Na Wonder (Lyrics)

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Nawonder nawonder kila rhyme kila stanza/
Napanga na kuranda kwenye home za kupanga/
Kupanga kupanda kila mbegu juu ya mwamba/
Na mbegu zinagonga mwamba kila nyanda/

Najitahidi kung'ara bila pamba/
Maana ni masikhara kusubiri Tanzania ya Vi wonder/
Wakati textiles hazitoi hata kanga/
Viongozi mafake smile wakicheka na kujiramba/
Wakibuni kila style za kujivika kila Gamba/

Nawonder why tunakamua vipele/
Na majipu yameuchubua eti yaliyopita sio ndwele/
Na wonder nani atamvisha paka Kengele/
Wakati Panya akiteseka wenzake wanapiga vigelegele/
Panya wengine viherehere/
Nawashangaa ni nyani halafu wanamcheka ngedele/

Najua sio lazima kujua kila kitu/
Ila kuna ulazima kufuatilia kila issue/
Wanaoonewa ni wanyonge kila siku/
Na wanaoleta bifu ndo hao wameshika mpini wa kisu/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom