Na hizi ndio sababu kwanini nimepunguza trip za kwenda Kanisani

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Mwanzo kidogo mwa mwaka 2012 kushuka chini huko nilikuwa sikosi kwenda kanisani jumapili ata kwa dawa maybe labda niwe naumwa na homa yenyewe iwe ile ya kulazwa ndio naweza nisiende,

Ibada ilikuwa ibada kweli kweli, kwanza ukianzia kwa muongozaji wa misa(padre)anavyoiongoza misa na jinsi anavyolichambua somo kwa mifano ukirudi kwa wanakwaya wanavyoimba nyimbo zao zinavyoeleweka kanisa zima mnakaa mnaimba na kusali kwa furaha kabisa utafikiri ile siku ya Yesu kristo kurudi imewadia,

Siku hizi sasa kwa nini nimepunguza trip za kwenda kanisani ni kwa hizi sababu,

--siku hizi ukienda kwenye ibada unakutana na muongozaji wa misa(padre) hana mudi ya kusalisha katikati ya kuhubiri (maana siku hizi wanafail sana kuchambua somo) lazima ataweka na maneno ya kutoa fungu la kumi,

--ukija kwenye kwaya sasa kila siku wanaimba nyimbo mpya nyimbo zenyewe zinavyovutwa sasa alafu zinavyopokelewa kila sauti toka ya kwanza mpaka nne wanaimba kipande tofauti wanaenda kukutana mwishoniii utasikiaa tu Aleluyaaaaaa, ata hujui uimbe kipande kipi uache kipi yaani haunjoi ule mziki unabaki kugugumia tu,
Siku hizi hadi ile bwana utuhurumie wanaimba kwa mbwe mbwe hatari yaani dakika tatu nzima ni yenyewe tu na wakati ina vimstari vitatu tu unavyovutwa sasa aiseee, (bwana hutuhurumie, kristo utuhurumie, bwana utuhurumie)

--ukija kwenye sadaka sasa siku hizi ziko kuanzia mbili na kuendelea,

--matangazo yanachukua muda mrefu kuliko ata misa yenyewe na hii ndio aswaa inaniboa sanaaa,

Zipo sababu nyingine lakini hizi ni main kwangu zinazonifanya nipunguze trip za kwenda kanisani.

CC Zero IQ
 
Axee hapo kwa matangazo umeguza penyew,huwa hata nashangaa kuna haja gan ya kuweka mbao za matangazo wkt yanasomwa ndani,hilo la michango pia halijakaa sawaa kwan kila kukicha kunatafutwa njia mbadala ya kukusanya michango bila kuangalia na vipato vya waumini
 
Maybe labda?
Mm sisemi uwongo siendagi kanisani kabisa. Labda itokee nasimamia harusi ndo nafikaga huko
Mana nmelichunguza kanisa kwa undani mpaka naona uivivu kwenda jinsi lilivyo na maswali yasiyojibika

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe achakwenda kanisani. Mabwana utawapatia bar na kwenye vigodoro na ndoa utaisikia kwa wenzio. Umeongea kabisa kwa kujiamini kwamba huna habari na Mungu?
Na huyo anaekupa usimamizi wa Harrusi sijui anashetani gani kichwani.
 
Back
Top Bottom