Na huu ndio ukokotozi wa bei ya mafuta ya petroli kwa lita 1

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Kwema Wakuu,

Hivi Karibuni bei ya Mafuta imepanda kwa Takriban TZS 100 kwa lita kulinganisha na bei iliyokuwepo awali. Wengi wamejiuliza kwanini Mafuta haya yanauzwa Rahisi nchi za jirani kama Zambia wakati yanapita hapa hapa kwetu hivyo katika nchi hizo yangekua bei ghali zaidi.

Hapa chini ni mchanganuo wa bei ya Mafuta ya Petrol kwa Tanzania. CIF-DSM Price inaweza kua sawa ila kuanzia hapo kila serikali inaamua nini iongeze kwenye hiyo bei ndiomaana zinatofautiana.

Kuanzia 1-19 ni gharama zinazohusu Makampuni ya Mafuta. Na kuanzia 20 ni Wenye vituo vya mafuta

1625678586027.png
 
Kwema Wakuu,

Hivi Karibuni bei ya Mafuta imepanda kwa Takriban TZS 100 kwa lita kulinganisha na bei iliyokuwepo awali. Wengi wamejiuliza kwanini Mafuta haya yanauzwa Rahisi nchi za jirani kama Zambia wakati yanapita hapa hapa kwetu hivyo katika nchi hizo yangekua bei ghali zaidi. Hapa chini ni mchanganuo wa bei ya Mafuta ya Petrol kwa Tanzania. CIF-DSM Price inaweza kua sawa ila kuanzia hapo kila serikali inaamua nini iongeze kwenye hiyo bei ndiomaana zinatofautiana.


View attachment 1845132
Kudadadeki msururu wa makodi
 
Namba 18 na 21 imejirudia.
A4 imejaa tozo za bidhaa moja. Kudadeki! Hatoki mtu.
Kumbe ndio maana bei ya mafuta Zambia na Malawi ni nafuu Sana.
 
Namba 18 na 21 imejirudia.
A4 imejaa tozo za bidhaa moja. Kudadeki! Hatoki mtu.
Kumbe ndio maana bei ya mafuta Zambia na Malawi ni nafuu Sana.
Nimeongezea hii,

Kuanzia 1-19 ni gharama zinazohusu Makampuni ya Mafuta. Na kuanzia 20 ni Wenye vituo vya mafuta
 
Kuna kemikali zinawekwa kwenye mafuta yanayotumika nchini. Sasa ukisema mafuta yanaenda nje ya nchi Kisha ukayatumia hapa nchini kinyemela yatakua hayana hizi kemikali.
Anaetengeneza hizo kemikali hana tofauti na aliyepewa kazi ya kuchapisha noti, maana akizalisha nyingi kuliko tuliyomuagiza na kisha akaiuza kwa wafanyabiashara wa mafuta inakuwaje? Na tutajuaje hilo halifanyiki?
 
Vinasaba una maanisha kemikali maalum au DNA ya viumbe hai?
DNA inayoongelewa hapa sio DNA za viumbe hai unazozifahamu mkuu.
Kwa, lugha ya malaika wanaviita Molecular Fuel marker.
Kwa Tanzania nimeona wanatumia sana "dyes" (rangi maalumu)

Mafuta huwa yakiingia tu yakishalipa kodi pale bandarini serikali inayawekea dyes, rangi. Then ndio yanaruhusiwa kuanza kuuzwa kwenye vituo. Mara nyingi kiwango kinachowekwa huwa ni 3ppm+/-7.

Mafuta ambayo hayajalipiwa kodi yakipimwa hayatonyesha hiyo 3 lakn pia hayatakua na hiyo rangi.

Mafuta ambayo yamechakachuliwa yakipimwa hayataonyesha hiyo standard. Inaweza kuwa zaidi ya 3 au chini ya Tatu depending na kampaundi zilizoongezwa kwenye hayo mafuta ili yachakachuliwe. Mfano molecule za mafuta ya condensate zikiongezewa kwenye petroli

Mafuta ambayo yameingizwa kimagendo kutoka nchi za jirani pia yakipimwa hayataonyesha uwepo wa hiyo marker lkn pia hayataonesha rangi hiyo.

Na hizi chemikali ziko highly controled zaidi ya unavyoweza kufikiri.
 
Back
Top Bottom