Na Kwa Hili UDSM/Mlimani Tukigoma Tufukuzwe!?

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Tukiwa na siku tatu, tu toka tufungue chuo baada ya kuwa na likizo ya wiki tatu, hakuna Boom (yaani hela ya kujikimu tukiwa chuo) cha ajabu ni kwamba hela hii aliyepewa dhamana ya kutoa hela hizo ni chuo, hapo awali bodi ya mikopo ndiyo walikuwa responsible.
Asilimia 75% ya wanachuo wa mlimani mpaka sasa hawajaripoti chuo kutokana na sababu mbalimbali kubwa ni kutopata boom kwani wengi wa hao hutegemea boom kwa nauli na kulipa ada.
Nawasilisha
 
Huu ni uzembe mwingine kati ya 'zembe' nyingi zitokanazo na tume zinazoundwa na rais. Na vile vile ni ushahidi wa jinsi wasomi wa serikali wanavyoshindwa kutoa muongozo wa kutatua kero za wananchi.
Kwa nini hizo tafti hazikushirikisha wanafunzi hata kupitia midahalo ili kupata maoni juu ya utoaji mikopo kupitia vyuo? Mimi naamini wanafunzi wangekuwa na maoni ya msingi kuliko vichwa vya hawa wasomi wa serikali.
Sasa haya yanatokea, bado tuwalaumu wanafunzi wakigoma? Siku za masomo ndo zinaishia, je wakuu wa vyuo wanafanya nini kuzuia hilo? Poleni wanafunzi.
 
Ahsante ndugu, ndiyo UDSM hiyo, tungependa wote mliosoma hapa na wazawa mjue kuwa UDSM ina kero nyingi sana tena nzito, wanachuo hawapewi nafasi ya kuziwakilisha, wakitaka kuziwasilisha ndo hayo mnayoyasikia kwenye vyombo vya habari "UDSM yawatimua wanachuo kadhaa"
 
Mkuu nilishaandika siku nyingi kwamba hazina ya serikali imekauka, haina hela za kuwalipa wanafunzi vyuoni. Nikatolea mfano chuo cha SAUT sasa mwezi unaenda kuishi hakuna hata tetesi za boom, wengine wakaponda eti SAUT huwa wanakiherehere cha kufungua mapema. Najua UDSM pressure yenu nikubwa, andamaneni kwani hivi sasa huwezi kudai kitu serikalini mpaka uwape pressure na madhara kutokea.
 
Inasikitisha sana tena ni udhalilishaji mana hizo fedha tunakopeshwa na si za bure, Sua kuna wanafunzi zaidi ya 780 hawajapewa fedha za meals and Accomodation pamoja na facult allowance tangu mwaka huu wa masomo ulipoaanza.... huu ni unyanyasaji... serikali inakosaje fedha wakati hata napotuma hii post nimelipa kodi?
 
Mkuu nilishaandika siku nyingi kwamba hazina ya serikali imekauka, haina hela za kuwalipa wanafunzi vyuoni. Nikatolea mfano chuo cha SAUT sasa mwezi unaenda kuishi hakuna hata tetesi za boom, wengine wakaponda eti SAUT huwa wanakiherehere cha kufungua mapema. Najua UDSM pressure yenu nikubwa, andamaneni kwani hivi sasa huwezi kudai kitu serikalini mpaka uwape pressure na madhara kutokea.

Mkuu woga tuliojengewa sasa kutokana na wenzetu kufukuzwa sidhani kama kuna m2 atasimama kugoma sasa.
 
poleni sana haya ila kinachongaza wakati mpo mnasoma sekondari mlikuwa mnategemea pia boom....kwenye nauli na kula poleni sana students of tanzania
 
Mimi ni mmojawapo kati ya watu tunaoteseka kwa hilo. Mpaka sasa nipo home tu, nikiwahi kuja nitakula nini? Nitalala wapi? Bora nijipange, nikawa sawa ndio nije.
 
Mimi ni mmojawapo kati ya watu tunaoteseka kwa hilo. Mpaka sasa nipo home tu, nikiwahi kuja nitakula nini? Nitalala wapi? Bora nijipange, nikawa sawa ndio nije.

kwa hyo na wewe huna hata nauli sio?
 
na hapo tumbo bado linahitaji ndio na nyie mkipewa kitengo cha mikopo msiwe na roho hizo hatutaendelea..
 
Poleni saaaana. Lakini kwa upande mwingine huu uzembe ni kutokuwa na liquid funds sirikali. Sasa mnaposoma na kuhitimu kumbukeni kuwa hizo shida zina wakabili wanafunzi wooote isipokuwa watoto wa matajiri na mafisadi.

Usije nawe ukawa fisadi.
 
Nimetoka pishana na msafala wa makamu wa raisi nkawa nahesabu idadi ya magari aliyoongozana nayo si chini ya kumi.
Moyoni nkawaza tungekuwa na serikali makini tungefanya cost saving apa ie including mafuta,idadi ya magari.
Kuweni wavumilivu JK soon ataenda USA maana hii ya UK haijaleta kitu zaidi ya kukubali wasomali washitakiwe Tz nduguze Al Shababy
 
Ngoja niendelee kuchunga ng'ombe boom likitoka nitakwenda maana maisha ya Dar bila Boom unaweza olewa mwanaume
 
Back
Top Bottom