Naacha kazi ya kuajiriwa, naomba ushauri

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,614
8,617
Habarini za Asubuhi ndugu wote.
Mwenzenu mimi ni Dereva mzoefu wa magari toka mwaka 1996.

Nimekua taxi mani kwa kipindi kirefu sana na mwaka 2009 niliamua kutafuta ajira katika mashirika na nikapata kwa uweza wa MUNGU, nakubali kupitia kazi hiyo nimeweza kutengeneza japo nyumba ya kuishi na familia jijini Mwanza, tatizo imefikia naona ni kama nimechoka kua hapa lakini pia natamani kufanya shughuli binafsi.

Kuja kwangu hapa ni kukutana na msaada wa mawazo tofauti ya nini nitafanya baada ya hapa, naweza kuwa na mawazo yangu lakini mawazo ya wengi pia ni faida, nimefikia uamuzi huo kwa kuwaza sana zaidi ya mwaka mzima juu ya mshahara ninaoupata ambao nafikiri hata nikirudi kuwa taxi man naweza kuupata, kimsingi nikitoka nitakutana pesa kidogo kama 15Milion na nina kigari changu Carina TI.

Najiuliza nikinunua japo na kingine nikaingia vijiweni na vigari vyangu viwili siwezi kusukuma maisha?

Napenda kupata mawazo tofauti tofauti kwa wazoefu wengine pia, maana ajira kweli yaweza kuwa nzuri hasa inapoweza kukutoa sehemu moja kwenda nyingine lakini pia ina changamoto zake zinazochosha na zimenifanya kufikia maamuzi hayo.

Nakaribisha mchango wako wa mawazo.
 
Mkuu, kwa hiyo biashara, wala usithubutu kuacha kazi. Ujinga wa biashara za magari ni kwamba, moja ikiingiza pesa, nyingine inakula, so kile kinachobaki utaishia kutumia kwa matumizi binafsi na utaibemenda biashara yako na hiatokua...
Huo mtaji ni bora hata uingie chimbo la Dangote uanze kuuza cement...
 
Nimemaanisha kua chochote naweza fanya mkuu siyo lazimatiwe magari,nimesema magari nikimaanisha nina uzoefu nayo naweza fanya,yani mtu mwingine anapiga kazi na mimi napiga kazi vijiweni kama kawaida,asante kwa ushauli mkuu!
 
Mkuu wala hata hujakosea kuchukua uamzi huo!
Mwenzio nilichepuka kwa mkoloni zaidi ya miaka minne sasa...

Ni maamzi magumu na wengi kuanzia familia yako, ndugu, jamaa na marafiki huwa hawaafiki kirahisi!
Uwe na msimamo thabiti haijarishi utakutana na magumu yapi mbeleni... kikubwa ni kuzichanga vizuri karata zako.

Hakikisha unafanya biashara uliyo na uzoefu nayo na utajitanua zaidi kwa fursa nyingine baada ya kuona msimamo wa mradi wa awali.
Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla bado inazo fursa lukuki.

Umesema una uzoefu kama taximan, anza nayo na ukipata hela yako igawe hivi;
1) kwakuwa biashara ya taxi siku hizi inachagizwa sana na bajaj, mpe mtu TI yako akuletee hesabu kisha wewe nunua bajaj moja ipigishe mzigo mwenyewe. Iweke kijiwe kizuri kwa siku hutakosa sh40,000/= na utalala na mafuta ya route za kesho.

2)Nenda Sengerema vijiji vya karibu na BUHINDI Forest nunua shamba walau eka3 panda miti ya syprus kama backup pindi ukiteteleka unauza kwa bei nzuri make haichelewi kukua na wateja wake ni wengi.
 
Mkuu bigup, kuna kitu kinaitwa dhamira, mimi nilipanga nikifikisha umri fulani ni lazima niachane na ajira. Kwa kweli ilikuwa ni shughuli pevu kwani kiuhalisia maisha si lazima yaende kama ulivyopanga, nikawa nikikumbuka na mshahara nikawa napata woga sana, hata wife wangu hakukubaliana na wazo la mimi kuacha kazi eti tutateseka. Lakini nilishindwa kuishinda dhamira yangu. Wakati nikiwa kazini nilinunua shamba kama heka 15, bei ndogo sana ukilinganisha na plot za mjini. Kwa kweli lilikuwa pori hasa. Nikajibana mpaka nikachimba lambo la maji, nikaanza na kuku 20 machotara, baadae nikaongeza wengine 60. Kutokana na changomoto za magonjwa wakafa wakabaki 40 toka 80. Kumbuka nilikuwa na lambo hivyo nikaweka vijana wawili wakawa wanalima mbogamboga kuzunguka hilo lambo. Baada ya muda kuku wakaanza kutaga, nikanunua kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuatamia, Mungu si Athumani sasa nina kuku zaidi ya 400 na nimejenga mabanda ya kuku. Kazi nimeacha nina mwaka sasa, kwa kweli napata pato la wastani lakini ninakopesheka kwa uhakika. Ninaona kesho yenye matumaini kwani nazidi kupanuka mpaka ninaona kama nilikuwa napoteza muda kwenye ajira japo ajira ilinisaidia kupata mtaji wa hayo niliyoanza nayo. Kama umedhamiria kuacha kazi hebu jaribu kuweka kamradi kamoja hasa shamba ni uhakika zaidi kuliko mengine japo miradi mingine simaanishi huwezi kutoka.
 
Asante ndugu,nakushukulu kwa kunitia moyo,MUNGU akubariki
 
Mkuu bigup, kuna kitu kinaitwa dhamira, mimi nilipanga nikifikisha umri fulani ni lazima niachane na ajira. Kwa kweli ilikuwa ni shughuli pevu kwani kiuhalisia maisha si lazima yaende kama ulivyopanga, nikawa nikikumbuka na mshahara nikawa napata woga sana, hata wife wangu hakukubaliana na wazo la mimi kuacha kazi eti tutateseka. Lakini nilishindwa kuishinda dhamira yangu. Wakati nikiwa kazini nilinunua shamba kama heka 15, bei ndogo sana ukilinganisha na plot za mjini. Kwa kweli lilikuwa pori hasa. Nikajibana mpaka nikachimbwa lambo la maji, nikaanza na kuku 20 machotara, baadae nikaongeza wengine 60. Kutokana na changomoto za magonjwa wakafa wakabaki 40 toka 80. Kumbuka nilikuwa na lambo hivyo nikaweka vijana wawili wakawa wanalima mbogamboga kuzunguka hilo lambo. Baada ya muda kuku wakaanza kutaga, nikanunua kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuatamia, Mungu si Athumani sasa nina kuku zaidi ya 400 na nimejenga mabanda ya kuku. Kazi nimeacha nina mwaka sasa, kwa kweli napata pato la wastani lakini ninakopesheka kwa uhakika. Ninaona kesho yenye matumaini kwani nazidi kupanuka mpaka ninaona kama nilikuwa napoteza muda kwenye ajira japo ajira ilinisaidia kupata mtaji wa hayo niliyoanza nayo. Kama umedhamiria kuacha kazi hebu jaribu kuweka kamradi kamoja hasa shamba ni uhakika zaidi kuliko mengine japo mengi simaanishi huwezi kutoka.
Ukiachana na niliposema hapo juu nachotaka kufanya na kuomba ushauli wa nini nifanye kama unavyonishauli,nina shamba pia ninalima tikiti maji,na ninaona mkono wa MUNGU ndugu,asante mkuu kwa ushauli wako
 
