Naachana na harakati za kisiasa Tanzania, hazina faida yoyote

Ndugu zangu nimekuwa na nyie hapa kwa zaidi ya miaka 7 sasa.

Kulingana na mwenendo wa siasa za nchi hii naomba niachane kabisa na siasa, ni kujipa presha na usumbufu usio na faida.

Mwanzo nilifikiri tatizo ni Marais wanaotawala hii nchi kumbe tatizo sio Marais wanaotawala hii nchi bali ni mfumo ulisimikwa na sisi wananchi wenyewe.

Kumbe tatizo ni sisi sio Marais wa CCM.

Naumia sana juu ya taifa langu naona litachelewa kwa sababu ya mfumo huu tuliojiwekea na kuulea sisi wenyewe.

Nimegundua Marais hawajawai kuwa na tatizo katika nchi hii.

Nimegundua CCM haijawai kuwa na tatizo katika nchi hii tatizo ni sisi wenyewe.

Kwamba Akwilina alipigwa risasi hata wanafunzi tu wa chuo chake wakashindwa hata kuandamana?

Mawazo aliuwawa kihuni wafuasi wa chadema Geita wakashindwa hata kuandamana?

Mwangosi na Gwanda waliuwawa wahandishi wa habari wakashindwa kabisa hata kuandamana?

Msanii Roma na Ney walitekwa na wasanii wakashindwa hata kuandamana?

Mo alitekwa hata wafanyabiashara wenzie wakashindwa hata kuandamana?

Ulimboka alivunjwa vunjwa hata madactari wakashindwa kuandamana?

Lissu akapigwa risasi wanachama Chadema wakashindwa hata kuandamana?

Nape akanyooshewa bastola lakini wanachi wakashindwa hata kuandamana.

Mbowe akafungwa,Sugu akafungwa, Lema akafungwa watu hata kuandamana?

Sasa hivi Mbowe kafungwa jiulize Mbowe anakosa nini kuishi na familia yake?

Mbowe hana pesa za kula mpaka mwisho wa maisha yake? Jibu anazo ila anapigania watu ambao hawajielewi.

Lakini jambo lililonishangaza zaidi ni Watu kuvunjiwa nyumba zao kinyume na sheria lakini hata kuandamana hakuna? Hizo nyumba zilikiwa za chadema, CUF au ACT?

Ila kilichonifanya kabisa niachane na siasa na kuona tatizo sio Ccm wala Rais anayekuwa madarakani tatizo ni Watanzania ni hili swala la TOZO.

Kwa nchi za wenzetu kupandisha hata mia kwenye mkate tu kungeiondoa serikali madarakani.

Leo hii sukari imepanda kwa 100% within 5 years

Mafuta yanapanda tu hovyo hovyo ila watu tumelala tu.

Kuna mtu anasema eti Rais anawalazimisha polisi kutesa watu sio kweli nakataa Rais anabeba bunduki wewe unayebeba bunduki kwanini usifuate Sheria? Kwamba Rais anawalazimisha mahakimi kuhukumu kesi kihuni? Wewe hakimu kwanini usifuate sheria?

Kwamba Rais alibeba bunduki na kumpiga risasi Tundu Lissu au Mwangosi wewe uliyetumwa unge kataa wangekufanya nini? Mfumo tunaulea sisi wananchi, Wafanyakazi wa serikali ndio tatizo zaidi lakini cha kishangaza na wao mishahara yao inachezewa tu na kutopandishwa.

Mfumo tumeulea sisi Watanzania na tuache kuwasingizia Ccm na Rais aliyepo madarakani.

Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.

naomba nijibu kama mmoja wa waliotajwa hapa kua ni tatizo.

moja ya sababu ya mimi kutoandamana kwa lengo la kudai Haki, Amani na Maendeleo kwa Watanganyika wote ni kuwa, najua wazi nitakapo fanya hiyvo policcm watazuia maandamano hayo kwa Unyama na risasi za moto. Na ikitokea nimeuliwa, kifo changu hakita kua na IMPACT yoyote katika Lengo tajwa.

kama utaachana na siasa ni sawa, lakini nakusihi usiachane na harakati za kudai Haki, Usawa, Amani na Maendeleo kwa Watanganyika. It is your duty as human being & Mtanganyika.

Tukae chini tutafute njia ambazo hata tukipoteza maisha yetu katika harakati hizi basi angalau kuwe na SERIOUS REPERCUSSION kwa wahusika na SIGNIFACANT IMPACT kuelekea lengo.

Dont just loose your life, make sure when you do so it certainly counts…it is the only way i can justify, wilingly loosing mine.
 
Wewe ndiyo ujamuelewa jamaa kakata tamaa
Hajakata tamaa ila tunakatisha tamaa.

Mfano kwenye Corona . Awamu ya 5 kuitaja tu Corona na chanjo yake ilikuwa jinai machoni mwa vyombo vya dola.
Awamu ya 6 kuipinga Corona na chanjo yake ni jinai machoni mwa vyombo vya dola. Na wananchi hawawezi kuhoji !!. Kwanini jana hivi na leo vile !!.
 
I salute you Mkuu 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾👍🏽 Ahsante sana.
Tatizo ni sisi wenyewe watanzania mkuu

Tatizo lipo kwetu watu hawajui haki zao

Ufahamu upo chini

Kuna watu kama mimi hatuna chama cha siasa lakini tukiongelea siasa labda whatsapp status utasikia utatekwa wewe kaa kimya

We are so arrogant and coward ccm. Aendelee kutawala
I
Ona ishu ya mbowe no pressure kutoka kwa wananchi kabsa tumejawa na uwoga wivu, na ubinfsi
Sad for my country
 
Mwaka 1995 nilikimbia Tanzania baada ya kuwekwa jela wiki mbili na Mkuu wa wilaya kisa eti nimefanya maandamano saa mbili za usiku kijijini kwetu, Mwaka 1999 nilirudi Tanzania baada ya kukaa mwezi mmoja nilitafakari nikaona mambo bado ni yale yale na hakuna uwezekano wa mabadiliko yoyote nikaondoka tena , hadi leo hii niko ukimbizini.
Upo kambi gan ya wakimbizi?
 
Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.
Njauleje; nambi tujileuli?
Sisi hatuna nchi nyingine, kwa hiyo tutabanana hapa hapa. Yale yasiyo sawa tutaendelea kuyarekebisha polepole, kiungwana, kwa hoja badala ya vioja, bila fujo, na kwa ustaarabu bila kuvuruga amani ya nchi yetu.
 
Point! point! point! Najingine umelisahau kwanini jambo la katiba wa hoji chadema tu wakat kuna vyama vya siasa zaidi ya 20.
Katiba ni hitaji la wanasiasa, siyo hitaji letu wananchi huku vijijini. Sisi tunahitaji huduma nzuri za afya, maji, shule, barabara zinazopitika, masoko ya uhakika ya kuuzia mazao yetu, bei nzuri za mazao, kupunguza umaskini, nk. Hayo hayahitaji hiyo katiba yenu ili yaweze kupatikana.
 
Ndugu zangu nimekuwa na nyie hapa kwa zaidi ya miaka 7 sasa.

Kulingana na mwenendo wa siasa za nchi hii naomba niachane kabisa na siasa, ni kujipa presha na usumbufu usio na faida.

Mwanzo nilifikiri tatizo ni Marais wanaotawala hii nchi kumbe tatizo sio Marais wanaotawala hii nchi bali ni mfumo ulisimikwa na sisi wananchi wenyewe.

Kumbe tatizo ni sisi sio Marais wa CCM.

Naumia sana juu ya taifa langu naona litachelewa kwa sababu ya mfumo huu tuliojiwekea na kuulea sisi wenyewe.

Nimegundua Marais hawajawai kuwa na tatizo katika nchi hii.

Nimegundua CCM haijawai kuwa na tatizo katika nchi hii tatizo ni sisi wenyewe.

Kwamba Akwilina alipigwa risasi hata wanafunzi tu wa chuo chake wakashindwa hata kuandamana?

Mawazo aliuwawa kihuni wafuasi wa chadema Geita wakashindwa hata kuandamana?

Mwangosi na Gwanda waliuwawa wahandishi wa habari wakashindwa kabisa hata kuandamana?

Msanii Roma na Ney walitekwa na wasanii wakashindwa hata kuandamana?

Mo alitekwa hata wafanyabiashara wenzie wakashindwa hata kuandamana?

