasubiri tuje tuone mtu kajilipua walipo viongozi wetu wa chama cha makinikia ndio akili itakuja kuwa uovu ni mbaya dhidi ya raia wema?
 
Safari ya kwenda magogoni inachangamoto zake.changishaneni harambee makamanda jengeni chama acheni kulialia.
 
kama wale wa itikadi kali serikali zao zimechangiaje..?
unafikiria nini kwa wale wanaouwa wanyama(tembo,faru n.k)..?
unafikiria mataifa yaliyoendelea sio chachu ya ugaidi..?
 
Back
Top Bottom