".....na Mheshimiwa Rais nimeishamwambia" Mheshimiwa Makinda.

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,811
2,000
"'...Vijana woote waliomaliza Form Four watafanyiwa sensa wajulikane wako wangapi...hawa ndio 'watakao saidia kuendeleza' kilimo kwanza...... na Mheshimiwa rais nimeishamwambia."' Mheshimiwa Makida alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Njombe (Rejea Taarifa ya ITV jana saa mbili usiku). Tatizo langu wanaJF ni uhalali wa Mh. Makinda kutoa kauli hiyo kama yeye ndio msemaji wa serikali. Kwa maoni yangu, inaonekana hakuna mgawanyo wa majukumu ya nani aseme kipi na nani afanyelipi kulingana na nafasi aliyonayo.
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,337
2,000
May be hajui kazi yazke ni nini?? Ngonja moto utakapowashwa bungeni next year na akina Lissu ndipo atjua kazi yake ni ipi!!
 
Mbaha

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
697
225
"'...Vijana woote waliomaliza Form Four watafanyiwa sensa wajulikane wako wangapi...hawa ndio 'watakao saidia kuendeleza' kilimo kwanza...... na Mheshimiwa rais nimeishamwambia."' Mheshimiwa Makida alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Njombe (Rejea Taarifa ya ITV jana saa mbili usiku). Tatizo langu wanaJF ni uhalali wa Mh. Makinda kutoa kauli hiyo kama yeye ndio msemaji wa serikali. Kwa maoni yangu, inaonekana hakuna mgawanyo wa majukumu ya nani aseme kipi na nani afanyelipi kulingana na nafasi aliyonayo.

Huyu mama hana sera!!! Hivi hiyo sensa ni ya nini hasa??? Kama anataka idadi ya form four leavers hiyo si inapatikana wizarani kirahisi kabisa!!! Hii kweli ni Serikali ya kifisadi zaidi ya mno!!! Hapo ameshakosa njia ya kula hela zetu sasa anaanza kubuni upupu huo!!!! Hivi hawa viongozi wa CCM ni wakizazi gani hawa???!!!
 
limited

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
312
225
hiyo kwa serekal.i ya jk iko sana wazair ana sema hiki leo, kesho waziri mwingine kile.... kombana hatuhitaji katiba mpya pindaa kasema inahitajika kaaazi kwelikwel.
 
RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,373
2,000
Mimi niliposikia kashinda uspika, nilishangaa kwani huyo mama hana kiwango ni majungu pale mjengoni tusubiri tuone. Hana mwelekeo wa kutupa kile tunachotaka sana sana atatuchelewesha kupangua wachezaji kwenye timu yetu ya serikali.

Mama ajirekebisha na its too late for her.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
42,891
2,000
siku hizi kila kituu ni form iv leavers...walimu, polisi..., wanajeshi... soon tutaskia hata madaktari...! maana dhana ya kufunza mabwana shamba hamna tena
 
RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,749
1,250
Countries are talking of university education, our poor old lady is talking of secondary education? Poor us!
 
Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Hii ni bongoland bwana, mgawanyo wa madaraka ya dola siyo utamanduni wetu. kwetu sisi kipaumbele ni mshikamano na umoja. Ukianza kuendekeza huu utamanduni wa kugawanya madaraka ya dola kwa mihimili mitatu hisiyoingiliana huo ndiyo utakuwa mwanzo wa kuvunjika kwa utulivu tulio nao. Huu ni mwanzo mzuri kwa Makinda, siku zote ni lazima kuhakikisha anafanya kazi yake sambamba na serikali.
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,544
2,000
tatizo kila mtu anajisemea tu, no thinking, look Kombani alivyotofautiana na PM kuhusu katiba, Look huyu Makinda kinda sasa waliomaliza F4 hata ukiwa na sensa je waliojiunga na A-Level hadi University itakuwaje? what kind of sensa? idadai ya wanaoliza fm4 inajulikana, eti ndio watakaoendeleza Kilimo kwanza? Vituko hivi, just talking, talking, no thinking, hivi vichwa vingine are totally VACUUM inside i believe so
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,200

Sifa aliyojipatia nayo uspika ni kwamba yeye ni mwanamke, basi! Mizigo mingine mnamwonea tu jamani!
 
Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,395
1,500
jamani lakini si amevaa kofia mbili? pale nadhani alikuwa anaongea kama mbunge njombe na si spika wa bunge la ccm & cuf
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
53,586
2,000
bora angrsema wafungwa na watu wa kujitolea ndio waendeleze ..huyu mama ni mwehu tena naruda tena ni mwe** Tanzania watu wangapi hawaana kazi na wapo vijijini tu bila la kufanya?? iweje leo urukie watoto wa shule? huyu anatofauti gani na mbakaji? au anajitafutia laana kama yeye ni mwanamke wa kweli aanze kuwapeleka wanae kwanza si anao watoto wa kike nawajua sana wapo dodom wanachakachua tu mitaani awapeleke wakalime kwanza ndio aongelee wanetu mi nna hasira
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,776
2,000
He! Kwahiyo hao vijana ndio watashika majembe au?
Sa zingine kukaa kimya ni busara zaidi.
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,666
2,000
mmesahau kuwa ni mmbunge/

ni kweli, yeye ni mbunge na amelisemea hilo jimboni kwake, lakini mkuu wa mkoa ndiye aliyepaswa kulisemea, kama sio mkuu wa mkoa basi mkuu wa wilaya, hata kama idea hiyo ilikuwa yake angeidelegate kwa wakuu hao waitangaze. Tunaposema Tz kuna leadership vacuum hii yaweza kuwa ni tafsiri moja wapo
 
Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593

hakuna mahali popote duniani penye uongozi huo unaousema. umeshindwa kuelewa maana ya delegation. probably point yako iko katika mising ya kikatiba lakini si si misingi ya kiuongozi
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,143
2,000
Labda hajui maana ya sensa... si taarifa na takwimu zipo kuanzia miaka, jinsia zao, majina yao, anuani zao, sasa alikua anaongea ujinga gani? samahani kwa kutumia lugha kali but i hate speech za kijinga, huwezi kusimama mbele ya watu uwadanganye au uongee upupu kama huo, ndio yale yale ya kila shule kuwa na laptop kwa kila mwanafunzi...sijui kinachowafanya waropoke ni nini?!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom