Na sisi watu wa Mtwara na Lindi tunapenda maendeleo, tuachieni Dangote

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,317
Salama leikum!

Kila mmoja anafahamu historia ya mikoa ya Mtwara na Lindi tangu mkoloni,uhuru mpk sasa.

Mikoa hii imepitia magumu mengi sana kijamii na kiuchumi hasa kuanzia miaka ya 2010 kurudi nyuma.kiasi kwamba ilikua hata kujitambulisha mbele ya jamii kua unatoka Mtwara au Lindi unaona aibu kutokana na kudharaulika kwa mikoa hiyo kwa kua ilikua inaonekana ni maskini na wakazi wake ni duni.(wenyewe walikua wanaita "kusini").

Ikumbukwe tu miaka ya 1990 ilifikia hatua mtumishi akihamishiwa au kupangiwa kazi mtwara ilikua km ni adhabu kwake na wengi waliacha kazi.wakati huo kutoka dar kwenda mtwara unasafiri wiki mbili,Hali ikiwa nzuri unaweza kusafiri kwa siku 3,wakati huo soda ilikua inauzwa 500 wakati dar inauzwa tsh 150! hpo bado sijaongelea bei ya cement na vitu vingine.

Angalau sasa miaka ya hivi karibuni mikoa hii imeanza kufunguka kiuchumi hasa baada ya gesi kuanza kuchimbwa na barabara inayounganisha dar na mtwara kutengemaa..lakini cha ajabu imeonaka kutokea mambo yasiyo eleweka na yenye kuumiza vichwa.kwa nini kila linapokuja jambo jema kwa mikoa hii kunatokea figisu figisu zisizo eleweka?

1. Kulikua na reli ya Nachingwea ikang'olewa kipindi kile cha wakina Kawawa na Jk sijui sababu ilikua ni nini?

2.Ilipoanza kuchimbwa gesi tukaona sasa ndio nafasi pekee ya Mtwara na Lindi kua na viwanda Lukuki,tooobaaaa mara tunaskia hiyooo daslama kinyerezi watu wakapigana wee kupinga hili swala tukatukanwa na kuitwa hatuja soma mara hivi but ndo hivyo mwenye nguvu muite 'power'.

3. Tukapozwa na kiwanda kikuuubwaa na cha pekee cha Dangote ambacho ndio tunachojivunia watu wa mtwara na lindi,cha kushangaza zimeanza ishu zisizo eleweka eleweka mara hivi mara vile mwisho wa siku ndo itakua yale yale tu km ya reli na gesi.

Hivi sisi watu wa mtwara na Lindi tuna mkosi gani mbona kila jambo jema linapokuja kwetu lazima kutokee sintofahamu? au ndo kutokusoma kwetu kunapelekea haya yote? au kuna mtu yupo kati hataki mikoa hii ifanane na ya huko kwao?

Jamani na sisi tunapenda kuitwa 'mikoa iliyo endelea' tunapenda kutembea kifua mbele kwa kujivunia maendeleo ya kwetu km na nyinyi mnavyo vimba migongo kwa kujinasibu kua kwenu ni Dar,Mwanza,Arusha,Moshi,Tanga kume endelea.

Na nyie wabunge wetu acheni kulala mnatuangusha sana Dangote anaondoka huyu mmekaa kimya tuuu hata hatuwaskii mkipiga kelele? mbona wenzenu wachaga wanakuaga makini sana kutetea maendelea ya mikoa yao? au hii ya korosho kuuzwa alfu 4 kilo ndo mnaona mmesha maliza kazi? 2020 sio mbali mjue ohoooo!!!

INAUMA SANA UNAJUA.
 
Taarifa iliyotoka (mpya) ni kuwa kuna tatizo dogo tu la mitambo linashughurikiwa.

KADA
 
Inauma Sana, wanakusini tuanzishe vuguvugu kuliko lile la gesi, siipendi tufikie kuwaza kujitenga, tusiwe tena Tanzania maana wenzetu hawatutakii mema, please tuungane wanakusini ajira zetu zinapotea, cement ya bei rahisi inapotea, huyu dangote alisaidia huduma zingine, kwa kweli inauma Sana
 
Acheni ujinga sasa mtu anataka gesi apewe Bure ili b Iweje? Kwani akipewa Bure ndo mmepata ajira Lindi na mtwara wote? Hiki kiwanda lipo hapo na kimeajiri watu nje ya mtwara na Lindi kwani ajira ni qualification si ukaazi wa mtwara na Lindi.
 
Ifike sehemu waone haibu kwa kweli.. Nakumbuka wakati chuo cha Sauti, Kuna watu walikataa kutoa kibali kwa ajili ya ufunguzi wa chuo Mtwara, Dr Kitime akapeleka wanafunzi kwa nguvu

Pia hiki kiwanda Kuna watu walikua wanakataa kisifungulie kusini ni wizarani, Hawa Ghasia amepigana sana ili kiwanda kifungulie Mtwara , lile eneo lenye kiwanda Kuna watu walijifanya lao, hivyo walipwe mamilioni, wale wazee Wa madili, kama walivyokuwa wanazuia Lindi, pasijengwe mitambo ya kufua umeme, na kuchakata gesi, walijifanya eneo lao.. MUNGU AWALAANI WOTE
 
Tuna kiherehere na ccm acha tuisome namba.Wakija na kofia zao na t shart tunasahau kila kitu.
 
