Na hili limetushinda kwa miaka yoote 51 ya uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na hili limetushinda kwa miaka yoote 51 ya uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Sep 17, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu leo 17/09/2012 nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya kutoka itv saa 2.00 usiku. Kuna taarifa moja iliyokuwa inaelezea jinsi mbuga yetu ya serengeti ilivyobarikiwa wanyama wengisana (simba 3000, fisi 7500, nyumbu takribani 5000 na nk ambayo ni idadi kubwa sana isiyoweza patikana katika nchi yoyote ile duniani), na pia ikawa inaeleza kuwa katika watalii woote 800,000 wanaoingia nchini kwetu kila mwaka , mbuga hii hutembelewa na watalii wapatao 500,000.

  Mjadala wangu uanaanzia hapa, kwa kuangalia sehemu moja tu ya utalii na nikalinganisha na tatizo dogo tu la ukosefu wa madawati katika shule zetu za msingi (zaidi) na sekondari.Nikachulia matharani hao watalii 500,000 tu wa mwaka mmoja kila mmoja alipe kiingilio cha tsh 50,000 tu kuingia mbuga hii ukizidisha hapo utapata (watalii 500,000 x tsh 50,000/= 25,000,000,000/= mapato ya mwaka mmoja tu).

  Nikajiuliza hivi gharama ya kutengeneza dawati mmoja tu ni shillingi ngapi, nikasema matharani iwe 50,000/= nikajiuliza tena je kwasasa tuna jumla ya watoto wangapi waliopo shule zetu za misingi nchi nzima nikasema iwe 500,000 (mtanisamehe kama ni takwimu ndogo)kwa hiyo gharama ya kutengeneza madawati 500,000 ya watoto wetu woote wa shule ya msingi itakuwa 500,000/= x 50,000 wanafunzi =25,000,000,000/= (ambayo ni sawa na mapato ya mwaka mmoja tu ya mbuga mmoja tu ya serengeti iliyotembelewa na watalii 500,000).

  Je imekuwaje hadi leo tunazaidi ya miaka 50 hata nusu ya tatizo hili hatujalimaza, je ni kweli tunakimbizana kuendelea kama wengine??? kama wenzetu wako dunia ya kwanza na sisi bado tuko dunia ya tatu (tena ni nchi ya 3 kwa kuombaomba baada ya afrighanstan na iraq)

  Je ni lini tutafika huko katika listi ya dunia ya kwanza???

  Je tunamikakati gani ya kufikia hukokaribuni ndugu zangu kwa majadiliano, mataniwia radhi kwa mahali popote nilipo kosea takwimu, lakini lengo langu ni kuonyesha ni kwa vipi kama tuna fursa kama hii lakini hatuzitumii kutatua matatizo yetu ikiwa tuna kila kitu leo tz ni ya 3 barani africa kwa ku export nje dhahabu, tunakila kitu achilia mbali gesi, na makaa ya mawe na kadhalika.

  JK aliwahi kusema hata yeye hajui kwanini tz ni maskini lakini hapa leo muda huu katika kipindi cha dk 45 ITV Mzee malecela anasema chanzo kikubwa cha umaskini wa tz ni ukosefu wa mtaji,,,, karibuni
   
 2. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Committed ako ni kamfano kadogo ka UTAJIRI wa nchi hii (Kumbukla mkulu aliulizwa kwa nini bongo ni masikini akasema hajui!!)
  Tatizo kubwa linalotukabili ni VIPAUMBELE. Enzi zake Mwl JKN (RIP) alikuwa akisisitiza kuwa 'kupanga ni kuchagua'.
  asilimia 75 ya mapato kama hayo ndio yanaendesha serikali kubwa na matumizi amabyo yangeweza kubanwa. Kwa mfano, mashangingi ya bei mbaya kuanzia serikali kuu hadi za mitaa (yana kiu ya mafuta ambayo ni lazima tuyanunue kwa pesa za kigeni, utunzaji wake ni mkubwa pamoja na ufisadi unaombatana nayo) - serikali ni kubwa, vyeo visivyo na faida yo yote ila kutafuna pesa hizo hizo - kwa mfano ma-RC na ma-DC wana faida gani katika maendeleo ya nchi? Lakini ndivyo tulivyochagua. Nimewahi kukutana na mtu mmoja kutoka nje ya nchi na ndo alikuwa ametoka kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro - kwa hakika alikuwa anaeleza kwa uchungu kwa nini watoto wa shule za msingi wilayani humo wanakaa sakafuni katika eneo ambalo limejaaliwa utajiri. Kwa hivyo, hata watalii wenyewe wanatushangaa lakini ndivyo tulivyochagua. Kupanga ni kuchagua.
   
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hapa duniani kuna watu wavivu wa kufikiri kweli, yani mnakaa kulaumu serikali kwa jambo la kawaida ambalo hata wanakijiji wakilidhamiria wanaweza kulifanikisha. Tuwe wepesi wa kufikiri tunayochangia kuliko kujaza post zisizo na mantiki.

