Naamini nimefaulu majaribio ya kujiunga na seattle sounders-mrisho ngassa

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
'' Mara tu baada ya mazoezi kabla ya timu kuelekea nchini Panama,kocha mkuu wa Sounders bwana Sigi Schmid aliniita na kufanya naye mazungumzo ya takribani dakika kama 20 hivi,kimsingi alikuwa ananiuliza maswali mbali mbali, mfano aliniuliza kama nipo tayari kuichezea SEATTLE SOUNDERS pi akaniuliza kama ningefurahia kuishi hapa SEATTLE ,namimi nilimjibu kuwa nipo tayari ,basi baada ya hapo akaanza kunielezea namna nilivyofanya vizuri kwenye majaribio na angependa niichezee Sounders,mwisho kabisa akaniambia kwakuwa muda wangu wa majaribio umekwisha sina budu kurejea nyumbani taratibu husika zifanyike ili niweze lurejea hapa mapema mwezi december kwa ajili ya kujiunga na timu moja kwa moja ''- MRISHO NGASSA


My take:. Issue ni kuwa je atakuwa fit na kumantain perfomance mpaka hiyo December au ndio changa la macho kama la West Ham, otherwise big up Ngassa kwa kufuzu majaribio ila kuwa makini kwenye mazungumzo ya Maslahi maana one of the Key Sounders player Rosaire analipwa US$ 42000 per annum!Kwa kuanzia namshauri Ngassa aongee na Nizar Khalfan kuhusu mshahara anaolipwa na Vancouver White Caps japo mishahara ya wachezaji wa bongo ni siri sana! Pia waweza peruzi hapa http://gosounders.com/roster/salaries/ kujua salary structure ya Seattle Sounders FC.

Tatizo la MSL ni ligi kubwa duniani ila wachezaji wanalipwa kiduchu sana isipokuwa wale wa ulaya wenye majina kama Beckham, Freddie Ljungberg, Thierry Henry etc.Source: Shafih Dauda Sports Blog
 
Ngassa kajitahidi sana, sina shaka na kumaintain kiwango chake kwan naamini anaweza sana! Mafanikio mema MKN.
 
Lazima aangalie anafuata nini huko,ningependa pesa isiwe concern kubwa sana kwake kwa sasa,achukulie nafasi aliyopata kama platform ya kufanya vizuri na kufika mbali zaidi,mshahara utapanda tu taratibu,natumaini atakuwa amejifunza toka kwa boban aliyefika sweden na kutaka kuanza na mshahara kama wa beckham.
 
Asijekutuletea mambo ya Boban ambae aliu'miss mmea akaamua kurudi.
 
December wakati ligi inaisha november? Preseason inaanza february.
 
Hivi ni kwanini kijana asubiri mpaka December?? Mbona League inaendelea na ni jana tu Robbie Keane amejiunga na LA Galax na keshafunga mechi yake ya kwanza kabisa? Isije kuwa kijana kapigwa changa la macho...

BBC Sport - Robbie Keane scores on debut as LA Galaxy beat San Jose

Wazee ni mara ya pili sasa huyu dogo anakwama katika mbio za soka la Ughaibuni, nini tatizo??? West ham tuliambiwa atarejea imepita mpakaleo, Seattle Sounders mambo ndo hivyo tena. Ni soka au kuna tatiizo lingine????????



Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall amekanusha taarifa kuwa kiungo wa timu hiyo, Mrisho Ngassa alifuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa aliyoyafanya mwaka jana nchini Marekani katika klabu ya Seattle Sounders.
Ngassa ambaye alipata nafasi ya kucheza dhidi ya Manchester United alipokuwa kwenye majaribio hayo, ilielezwa kuwa amefanya vizuri na angeitwa kufanya mazungumzo juu ya kusajiliwa mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Stewart alisema wenyeji wa Ngassa katika majaribio hayo walifurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na winga huyo lakini hakuwa na ubora wa kucheza katika Ligi Kuu ya Marekani.
“Nilishangazwa na taarifa zilizokuwa zimeenea mara baada ya Ngassa kumaliza majaribio yake, hakufuzu, kilichotokea ni kwamba walimsifia kwa kiwango alichoonyesha katika mazoezi waliyompa,” alisema Stewart na kuongeza:
“Ukiangalia Ngassa anatoka katika ligi yenye ubora mdogo ukilinganisha na ile ya Marekani, jambo ambalo lingemlazimu kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia kiwango cha kucheza ligi hiyo.
“Nadhani hilo pia ndilo lililosababisha acheze chini ya kiwango katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Bara kwa kuwa bado alikuwa na ndoto za kwenda kucheza soka la kulipwa nje.”
Viongozi wa Azam FC, waliwahi kusema Ngassa alifuzu baada ya kucheza katika mechi ya kirafiki ya Seattle Sounders dhidi ya Manchester United ya England.

SOURCE: Kocha Azam: Mrisho Ngassa hakufuzu majaribio Marekani - Global Publishers
 
Hahaha wachezaji wetu wengi hawana afya ya kwuawezesha kucheza huko, wataishia hapa hapa.
 
Daaa inasikitisha ngasa aiulizwa maswali ya kisaikolijia ili wajue jinsi kumsaidia baadae yeye akaona ameshafuzu lugha kazi kweli kweli!!
 
Back
Top Bottom