Salama leikum!

Kila mmoja anafahamu historia ya mikoa ya Mtwara na Lindi tangu mkoloni,uhuru mpk sasa.

Mikoa hii imepitia magumu mengi sana kijamii na kiuchumi hasa kuanzia miaka ya 2010 kurudi nyuma.kiasi kwamba ilikua hata kujitambulisha mbele ya jamii kua unatoka Mtwara au Lindi unaona aibu kutokana na kudharaulika kwa mikoa hiyo kwa kua ilikua inaonekana ni maskini na wakazi wake ni duni.(wenyewe walikua wanaita "kusini").

Ikumbukwe tu miaka ya 1990 ilifikia hatua mtumishi akihamishiwa au kupangiwa kazi mtwara ilikua km ni adhabu kwake na wengi waliacha kazi.wakati huo kutoka dar kwenda mtwara unasafiri wiki mbili,Hali ikiwa nzuri unaweza kusafiri kwa siku 3,wakati huo soda ilikua inauzwa 500 wakati dar inauzwa tsh 150! hpo bado sijaongelea bei ya cement na vitu vingine.

Angalau sasa miaka ya hivi karibuni mikoa hii imeanza kufunguka kiuchumi hasa baada ya gesi kuanza kuchimbwa na barabara inayounganisha dar na mtwara kutengemaa..lakini cha ajabu imeonaka kutokea mambo yasiyo eleweka na yenye kuumiza vichwa.kwa nini kila linapokuja jambo jema kwa mikoa hii kunatokea figisu figisu zisizo eleweka?

1. Kulikua na reli ya Nachingwea ikang'olewa kipindi kile cha wakina Kawawa na Jk sijui sababu ilikua ni nini?

2.Ilipoanza kuchimbwa gesi tukaona sasa ndio nafasi pekee ya Mtwara na Lindi kua na viwanda Lukuki,tooobaaaa mara tunaskia hiyooo daslama kinyerezi watu wakapigana wee kupinga hili swala tukatukanwa na kuitwa hatuja soma mara hivi but ndo hivyo mwenye nguvu muite 'power'.

3. Tukapozwa na kiwanda kikuuubwaa na cha pekee cha Dangote ambacho ndio tunachojivunia watu wa mtwara na lindi,cha kushangaza zimeanza ishu zisizo eleweka eleweka mara hivi mara vile mwisho wa siku ndo itakua yale yale tu km ya reli na gesi.

Hivi sisi watu wa mtwara na Lindi tuna mkosi gani mbona kila jambo jema linapokuja kwetu lazima kutokee sintofahamu? au ndo kutokusoma kwetu kunapelekea haya yote? au kuna mtu yupo kati hataki mikoa hii ifanane na ya huko kwao?

Jamani na sisi tunapenda kuitwa 'mikoa iliyo endelea' tunapenda kutembea kifua mbele kwa kujivunia maendeleo ya kwetu km na nyinyi mnavyo vimba migongo kwa kujinasibu kua kwenu ni Dar,Mwanza,Arusha,Moshi,Tanga kume endelea.

Na nyie wabunge wetu acheni kulala mnatuangusha sana Dangote anaondoka huyu mmekaa kimya tuuu hata hatuwaskii mkipiga kelele? mbona wenzenu wachaga wanakuaga makini sana kutetea maendelea ya mikoa yao? au hii ya korosho kuuzwa alfu 4 kilo ndo mnaona mmesha maliza kazi? 2020 sio mbali mjue ohoooo!!!

INAUMA SANA UNAJUA.
Afadhari muisome namba maana bwana yule mwingine alishinda kwa kishindo huko kweni sasa mnalalamika nini?
 
Dangote analeta maendeleo au kuchapa kwenu kazi ndio kunaleta maendeleo, acheni mambo ya ngoma, ngono na mfanye kazi muome kama hamtaendelea,,,
Watanzania bwana sijuhi tukoje mtegemea cha ndugu hufa masikini hamkeni
 
Acheni ujinga sasa mtu anataka gesi apewe Bure ili b Iweje? Kwani akipewa Bure ndo mmepata ajira Lindi na mtwara wote? Hiki kiwanda lipo hapo na kimeajiri watu nje ya mtwara na Lindi kwani ajira ni qualification si ukaazi wa mtwara na Lindi.
Acha upuuz wewe. Mtu mwenye akili timamu hawez kuwa na mawazo mgando, mpuuz mkubwa ww
 
Acheni ujinga sasa mtu anataka gesi apewe Bure ili b Iweje? Kwani akipewa Bure ndo mmepata ajira Lindi na mtwara wote? Hiki kiwanda lipo hapo na kimeajiri watu nje ya mtwara na Lindi kwani ajira ni qualification si ukaazi wa mtwara na Lindi.
Mpuuzi hupuuzwa....mchonyo wewe!
 
Munaozani mtwara na lindi ngome ya ccm hamuna takwimu, huku ccm deleted ila yule mzee wa malofa kapindua Sana matokeo,
 
Acheni ujinga sasa mtu anataka gesi apewe Bure ili b Iweje? Kwani akipewa Bure ndo mmepata ajira Lindi na mtwara wote? Hiki kiwanda lipo hapo na kimeajiri watu nje ya mtwara na Lindi kwani ajira ni qualification si ukaazi wa mtwara na Lindi.
Unajuwa wewe wacha kuwaita watu wajinga wana haki ya kusema maana mm niliwahi kusoma pale TTC mtwara ilifika wakati umeme ulikosekana mtwara kwa wiki mbili je ingekuwa musoma
Dangote analeta maendeleo au kuchapa kwenu kazi ndio kunaleta maendeleo, acheni mambo ya ngoma, ngono na mfanye kazi muome kama hamtaendelea,,,
Watanzania bwana sijuhi tukoje mtegemea cha ndugu hufa masikini hamkeni
Kwakweli wakazi wa kusini wanasema ukweli mimi niliwahi kusoma TTC pale mtwara ilifika wakati umeme hakuna mji mzima kwa wiki mbili hivi Ingekuwa mwanza musoma au kagera ingekalika hii McGill?? wacheni waseme maana hamuwaambii ukweli
 
Mkuu,
Natamani uwe na adabu kidogo unapochangia humu jf. Kuwaambia wenzio ni wajinga halaf weye unatoa pumba za lipumba humu ni mbaya sana.
Hata kama dangote angepewa gas ya bure, ni afadhali kwani alikuwa na nia nzuri tu ya kutupa cement ya karibu na bure pia. Hivyo vitu vingelikuwa ni Bure kwa Bure. Ova and autiiiii kabisa
 
Ifike sehemu waone haibu kwa kweli.. Nakumbuka wakati chuo cha Sauti, Kuna watu walikataa kutoa kibali kwa ajili ya ufunguzi wa chuo Mtwara, Dr Kitime akapeleka wanafunzi kwa nguvu

Pia hiki kiwanda Kuna watu walikua wanakataa kisifungulie kusini ni wizarani, Hawa Ghasia amepigana sana ili kiwanda kifungulie Mtwara , lile eneo lenye kiwanda Kuna watu walijifanya lao, hivyo walipwe mamilioni, wale wazee Wa madili, kama walivyokuwa wanazuia Lindi, pasijengwe mitambo ya kufua umeme, na kuchakata gesi, walijifanya eneo lao.. MUNGU AWALAANI WOTE
Hata hii naona watu inawauma sana. Kusini imesababishiwa umaskini wake. Mtwara corridor iko wapi. Rais wa Awam ya tatu alipigania sana, hadi akina Bakili Muluz walikubali wakasign MOU, Mzee ile anamaliza tu utawala wake Mtwara Corridor ikatupwa huko. Leo haitajwi kabisa.
 
Dangote analeta maendeleo au kuchapa kwenu kazi ndio kunaleta maendeleo, acheni mambo ya ngoma, ngono na mfanye kazi muome kama hamtaendelea,,,
Watanzania bwana sijuhi tukoje mtegemea cha ndugu hufa masikini hamkeni

kweli mkuu! wale wa mtwara na lindi waache ngoma na ngono.

Na sisi wa uku tuache singeli, vigodoro, disco na dada poa
 
Unajuwa wewe wacha kuwaita watu wajinga wana haki ya kusema maana mm niliwahi kusoma pale TTC mtwara ilifika wakati umeme ulikosekana mtwara kwa wiki mbili je ingekuwa musoma

Kwakweli wakazi wa kusini wanasema ukweli mimi niliwahi kusoma TTC pale mtwara ilifika wakati umeme hakuna mji mzima kwa wiki mbili hivi Ingekuwa mwanza musoma au kagera ingekalika hii McGill?? wacheni waseme maana hamuwaambii ukweli
tena sio wiki mbili ilikua unakatika miezi miwili unaambiwa mpk mafuta yaje kwa meli kurun mitambo ya tanesco kipindi kile tanesco ya mtwara wanatumia majenereta kutengeneza umeme.
 
Hawatupendi watu wa Kusini mijitu ina roho ngumu kama wanyonya damu..hivi waziri Mwijage huwa anachokiongea anakifikiria mara mbili kweli mana sometimes kama kuna fyuzi zimeungua
 
Mimi sipendagi ujinga. Hivi gesi mnafkiri inatoka ardhini Bure haina gharama za uendeshaji? Kwahiyo Dangote ndo alikuwa a naleta maendeleo hapo kwenu mtwara na Lindi asingejenga kiwanda msingi Pata maendeleo?

Halafu wengine walivyo wajinga wanazungumzia ccm. Ccm imefanyaje sasa hapo Dangote?

Mtwara yote ni CUF na LINDI.

Narudia tena acheni ujinga JF.
 
Back
Top Bottom