Na Sisi tuwasusie madaktari kuwapa huduma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na Sisi tuwasusie madaktari kuwapa huduma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Boligado, Jun 25, 2012.

 1. B

  Boligado Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani wadau kwa jinsi hali ilivyo kama wao wamekataa kutupa huduma na sisi tuwasusie kuwapa huduma kama wao wanavyofanya kwa jamii. Wahasibu wasiwalipe mshahara yao na hata huduma nyingine pia tuwatose. Tusiwafundishe watoto wao hata wakija na hela yao na huduma nyinginezo...mgogoro wauletao wanaoumia ni watanzania maskini na sip viongozi wa serikali. Mgogoro huu Pinda. Hawa ghasia.Mwinyi aathiriki nao n.k
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Kila 1 agome?
   
 3. mandella

  mandella JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,635
  Trophy Points: 280
  Cjaelewa tija yako ni kujenga ama kubomoa !! Sidhani kama unawezana na Familia yako !! Ina maana mke wako akigoma kupika na ww unagoma !! Bila kujali hali ya watoto !! Tulia na tafakari upya kauli yako ! !! To hoja za kujenga na kusaidi kupata muafaka na si kubomoa !!

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 4. B

  Boligado Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jino kwa jino ndio waone umuhimu wa kada nyingine. Pia muathirika wa kwanza kwenye ni mtanzania maskini ategemeae gov. Hospitals ambazo viongozi wengi. Watu wenye kipato kikubwa hawajui hizo hospital zinanafanaje
   
 5. B

  Boligado Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tija yangu ni kujenga na kufanya kila mmoja wetu afikiri bila ubinafsi
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  mgomee dhaifu acha kuhangaika na madaktari, mambo yao yakiwa mazuri hata wewe utafurahi
   
 7. mandella

  mandella JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,635
  Trophy Points: 280
  Tatizo wabongo tumelewa Siasa !! Kila ki2 tunafanya siasa !!

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,347
  Likes Received: 10,485
  Trophy Points: 280
  wewe ndugu yangu ni diwani nini?  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 9. a

  alibaba Senior Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuwaona Madaktari wetu Wanajiweka katika nafasi ya kuwa Miungu watu kwa kuwasaliti Wananchi wenzao. Haiwezekani kuwa Ninyi ndio wenye Shida na mnalipwa haba kuliko fani nyingine, huo wenu ni UROHO, TAMAA, TABIA MBAYA, WIVU, UJINGA na kuelimika kulikowavua USTAARABU, kwa msemo wa jamaazetu wa Visiwani HAMFAI PESA MBILI gomeni msubiri kujaza MATUMBO YENU kwa TAMAA halafu tuone MSIENDE CHOONI!!.....................!!
   
 10. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani wito kutoka kwa madaktari ni kuwa fani zote mgome hapo ndio itakuwa sawia kabisa

  Ila kuna watu wengi humu naona uelewa wao ni mfupi au ndio wanaokula mkate wa wa tz
   
 11. B

  Boligado Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kosa kubwa kwa serikali ni kuhurusu watumishi wa sekta ya afya kufanya kazi za nje baada ya kumaliza kuhudumia kwenye hospital za umma. Ili wapate akili serikali inabidi kuondoa hili kwenye taratibu za ajira za watumishi wa sekta hii.

  Wakiwa na mahali pamoja pa kushika huenda wataona umuhimu wa kudai maslahi yao kistaarabu na sio kwa stahili hii ya kuumiza/kuua watanzania maskini
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani hao ni wake za madaktari?
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JF imeingiliwa! Tigo imeanza kutumika kufikiri namna ya kutatua mambo magumu.
   
 14. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu ubinafsi unaosema ni upi? Kudai uboreshwaji wa huduma ktk hospitali zetu au kwenda kutibiwa Apollo?
  Kama huelewi wanachodai, si ungeuliza tu au ukakaa kimya.
  Duh, usingizi una shida kweli.
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  Jamani swala hili la mgomo wenzenu nalitazama katik mambo mawili tofuti.