Mkuu bigup, kuna kitu kinaitwa dhamira, mimi nilipanga nikifikisha umri fulani ni lazima niachane na ajira. Kwa kweli ilikuwa ni shughuli pevu kwani kiuhalisia maisha si lazima yaende kama ulivyopanga, nikawa nikikumbuka na mshahara nikawa napata woga sana, hata wife wangu hakukubaliana na wazo la mimi kuacha kazi eti tutateseka. Lakini nilishindwa kuishinda dhamira yangu. Wakati nikiwa kazini nilinunua shamba kama heka 15, bei ndogo sana ukilinganisha na plot za mjini. Kwa kweli lilikuwa pori hasa. Nikajibana mpaka nikachimba lambo la maji, nikaanza na kuku 20 machotara, baadae nikaongeza wengine 60. Kutokana na changomoto za magonjwa wakafa wakabaki 40 toka 80. Kumbuka nilikuwa na lambo hivyo nikaweka vijana wawili wakawa wanalima mbogamboga kuzunguka hilo lambo. Baada ya muda kuku wakaanza kutaga, nikanunua kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuatamia, Mungu si Athumani sasa nina kuku zaidi ya 400 na nimejenga mabanda ya kuku. Kazi nimeacha nina mwaka sasa, kwa kweli napata pato la wastani lakini ninakopesheka kwa uhakika. Ninaona kesho yenye matumaini kwani nazidi kupanuka mpaka ninaona kama nilikuwa napoteza muda kwenye ajira japo ajira ilinisaidia kupata mtaji wa hayo niliyoanza nayo. Kama umedhamiria kuacha kazi hebu jaribu kuweka kamradi kamoja hasa shamba ni uhakika zaidi kuliko mengine japo miradi mingine simaanishi huwezi kutoka.
Hili wazo la ufugaji liko akilini mwangu sana,hebu nisaidie mawazo ya namna ya kuanza kwa maana ya eneo,mabanda chakula na kuku wenyewe
 
Kimsingi mimi nilianza na banda dogo nikawa naongeza kadiri ninavyoongeza kuku ama kuongezeka. Kuku wapya ninapowaleta hasa hawa machotara nawaletea chakula chao special. Baada ya hapo naanza kuwapa pumba tu huku nikiwafungulia wajitafutie wenyewe na chakula kingine nawawekea kwenye vyombo nje pamoja na maji ya kunywa. Ila mradi wa kuku unalipa taratibu kidogo. Kwa sasa nimeanza kufuga sungura maana wanalipa zaidi na chakula wanakula kidogo kulinganisha na kuku. Pia sungura wanazaa sana kulinganisha na kuku, huku nilipo nimepata soko la sungura upande wa Kenya, sungura unamuuza kwa kilo na kilo moja ya sungura ni 10,000, kwa sungura anayekula vizuri wangalau unaweza kumuuza baada ya miezi minne toka amezaliwa na anakuwa na kilo 3 na kuendelea. Iwapo tutaendelea kuwasiliana nitakupa undani wa ufugaji wa sungura iwapo utapenda baada ya mimi kujua changamoto zake. Na iwapo utapenda hawa jamaa wanaonunua iwapo utauza sungura wasiopungua 50 wanakuja wenyewe kufuata katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Na iwapo utauza kuanzia 100 kwa mpigo wanafuata popote tanzania. Ni biashara nzuri sana kwani wanahitaji tani kwa tani ya sungura. Ila kwa kuanzia anza na kuku kwani ni rahisi na ufugaji wake wengi wameuzoea.
 
Asante mkuu..nitakutafuta muda c mrefu kiongozi
 
Mkuu bigup, kuna kitu kinaitwa dhamira, mimi nilipanga nikifikisha umri fulani ni lazima niachane na ajira. Kwa kweli ilikuwa ni shughuli pevu kwani kiuhalisia maisha si lazima yaende kama ulivyopanga, nikawa nikikumbuka na mshahara nikawa napata woga sana, hata wife wangu hakukubaliana na wazo la mimi kuacha kazi eti tutateseka. Lakini nilishindwa kuishinda dhamira yangu. Wakati nikiwa kazini nilinunua shamba kama heka 15, bei ndogo sana ukilinganisha na plot za mjini. Kwa kweli lilikuwa pori hasa. Nikajibana mpaka nikachimba lambo la maji, nikaanza na kuku 20 machotara, baadae nikaongeza wengine 60. Kutokana na changomoto za magonjwa wakafa wakabaki 40 toka 80. Kumbuka nilikuwa na lambo hivyo nikaweka vijana wawili wakawa wanalima mbogamboga kuzunguka hilo lambo. Baada ya muda kuku wakaanza kutaga, nikanunua kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuatamia, Mungu si Athumani sasa nina kuku zaidi ya 400 na nimejenga mabanda ya kuku. Kazi nimeacha nina mwaka sasa, kwa kweli napata pato la wastani lakini ninakopesheka kwa uhakika. Ninaona kesho yenye matumaini kwani nazidi kupanuka mpaka ninaona kama nilikuwa napoteza muda kwenye ajira japo ajira ilinisaidia kupata mtaji wa hayo niliyoanza nayo. Kama umedhamiria kuacha kazi hebu jaribu kuweka kamradi kamoja hasa shamba ni uhakika zaidi kuliko mengine japo miradi mingine simaanishi huwezi kutoka.
ushauri mzuri sana huu kama mlengwa akiuzingatia atatusua kabisa.