Ulimboka alivunjwa vunjwa hata madactari wakashindwa kuandamana?

Lissu akapigwa risasi wanachama Chadema wakashindwa hata kuandamana?

Nape akanyooshewa bastola lakini wanachi wakashindwa hata kuandamana.

Mbowe akafungwa,Sugu akafungwa, Lema akafungwa watu hata kuandamana?

Sasa hivi Mbowe kafungwa jiulize Mbowe anakosa nini kuishi na familia yake?

Mbowe hana pesa za kula mpaka mwisho wa maisha yake? Jibu anazo ila anapigania watu ambao hawajielewi.

Lakini jambo lililonishangaza zaidi ni Watu kuvunjiwa nyumba zao kinyume na sheria lakini hata kuandamana hakuna? Hizo nyumba zilikiwa za chadema, CUF au ACT?

Ila kilichonifanya kabisa niachane na siasa na kuona tatizo sio Ccm wala Rais anayekuwa madarakani tatizo ni Watanzania ni hili swala la TOZO.

Kwa nchi za wenzetu kupandisha hata mia kwenye mkate tu kungeiondoa serikali madarakani.

Leo hii sukari imepanda kwa 100% within 5 years

Mafuta yanapanda tu hovyo hovyo ila watu tumelala tu.

Kuna mtu anasema eti Rais anawalazimisha polisi kutesa watu sio kweli nakataa Rais anabeba bunduki wewe unayebeba bunduki kwanini usifuate Sheria? Kwamba Rais anawalazimisha mahakimi kuhukumu kesi kihuni? Wewe hakimu kwanini usifuate sheria?

Kwamba Rais alibeba bunduki na kumpiga risasi Tundu Lissu au Mwangosi wewe uliyetumwa unge kataa wangekufanya nini? Mfumo tunaulea sisi wananchi, Wafanyakazi wa serikali ndio tatizo zaidi lakini cha kishangaza na wao mishahara yao inachezewa tu na kutopandishwa.

Mfumo tumeulea sisi Watanzania na tuache kuwasingizia Ccm na Rais aliyepo madarakani.

Kiufupi nimeachana na siasa, nimeachana na Tanzania nimekata tamaa, nimepoteza uzalendo nitaondoka Tanzania na kwenda kuishi na familia yangu kwenye nchi nyingine inayofuata misigi ya Sheria, Haki na Uwajibikaji wa viongozi.
Kwani kuna mtu alikushika miguu na mikono usiandamane?? Kwa jinsi unavyoandikaga nyuzi zako niliona kabsiaa hatuna mtu hapoo.. kama kweli ww n mwanamabadiliko ungeonesha mfano..uandamane peke yako..shida yako ww na kina maria sarungi na huyoo mtoto wa rais wa zanzibar mnaandamana kwenye keyboard zenu. Tena mmegawana, ww humu jf kwa wajinga wenzio, maria ma mwenzake wako twiter.
Zero brain!
 
Hajakata tamaa ila tunakatisha tamaa.

Mfano kwenye Corona . Awamu ya 5 kuitaja tu Corona na chanjo yake ilikuwa jinai machoni mwa vyombo vya dola.
Awamu ya 6 kuipinga Corona na chanjo yake ni jinai machoni mwa vyombo vya dola. Na wananchi hawawezi kuhoji !!. Kwanini jana hivi na leo vile !!.
Kila kitu kina sababu zake wewe ukujua yaliyokuwa nyuma ya kovid katika awamu ya 5 hadi kupelekea serikali ya magufuli kutambua kuna ujuma acha nikukumbushe maana nyinyi vichwa panzi ni wepesi kusahau ,unakumbuka kabla ya covid duniani watu wasiyo itakia mama nchi yetu walisema tanzania kunaugonjwa wa ZIKA vyombo vyote vya habari vya kimataifa vilipiga kelele kuwa serikali inaficha zika walipo shindwa kwenye ili wakasema tena tanzania kuna ugonjwa wa EBOLA sasa mm nakuuliza unadhani serikali makini inge noti kitu gani ,pia umesahau walivyo kuwa wanasema tz tuna anguka mabarabarani kwa kovid sasa mimi nakuuliza ilikuwa kweli au uongo
 
Back
Top Bottom