  Nautizama mgomo huu kama sehemu ya kuishinikiza serikali iwaangalie upya katika kile wanachokifanya. Binafsi numia sana na mishahara na posho ndogo wanazopewa au wasizopewa kama ni halali yao.Serikali haijui ipriotise wapi na kwanini na tena haijui nani ni muhitaji katika taifa hili. Inasikitisha kuona wabunge wanakaa na kudai nyongeza za maslahai yao kwa kuongea tu bungeni tena kusikokuwa na tija na anasikilizwa mara moja na kuongezewa posho hizo lakin mtumisha wa serikali kama huyu ambaye mazingira anyofanyia kazi siyo pendwa, kazi yenye ni risk na malipo pia. mungu na atusaidie jamani.

  kwa upande mwingine namuonea huruma sana yule mtanzania wa kawaida anayehitaji huduma hospitalini na hajaipata kisa mgomo huu kweli inasikitisha sana.

  lakini namuonea huruma zaid askari aliyekesha usiku kumlinda huyu dr na malizake na kwa bahati mbaya akapata ajaliaaaa wakati wa patrol ama akavamiwa na majambazi na sasa anahitaji na hana mtu wa kumuhudumia.

  pia namuonea huruma sana tena sana mwalimu mwenzangu wa sayansi kama mimi ambaye muda huu alikuwa anaandaa practical ya chemistry na kwa bahati mbaya sana the conc. acid spilled na ikamuunguza na sasa anhitaji huduma za kitabibu lakini ameshindwa kuzipata, akaamua kwenda private hosp akiwa na kitambulisho chake cha bima lakini bima yake ni brown card, hakubaliki kutibiwa hosp yeyote ile kisa bima hii ni ndogo kiasi kwamba huduma anayoweza kupatiwa ktk hosp hizi hakuna.Jmani naandika hii post nikiwa nalia kwa uchungu sana serikali imetufanya tumekuwa watumwa kwenye nchi yetu, sisi tunaokesha kufundisha hawa madaktari lakin mwishowe shukurani inageuka kuwa ya punda. basi hata kabima tupewepo kazuri ni hako ka brown kadi kasiko na lolote.

  najiuliza mimi mwl mwenzangu kapata ajali maabara kaenda hosp kakosa huduma je mimi niendelee au niondoke? nikisusa maskini hawa watoto wa wakulima nitawalostisha damu yao nitadaiwa siku moja. pengine kwa kuwafundisha siku ya leo Mungu alitegemea niwavushe daraja moja kwenda jingine je nikisusa sinitawakwamisha?

  lakini pia hawa baadae hawatakumbuka kwamba niliwafundisha manake hata hao waliogoma wanasahau kwamba kuna waalimu walichangia sana kuwafikisha hapo walipo na leo hii ni mgonjwa hoi na ni mzee hana jinsi inabidi afie kitandani kwa kukosa huduma.

  Mungu najua uko fair sana basi tusikilize sisi waalim ambao hatuna uwezo wa kutibiwa private na sasa ni wagonjwa kwaajali ya maabara pengine na mmoja wa hawa wanafunzi ni mtoto wa huyo daktari lakin hatuna msaada pesa cash hatuna tunadhalilika na si kwamba hatufanyi kazi zetu ee Mungu tuhurumie sisi waja wako. nimesema silii tena nakaa kimya na najua Mungu atatupa msaada tu.wabarikiwa sana madaktari wa hosp ya hurbert kairuki walio amua kutusaidia kumuhudumia mwenzetu kwa mkopo. mungu ameona moyo wenu atawajaza zai na zaid.

  Kikwete tunakufa talk something gentleman
   
 16. Kalolo Junior

  Kalolo Junior Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mi nadhani wanachofanya Madaktari ni kuwawakilishi watumishi wengine wa Umma juu ya hali duni ya mazingira ya kazi katika Utumishi wa Umma. To me, they are just representatives kutokana na unyeti wao, it will attract more Goverment attention na kuliko wangegoma Proffession nyingine kama Wahasibu.
   
 17. B

  Boligado Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Haya mi na wewe nami anafikiri kwa kutumia.... wakati mwingine ukiishiwa hoja kaa kimya siyo kutujazia ***** humu ndani
   
 18. RubenM

  RubenM Senior Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo Jamaa hajielewi hata kidogo, hajui serikali Yake ndio imegoma then madaktari wamerespond????
  Alf anadhani uzalendo upo Kwa hiyo serikali??? Awaambie viongozi waache rongorongo bkoz miezi yote imepita wakiahidi kulimaliza kumbe siasa na porojo.. UTUMWA KWA WANASIASA UKOME... wanasema wamepandisha malipo ktk ukaguzi Wa Maiti wakati hao Madaktari ni takriban 11 tu nchi nzima.. UHUNI HUO
   
 19. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania maskini tunao umia, serikali yetu ndo inayotuumiza sababu imechangia kwa kiasi cha asili mia 100, kutufanya masikini na kutotupatia huduma za kijamii. inaingia akilini hospitali kukosa vitanda, urine bags nk.
   
 20. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,285
  Likes Received: 3,015
  Trophy Points: 280
  Huuuh..am speechless..
   
Loading...