Kimsingi huyu bwana aachana na biashara za tax za kuganga njaa, sekta ya kilimo na ufugaji, ina utajiri wa kutisha.

Mfano eka 1 ya vitunguu maji mtu unatengeneza mpaka milio 20 ukilima eka 30 unazaidi ya milioni 600.

Sasa jiulize kwanini watanzania ni maskini? Jibu ni uvivu wa kufikiri na uoga wa kutoku subutu.

Mimi nina jamaa yangu yeye ni mfugaji wa kuku. Kwa siku anaokota trei 50 za mayai.

Ukipiga maesabu kwa mwezi aningiza kibindoni zaidi ya milioni 24.

Kwazi kwenu. Umaskini uteme cheni, kufanikiwa inawezekana.
 
Kuajiriwa ni Kwa malengo ila ukijifanya ndo umefika basi uzeeni utajuta
Mbona ametoa ushauri mzuri tu wakuu?
1.
Amesema "kuajiriwa n kwa malengo" maana yake ukiajiriwa iwe kwa muda fulani tu wa aidha kukusanya mtaji wa kuanzia kujiajiri au kupata uzoefu wa kuja kuendesha project yako
2.
Amesema "ila ukijifanya ndo umefika basi uzeeni utajuta" maana yake ni kama utakubali kuajiriwa kwa maisha yako yote hadi kustaafu kwa umri hapo utajuta na uzee.

Mimi nahisi ametoa ushauri mzuri sana, kwamba:
KUAJIRIWA SI VIBAYA
VIBAYA NI KUAJIRIWA KWA MAISHA YAKO YOTE.
 
Mkuu bigup, kuna kitu kinaitwa dhamira, mimi nilipanga nikifikisha umri fulani ni lazima niachane na ajira. Kwa kweli ilikuwa ni shughuli pevu kwani kiuhalisia maisha si lazima yaende kama ulivyopanga, nikawa nikikumbuka na mshahara nikawa napata woga sana, hata wife wangu hakukubaliana na wazo la mimi kuacha kazi eti tutateseka. Lakini nilishindwa kuishinda dhamira yangu. Wakati nikiwa kazini nilinunua shamba kama heka 15, bei ndogo sana ukilinganisha na plot za mjini. Kwa kweli lilikuwa pori hasa. Nikajibana mpaka nikachimba lambo la maji, nikaanza na kuku 20 machotara, baadae nikaongeza wengine 60. Kutokana na changomoto za magonjwa wakafa wakabaki 40 toka 80. Kumbuka nilikuwa na lambo hivyo nikaweka vijana wawili wakawa wanalima mbogamboga kuzunguka hilo lambo. Baada ya muda kuku wakaanza kutaga, nikanunua kuku wa kienyeji kwa ajili ya kuatamia, Mungu si Athumani sasa nina kuku zaidi ya 400 na nimejenga mabanda ya kuku. Kazi nimeacha nina mwaka sasa, kwa kweli napata pato la wastani lakini ninakopesheka kwa uhakika. Ninaona kesho yenye matumaini kwani nazidi kupanuka mpaka ninaona kama nilikuwa napoteza muda kwenye ajira japo ajira ilinisaidia kupata mtaji wa hayo niliyoanza nayo. Kama umedhamiria kuacha kazi hebu jaribu kuweka kamradi kamoja hasa shamba ni uhakika zaidi kuliko mengine japo miradi mingine simaanishi huwezi kutoka.
Mkuu shamba lako lipo maeneo gani? Lambo ulilichimba la ukubwa gani kwa kutumia manpower au mashine? ilikugharimu shilingi ngapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom