Naacha ualimu naingia kwenye siasa

BG Seme

JF-Expert Member
Oct 29, 2014
360
260
Mimi ni mtumishi wa umma nimeajiriwa mwaka 2013 kama mwalimu.

Nimefundisha somo la hisabati kwa bidii kubwa sana hadi kufika mahali wanafunzi 16 kufaulu kwa daraja 'A' na wengine 'B' na wachache C. Kwa wilaya somo langu lilishika nafasi ya pili kwa wanafunzi kupata daraja A nyingi zaidi.
Sasa; kwa hali ilivyo sasa nimeamua kuacha kazi kwa hiyari yangu mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote.

Sababu za kuacha kazi:

=> Vyama vya wafanyakazi kutukata makato bila kutusemea/kututetea/ juu ya maslahi yetu, inaonesha wazi CWT wanaogopa kudai madai yetu kwa serikali ya chama cha mapinduzi kwani wengi wao ni viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi pia
 
Muulize kisandu atakupa ushauri mzuri yeye aliacha siasa akarudi kufundisha kabaki na siasa za mitandaoni
 
Acha zako huko kwenye siasa utapoteza muda cha muhimu kamata AK ingia road kwenye mabank huko kapore mamilioni uhame nchi
 
Mimi ni mtumishi wa umma nimeajiriwa mwaka 2013 kama mwalimu.

Nimefundisha somo la hisabati kwa bidii kubwa sana hadi kufika mahari wanafunzi 16 kufaulu kwa daraja 'A' na wengine 'B' na wachache C. Kwa wilaya somo langu lilishika nafasi ya pili kwa wanafunzi kupata daraja A nyingi zaidi.
Sasa; kwa hali ilivyo sasa nimeamua kuacha kazi kwa hiyari yangu mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote.

Sababu za kuacha kazi:

(1). Serikali kutudanganya watumishi, Rais hatimizi ahadi zake kuhusu nyongeza za mishahara na kupandisha madaraja.

(2) Serikali kutukatisha tamaa kwa kauli mbaya(zisizotia moyo) mfano rais alisema "kama mshahara kidogo acha kazi nenda kalime"

(3) Malipo hayaendani na kazi tunayofanya; darasa langu Lima wanafunzi 102 na lilitakiwa kuwa na wanafunzi 40 hadi 45 tu.

(4) Vyama vya wafanyakazi kutukata makato bila kutusemea/kututetea/ juu ya maslahi yetu, inaonesha wazi CWT wanaogopa kudai madai yetu kwa serikali ya chama cha mapinduzi kwani wengi wao ni viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi pia.

Mwisho; namshauri rais kusikiliza malalamiko ya walimu na wafanyakazi wote kwa ujumla, asiwe mwepesi kupuuza na kudai wanaolalamika ni wapiga dili, kwani mimi mwalimu tena shule ya msingi nitapaga dili gani?

Pole sana kama unayoondika ni ya kweli. Una uhakika utapata haya uliyoyakosa kwenye ajira ya ualimu kwenye siasa? Inaonekana unaenda kwenye siasa kwa sababu ya maslahi binafsi...... utakuja kulia zaidi
 
Mimi ni mtumishi wa umma nimeajiriwa mwaka 2013 kama mwalimu.

Nimefundisha somo la hisabati kwa bidii kubwa sana hadi kufika mahari wanafunzi 16 kufaulu kwa daraja 'A' na wengine 'B' na wachache C. Kwa wilaya somo langu lilishika nafasi ya pili kwa wanafunzi kupata daraja A nyingi zaidi.
Sasa; kwa hali ilivyo sasa nimeamua kuacha kazi kwa hiyari yangu mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote.

Sababu za kuacha kazi:

(1). Serikali kutudanganya watumishi, Rais hatimizi ahadi zake kuhusu nyongeza za mishahara na kupandisha madaraja.

(2) Serikali kutukatisha tamaa kwa kauli mbaya(zisizotia moyo) mfano rais alisema "kama mshahara kidogo acha kazi nenda kalime"

(3) Malipo hayaendani na kazi tunayofanya; darasa langu Lima wanafunzi 102 na lilitakiwa kuwa na wanafunzi 40 hadi 45 tu.

(4) Vyama vya wafanyakazi kutukata makato bila kutusemea/kututetea/ juu ya maslahi yetu, inaonesha wazi CWT wanaogopa kudai madai yetu kwa serikali ya chama cha mapinduzi kwani wengi wao ni viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi pia.

Mwisho; namshauri rais kusikiliza malalamiko ya walimu na wafanyakazi wote kwa ujumla, asiwe mwepesi kupuuza na kudai wanaolalamika ni wapiga dili, kwani mimi mwalimu tena shule ya msingi nitapaga dili gani?
Ukiingia kwenye siasa, sanasana utawasahau walimu wenzako pindi ukishafundishwa ufisadi.

Kama una nia njema, kuingia kwenye siasa unahitaji cause kubwa zaidi. Hata mwalimu Nyerere aliacha ualimu ili kusaidia watanzania wote na siyo waalimu peke yake.
 
Swali la kujiuliza, je ukiingia kwenye siasa hayo yote uliyoainisha hapo juu yatatatuliwa, je kwako siasa unachukulia kama kazi? (nini vyanzo vyako vya mapato ukishaacha kazi?hasa ukizingatia siasa ni mfum wa maisha ya kila siku ya mwanadamu)...nadhani ushauri namba mbili wa kwenda kulima naona ni mzuri zaidi
 
Siasa sio lazima ufanye hivi zetu za Chadema ukawa, Siasa ni maisha, kwakuwa kwenye hoja zako tayari umeonesha muelekeo sasa fanya hivi.

Kwakuwa siasa ni mchakato wa kuyatafuta madaraka na kuyatumia kuleta impact, basi anzia hapo ulipo kama Musa vile alipoulizwa mkononi mwako umeshika nini, akajibu fimbo. Basi sasa ualimu ambayo ndiyo system uliyopo ndio fimbo yako, tumia ualimu huo ufanye siasa huku target group lenye ushawishi ni walimu wenzio na wadau wa elimu, onesha nia yako na maono yako kwao, Fanya scientific politics huku main goal yako ni kuja kuwa kiongozi wa chama cha walimu CWT, anza kujenga hoja zenye ushawishi, huku ukisoma vitabu mbalimbali vya namna ya kuyakamata madaraka.
 
Wewe acha utani, endelea kufundisha watoto.Jaribu kutafakari iwapo aliyekufundisha hesabu ukazijua hivi angeamua kuingia ktk siasa, ww si ungekuwa mpiga debe Tandale kwa Tumbo? Ww si bure, unaelekea ni mvivu. Hata hiyo siasa itakushinda kwa uvivu huo.Walimu wa maths wanavyotoka hela hivi kwa tuition ww unasubiri uongezewe mushahara?
 
Swali la kujiuliza, je ukiingia kwenye siasa hayo yote uliyoainisha hapo juu yatatatuliwa, je kwako siasa unachukulia kama kazi? (nini vyanzo vyako vya mapato ukishaacha kazi?hasa ukizingatia siasa ni mfum wa maisha ya kila siku ya mwanadamu)...nadhani ushauri namba mbili wa kwenda kulima naona ni mzuri zaidi

Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom