Na misiba mingine ikitokea iwe kama huu wa Arusha

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Ajali na majanga yanaweza kutokea mkoa, wilaya au kijiji chochote nchini. Msiba huu wa watoto wetu wa Arusha ulitugusa karibu taifa lote. Naomba majanga kama haya yatakapotokea sehemu nyingine yoyote ya jamhuri yetu mwiitikio uwe kama huu huu na hivihivi kama Arusha. Nadhani huko nyuma tulilega sana, maana msiba ni msiba bila kujali ni wa raia, askari, watu wazima, watoto au umetokea mkoa gani.
 
Social media imesaidia sana kuhamasisha wengi kufuatilia hii ajali ya iliyochukua maisha ya hawa malaika. Nimegundua watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanatoka Arusha.
 
Nikajua unaomba Mungu atuepushie mbali misiba ya namna hiyo kumbe bado unaiombea iendelee kutokea ili tushikamane.

Hatuhitaji misiba ndio tushikamane, tunatakiwa kushikamana kila siku iwe kazini, mitaani, shuleni, hospitalini nk. Team work ndio silaha ya kusonga mbele kiuchumi, kisiasa, kidini na kijamii.
 
Feelings au mindsets hafundishwi mtu ila ni namna gani jamii fulani inavyoishi Katika kujali utu wa mwanadamu ktk malezi toka utoto wao na matokeo kwa kizazi na kizazi hiyo ni moja.

Lakini pia msiba inategemea na umewagusa watu kwa kiasi gani,kama ni kiongozi ulikuwa unawatumikia watu kwa moyo upi,kama hawa Watoto maskini ya MUNGU ni kama malaika tu ndiyo maana umeona Taifa linalia kila kona.

Hatuombei msiba mwingine kama huu ktk Taifa la Tanzania MUNGU apishie mbali kabisa.
 
Hapa si msiba wa kawaida.wanafunzi 32.kwa wakati mmoja.ni zaidi ya huzuni.binafsi wakifariki watu wazima uwa sishtuki sana maana tumezoea kusikia haya.ila kwa wanafunzi au watoto.inakuwa huzuni sana.
 
Social media imesaidia sana kuhamasisha wengi kufuatilia hii ajali ya iliyochukua maisha ya hawa malaika. Nimegundua watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanatoka Arusha.

Sikiliza argument ya mwandishi, na ujiba sawia, kwa hiyo social media imeanza baada ya hii msiba?
 
Hatari sana. Badala ya kusema tufanye nini msiba nwingine kama huu usitokee tunasema msiba mwingine ukitokea uwe kama huu.

Tushakubali kwamba hii misiba ya watu kufa mafungu kila mara haiepukiki kama kuchomoza kwa jua.

Anzisha uzi wako kujadili nini kifanyike ajali zisitokee watu watakuja kujadili kama una hoja.
 
Hatari sana. Badala ya kusema tufanye nini msiba nwingine kama huu usitokee tunasema msiba mwingine ukitokea uwe kama huu.

Tushakubali kwamba hii misiba ya watu kufa mafungu kila mara haiepukiki kama kuchomoza kwa jua.
Ajali kama hizi huwa zinatokea hata nchi kubwa zilizoendelea. Princes Daina alifia Ufaransa, huricans, ajali za ndege, mafuriko, kuzama kwa meli, nk. Tofauti pekee ni namna tunavyoyashughulikia mambo yakiharibika kama ilivyotokea Arusha, Kagera, Kigoma, Morogoro, Rufiji, JaribuMPAKANI, nk.
 
Hapa si msiba wa kawaida.wanafunzi 32.kwa wakati mmoja.ni zaidi ya huzuni.binafsi wakifariki watu wazima uwa sishtuki sana maana tumezoea kusikia haya.ila kwa wanafunzi au watoto.inakuwa huzuni sana.
Shauritanga?
 
Ajali kama hizi huwa zinatokea hata nchi kubwa zilizoendelea. Princes Daina alifia Ufaransa, huricans, ajali za ndege, mafuriko, kuzama kwa meli, nk. Tofauti pekee ni namna tunavyoyashughulikia mambo yakiharibika kama ilivyotokea Arusha, Kagera, Kigoma, Morogoro, Rufiji, JaribuMPAKANI, nk.
Ajali kama hizi?

Unafananisha hurricane na ajali ya gari?
 
Wa Arusha umepata kick kwa sababu ya watoto. Wangekuwa watu wazima mchanganyiko ingekuwa kama kawaida kama jana
 
Je, kama wale watoto wetu (Shule ya Lucky Vincent) waliopoteza maisha kwenye ajali mbaya Mkoani Arusha wangekuwa wanasoma Shule zetu za Kata muitikio ungekuwa ni kama ulivyo sasa?
Je Msiba ungekuwa mkubwa hivi hivi kama ulivyo sasa au ungekuwa ni tofauti? Tuseme Watoto hawa wangekuwa wanasoma Shule ya Msingi Mtakuja, Rufiji, ...
 
swali lako halina mantiki!

Nitakurudisha nyuma kwenye tukio la shule ya shauritanga tofauti ya wakati ule na wakati huu ni maendeleo ya mawasiliano na teknolojia! na pia wakati huu wananchi wana demand zaidi kutoka kwa viongozi wao sio zama zile! kwakuwa tunaona wafanyavyo wenzetu duniani.
 
Dah.... Badala ya kujifunza yasitokee kama ya Arusha.... Tunazidi kuombea? Wauza majeneza utawajua tu
Mleta mada labda mchawi, eti msiba mwingine uwe kama huu wa Arusha! Wewe subiri siku akiwamo mtoto wae tuone kama ataombea uwe kama wa Arusha.
 
Mleta mada labda mchawi, eti msiba mwingine uwe kama huu wa Arusha! Wewe subiri siku akiwamo mtoto wae tuone kama ataombea uwe kama wa Arusha.
Ajali kama hizi zitaendelea kutokea tu, maana mfumo wetu wa upatikanaji wa madereva, leseni, spea za magari, ajira, mafundi magari, ukaguzi wa magari vyote ni feki. Ninachosema hapa ni namna tu ya kushughulika na majanga ya aina hii kama yakitokea. Kwangu mimi msiba ni msiba na mfiwa ni mfiwa. Hata kama ajali ikipoteza watu wawili lakini familia zilizopoteza watu wao zitapata majonzi yaleyale sawa na ajali iliyopoteza watu 70. Hivyo hata hizo familia 2 zilizopoteza watu wao kwenye tukio kama mafuriko, kuzama kwa meli, mauaji, matetemeko, kuanguka kwa treni, kufukiwa na vifusi migodini, kuunguliwa na mabweni, n.k, zinahitaji kufurijiwa kwa aina yake bila kujali ni mkoa gani..
 
Back
Top Bottom