Na hili nalo linasubiri Rais aseme? Kunyanyasa wenye maduka siku ya Jumamosi

Lugeye

JF-Expert Member
Apr 18, 2011
1,679
2,914
Kwa kweli tumekua watu wa ajabu sana ,viongozi wote tumemuachia magufuli afikiri juu yetu

Kuna utaratibu wa ajabu Sana kuwa siku ya jumamosi utakuta maduka asubuhi yamefungwa mpaka saa nne eti sababu ni usafi na ukifungua unakamatwa faini 50000,

Kwanini serikali isiwaruhusu watu wafungue then waendelee kutoa huduma mtu anaweza kumpa kijana hela aendelee kufanya usafi eneo lake wakati yeye akiendelea na biashara,

Dodoma ndo imekua kero maduka yote yamefungwa na ajabu hakuna anaefanya usafi so watu wanasubiri tu mda ufike afungue , serikali nashauri iruhusu mtu aendelee kufanya biashara na wakati usafi ukiendelea kwanza mtatoa ajira ya vijana wengi maana kijana atapewa 3000 au zaid ya kufanya usafi huku tajiri akiendelea kufanya biashara kuliko kulazimisha kufunga duka na usafi haufanyiki,
 
sio tu dodoma ni TZ yote kwa ujumla hakuna anaefanya usafi ule ambao serikali ilivyosema wanasubiri sa4 wafungue biashara
 
Haya ni matokeo ya mifumo ya kikomunisti/kijamaa. Mawazo yote na kufikiri kote anaachiwa mwenyekititi wa chama. Huko china wamepitisha na sheria wataanza kuwafundisha watoto wao mawazo ya raisi wao Xi Jinping, pia mawazo hayo yanakua sehemu ya katiba. Magufuri anavinasaba vya kikomunisti/kidikteta na ndio maana wasaidizi wake wote hawatumii vichwa vyao bali wanangojea kutekeleza kauli/mawazo ya magufuri. Ni mifumo flani ya kipumbavu sana
 
Hakuna mechanism ya kuenforce hilo agizo, watu wanalala zao ikifika saa nne wanafungua

Wengine wanaweza kufanya usafi toka ijumaa jioni/usiku

Wengine wanaweza kufanya usafi within one hour wameshamaliza sasa sijui kwa nini wangoje hadi saa nne

Wengine wanaweza kufungua biashara huku vijana wakiendelea na kazi za usafi nje

I don't know kwa nini tujiwekee limit ya kufanya kazi badala ya kuhimiza kazi na usafi viende sambamba!
 
nilifikiri ingekuwa vizuri kama ingeamriwa kwamba ukikutwa una eneo chafu unachukuliwa hatua, wengine wangeamka saa kumi ili wafungue biashara saa kumi na mbili, hapa maisha yanasimama kwa takribani masaa sita! (assumption tunaanza shughuli saa kumi na mbili)
 
Mimi sio mwanasiasa
Lakini ktk mambo yanauzi mojawapo ni hili
Pili lipo suala la kunywa pombe kabla ya saa Kumi jioni
Pombe ni halali kisheria na unaponunua unalipa kodi za Nchi
Jiulize serikali inapoteza mapato kiasi gani?
 
Kwa hili Heshima na Taadhima niwaombe Viongozi wetu kua nzia Mtaa Kijiji Kata Tarafa Wilaya Mkoa Ngazi ya Taifa Walitafakari Zoezi hili la Usafi linaendeshwa Vipi?Katika Utafiti niliyoufanya na kuongea na Watu wengi ni Kama Sasa hivi watu ikifika JUMAMOSI ni kama vile ni kigezo cha watu kulala sana na kuchelewa kuamka Wakichukulia UONGOZI umetoa Ruksa maalum ya kuchelewesha Watu kuendelea na shughuli zao za Uzalishaji Mali TUTAFAKARI Ili nia na Azma ya Mh.Rais itekelezwe vema na kutoa matokeo Chanya
 
Kwa kweli hii ni kero kubwa sana. Unakuta sehemu unayotakiwa kufanya usafi ni kiasi cha dk 15 unakuwa umemaliza, lkn unatakiwa kufunga duka mpaka saa nne. Kwa nini hao wanaokagua kama duka limefungwa au limefunguliwa kabla ya saa nne wasipite kuangalia eneo chafu ndiyo wawatoze faini ili waache watu wafanye biashara na wateja wapate huduma. Hii imekua ni kero isiyo na tija kabisa. Serikali itafakari jambo hili kwa kweli
 
ilitakiwa jumamosi iwe siku ya kukagua usafi kwa hiyo mtu atafanya usafi kwa wakati wake, unakuta mtu anauza chai unamwambia afungue saa nne muda huo nani atakuja kunywa tena chai pia wafanyabiashara wanatozwa pesa za usafi halafu unawazuia wasifungue kwa ajili ya usafi kwani leseni zimefafanua muda wa kufanya usafi au watu tu kwa kupenda sifa wanajiamlia
 
hata nyama mteja ukanunue saa nne. Mimi Nina hakika wanajua wamekosea. Ila wanaona shida Ku admit ingawa inagharimu taifa.
 
Uchumi umesinyaa, mauzo kwenye biashara zetu yamepungua kwa asilimia takribani 60. Hivi tunalazimika kulipa kodi ya mapato, Leseni ya biashara, Fire Extiqusher, Tozo za kuzoa taka, kodi ya chumba cha biashara pia kuna kodi ya municipal ambayo hatuijui hata maana yake. Sasa unapunguziwa muda wa kufanya biashara hizo pesa za kulipa hayo yote utazipataje? Hapo hujapata mahitaji muhimu ya maisha yako. KERO KUBWA.
 
Back
Top Bottom