na wewe umeskia hii? eti kota za magomeni moja imeshindikana kuvunjwa, mvunjaji haioni!!!

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
Yaani ndo nimefika nyumbani sasa ivi kutoka kazini, nilikuwa kwenye daladala ziendazo mabibo ambazo wakati mwengine hukimbia foleni kwa kuzungukia huu upande wa tanesco. Ukipita pale ni kweli utaona kuna kajumba kamoja tu kamebaki, kwengine kote ni uwanja, hapo ndo kalianza kamjadala kasiko rasmi kama kawaida ya daladala. Eti mwendesha lile katapila akifika kwenhye hiyo nyumba haoni kitu cha kuvunja! Nimebaki nashangaa tu sielewi kama ni kweli. ila ukichungulia kwenye daladala basi utakaona hako ka kota kamebaki peke yake! umeiskia na wewe?
 
Mkuu inanikumbusha manzese kipindi kile cha Msufi upo pale
 
Acheni kuendekeza ushirikina.
Nimeskia wakiongea kwenye daladala, sielewi kama ni kweli au la! ndo maana nimeuliza kama na wewe umeskia. Niliwahi kuskia huko iringa pia eti watengeza barabara nao walishindwa kuhamisha kaburi ili wapitishe barabara, ikabidi waipindishe kulipisha kaburi
 
Hata mie nilishawahi kusikia kwamba mwezi umeundwa kwa jibini ya kijani.
 
Lazima waache angalau kastoo na sehemu ya kaofisi au hata kulala mlinzi, hivyo habari ya kwamba haionekani si kweli kabisa.
 
Nimeskia wakiongea kwenye daladala, sielewi kama ni kweli au la! ndo maana nimeuliza kama na wewe umeskia. Niliwahi kuskia huko iringa pia eti watengeza barabara nao walishindwa kuhamisha kaburi ili wapitishe barabara, ikabidi waipindishe kulipisha kaburi

Wakati wa ufanyaji wa TAM (Tathmini za Athari za Mazingira) kwenye miradi kama hii ya barabara huwa wanaangalia mambo kama haya, kuna makaburi mengine ni alama au ni kama sehemu za asili za wakazi wa eneo au jamii husika na wanatumia kama sehemu za ibada au ukumbusho wa jamii husika. Sehemu hizi huwa hazivunjwi ndio maana unakuta baadhi ya miti (mfano mbuyu wa pale Oysterbay St. Peter haukukatwa wakati wa ujenzi wa ile barabara maana ule mbuyu ni alama ya ile sehemu hata shule ya pale inaitwa Mbuyuni Primary School), na ndio maana hata kaburi la Iringa nalo likaachwa n.k. Mfano mwingine ni makaburi ya Karume Ilala.
 
Acheni kuendekeza ushirikina.

4.jpg

Physical forces of nature are sometimes no match to spiritual forces of nature!!!
 
Back
Top Bottom