Na MWANDISHI wa Globe & Mail, Michael Posner: JK: Tunahujumiwa;upotoshaji kuhusu Miradi ya Maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na MWANDISHI wa Globe & Mail, Michael Posner: JK: Tunahujumiwa;upotoshaji kuhusu Miradi ya Maendeleo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMAMOSI, OCTOBA 06, 2012 08:23 NA MWANDISHI MAALUMU, OTTAWA


  RAIS Jakaya Kikwete amesema, anashangazwa na jitihada za upotoshaji wa makusudi wa ukweli kuhusu miradi ya maendeleo, inayobuniwa na kuanzishwa na Serikali yake.

  Hata hivyo, Rais Kikwete amesema upotoshaji huo, hautaifanya Serikali yake ibadili uwamuzi wake kuhusu miradi ya maendeleo ya wananchi, ama kuacha kubuni miradi mipya.

  Rais Kikwete, alitoa kauli hiyo juzi wakati alipohojiwa na mwandishi wa habari mwandamizi wa Gazeti maarufu la Canada la Globe & Mail, Michael Posner.

  Katika shughuli ya kwanza, Rais Kikwete alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo jitihada za Serikali kuendeleza kilimo na mipango ya kujenga barabara kupitia Loliondo.

  "Kamwe hatujapata kuwa na mipango ya kujenga barabara ya lami kukatisha Mbunga ya Serengeti. Huu ni upotoshaji wa kushangaza. Najua ni upotoshaji wa makusudi, hata kama sijui unaanzia wapi. Nadhani watu hawa wanataka kunihujumu tu,

  …tumesema na kusema tena kuwa, tunalo jukumu la maendeleo kwa wananchi wote, wakiwemo wa Loliondo na Mugumu, ambao tumesema tutawajengea barabara ya lami."

  "Tunajenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 11,000 ili kuunganisha nchi nzima. Hivyo, wananchi wa Lolindo na Mugumu, nao watakuwa sehemu ya maendeleo haya makubwa ya barabara. Hakuna mtu atakayepitisha barabara ya lami ndani ya Serengeti.

  Kwa hakika, kwa upande wa Loliondo, barabara ya lami itaishia kiasi cha kilomita 80 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti."

  Alipoulizwa kwa nini Serikali yake haionyeshi uchangamfu mkubwa kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kupitia Kusini mwa Serengeti, badala ya barabara hiyo kupita Kaskazini ndani ya mbunga, kama inavyopendekezwa na baadhi ya wafadhili, Rais alisema, "Tunakaribisha wazo na ujenzi wa barabara kusini mwa Serengeti, lakini barabara hiyo haitakuwa jibu la matatizo ya usafiri kwa wakazi wa kaskazini. Barabara ya kusini itahudumia watu wa kusini na wala siyo watu wa kaskazini."

  Kuhusu suala jingine ambalo linachochewa kwa njia nyingi na kwa kila namna kuwa, Serikali inapora ardhi ya wakulima wadogo na kuitoa kwa wakulima wakubwa, ili kufanikisha mageuzi ya kilimo nchini, Rais alisema:

  "Huu ni upotoshaji mwingine wa mipango yetu ya maendeleo. Sijui upumbavu huu unatoka wapi? Tunchofanya sisi chini ya mipango yetu ya kuleta mageuzi katika kilimo cha Tanzania, ni kumsaidia mkulima mdogo kwa kulinda na kuiendeleza ardhi yake, ili kumwokoa na njaa, kumpunguzia umasikini na kuongeza usalama wake wa chakula.

  Hakuna mkulima mdogo ambaye atanyang'anywa ardhi yake, katika mipango yetu ili apewe mkulima mkubwa."

  Hata hivyo, Rais Kikwete amemwambia mwandishi huyo kuwa upotoshaji huo, hautaifanya Serikali yake kuogopa na kushindwa kutelekeza majukumu yake ya maendeleo kwa wananchi kama ilivyoahidi kwenye Ilani yake ya uchaguzi Mkuu.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni kwanini anaenda kulalamika NJE YA NCHI ? Kweli huo ni UZALENDO ? au kuuza SIRI za NCHI ? Ameshindwa kuwashawishi Wananchi na Wapinzani kuhusu Miradi ya Maendeleo kuwa ni ya kihalali na ni sawa ?

  Basi kuna Uwalakini...
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Aende Kisarawe aniambie kuwa ni uwongo kuwa raia hawakuhamishwa ili mzungu anayelima jathropa apate ardhi. Kuna mkazi mmoja alikuwa akijiendeshea biashara yake ya mkaa pale akipata pato la dola 150 kwa mwezi ( si haba) na baada ya mzungu kuchukua ardhi yake na kumwajiri analipwa sasa dola 50 kwa mwezi. Je, ni maendeleo hayo?
   
 4. m

  malaka JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mbona hajasema katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi amekimbilia kwa wafadhili wake? Mh hali mbaya sana tz zaidi unavyojua wewe. Yaani raisi anashindwa kuwachukulia hatua hao wanaohujumu anabaki kulalamika kweli?
   
 5. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwe wazalendo, kwa hili na mengine kama haya ni kweli Tanzania inachafuliwa na majirani zetu kwa makusudi kwa kuwa wanatuonea wivu.
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hutu jamaa yeye kila kulalamika Hilo la Serengeti ameliongea sana na watu walishagundua janja Yake anataka hotel zake zipate wateja wafungue na airport mugumu ili watupige vizuri. Tatizo lake ajuikuwa hao wandishi uwa wanafanya research kabla ya kuuliza au kuandika
   
 7. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Huyo ndio JK na majibu DHAIFU
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Really?
  Jinsi alivyojibu, yaelekea haijui hata hiyo miji inayozungumziwa zaidi ya kurudia maneno yaleyale yaliotumiwa na yule mwandishi wa Kikanada. Pia Rais anasema hakuna mwanakijiji aliyenyang'anywa ardhi yake na kupewa wawekezaji. Tumeshuhudia huko Mbalali hao wawezekezaji walivyopora ardhi na serikali inawapa ulinzi. Barrick Gold Mine kule Tarime, je Unataka tumsaport Rais kwa kusema uongo? Je umepata kukaa na wanavijiji waliodhurumiwa ardhi yao na kuongea nao au kuona wanavyoendesha maisha yao baada ya huo uporaji?
  I'll never ever support this guy who is pathetic liar and his corrupted government.
  Mkuu labda wewe ndio wale 1% mnaofaidi Tanzania na kusahau mlipotoka. keep it up, but God don't like ugly
   
Loading...