Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,944
- 18,653
- Thread starter
- #81
Usishangae siku kumo unaambiwa hata takwimu za watumishi hewa nazo zilikuwa hewa!Hatukatai utawala bora na demokrasia vikawa vimojawapo kwenye ukuaji wa uchumi lakini sio sana.Unataka watu walambwe miguu ili walipe kodi bila kutumia nguvu unadhani inawezekana,wafanyabiashara wanaingiza biashara zao kimagendo hawalipi kodi na wengine hata kudanganya vipato vyao.Wanachukua mishahara hewa,elimu hewa. Watu wanaphd hewa unadhani watafanya uchumi ukue,tambua huo utakuwa uchumi hewa uliokua.Sasa anapokuja kiongozi anayetumia nguvu ili hayo mambo yasikuwepo watu mnasema hakuna demokrasia,utawala wake ni wakimabavu kumbe yeye ndio anaiweka nchi katika hali ya ukweli na sio wa kihewahewa tu.Acha tupigike tu lakini matumizi ya kodi zetu tunaziona huyo anayesema uchumi unashuka ataendelea kuangalia tu hiyo statistics yake na wengine tutaangalia statistic yetu ya maendeleo.Hapa kazi tu.