  Swala la kusema heti mapato ya utalii yatengeneze madawati ni jambo la kushangaza kweli, nchi ina deficity ya budget kila mwaka, vyanzo vya mapato ni vichache kulinganisha na mahitaji halisi ya wananchi.

  Kuna huduma nyingi za msingi ambazo serikali inabidi izifanikishe za dharura kwa kuzipa kipaumbele, huduma kama afya, maji safi na salama, ulinzi na usalama, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ili kusisimua uwekezaji uliopo na uwekezaji mpya, kwa lengo la kuongeza ajira kwa wananchi, kutoa huduma ya elimu sanasana ya kuwaanda kwa kuwapa mafunzo stahili wataalamu katika sekta mbalimbali, sana sana serikali iwape motisha wanafunzi wanaochukua masomo ya ualimu na sayansi ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa taaluma hizo.

  Serikali inapaswa kulisimamia swala la kilimo kwa kuandaa mbinu za makusudi kabisa za kuwasaidia wakulima wazalishe kwa gharama ya chini na kuwawezesha kupata ziada ambayo itasaidia kuuza nje na kuchangia taifa kimapato. Hapa itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira, serikali inapaswa kusaidia wakulima kuacha kutegema zana za kale badala yake iwawezeshe zana za kisasa kama matrekta, wakulima waache kutegemea mvua bali waanze kutumia kilimo cha umwagiliaji. Hapa serikali isaidie sana.

  Hayo yote yanahitaji kutengewa fedha za kutosha hili yatekelezwe na kufanikishwa kama ilivyokusudiwa. Jukumu la kusomesha, kulisha na kuangalia maadili ya watoto wetu ni yakwetu wazazi hama walezi, serikali ilifuta ada shule za msingi na kupunguza ada katika shule za sekondari na zile za boarding ndio kama ada ya kutupa kabisa, wazazi wanashindwa kuchangia kwa hali na mali ujenzi wa madawati? Lawama gani hizi tunatoa kwa serikali? Yapo ya kulalamika sio madawati jamani.

  Swala la hizo nafasi mnazosema hazina maana ni kutokana na upeo tu mdogo, lengo hapa ni kupata ajira ili watanzania waweze kujitegemea katika maisha,

  kwa hali hii itafika hatua mtu unaachana na demu wako utaanza kuilaumu serikali.
   
 4. m

  muchetz JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Message nzuri. Ni me quote na ku-edit kurahisisha usomaji kwa wengine.
   
 5. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu mpendwa, viongozi wa nchi hii wanawaza ni jinsi gani watatumia kila pato linaloingia kwenda kubembea nchi za nje, kuyashangaa mananasi, mihogo, ng'ombe za wenzao huku watoto wetu wakiketi kwenye mawe bila hata mwalimu wa kuwaongoza. Tumeishia kuwa Tanzania feck. Kodi yenyewe inayookotwa inatumika kutulipua kama wanyama. Jua kwa hakika hii nchi inahitaji mabadiliko ya hali ya juu. Cha maana tuombe Mungu hii damu inayomwagwa isipotee bure bali ilete hayo mabadiliko na tupate viongozi wenye uchungu na nchi hii na ambao wataona kwa macho yao taabu ambazo zinatusonga na ambazo zingaliweza kuwa solved very simply. Mungu ibariki Tanzania!
   
 6. m

  muchetz JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Nawe ni kama majebere, zomba e.t.c. Ngumu sana kuwaelewa? Watu wanaweza kuwa wanazungumzia kalamu nyie mnaanza kuzungumzia meza. Anyway pole pole labda tutafika. Tuombe mungu gamba lisiwe gumu sana.
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Serikali inatoa misamaha ya kodi ya bilioni ngapi kwa mwaka?

  Kodi inazokusanya inazifanyia nini?

  Wale wawekezaji katika migodi wanatupa 97% au 3%?

  Je mikataba mibovu ndio vipaumbele?

  Magari ya kifahari ya wabunge na watendaji wa serikali ndio kipaumbele?

  Inaonekana na wewe HAMY huelewi kwa nini nchi ni maskini wala huelewi kwa nini nchi ina budjet deficit.

  Kama unaelewa,tuelimishe na sisi vipi nchi atatua tatizo la hiyo budjet deficit na vipi Tz itaacha kuwa maskini.
   
 8. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Tukifikia hatua hii ya kufanya majadiliano kwa ustaharabu bila kuweka vikomo vya sentensi zetu kwa kutumia matusi, kiukweli jamvi hili linastahili kuwa la Great Thinkers.

  Nirudi kwenye swali lako la msingi, ni jinsi gani serikali itaweza kuondokana na tatizo la bajeti finyu? hapa wote tunafahamu njia kuu ya serikali kujipatia mapato ni kutokana na kukusanya kodi.

  kodi hizo zinatokana na mishahara wanayolipwa wafanyakazi/watumishi na kodi zinazotozwa kwenye bidhaa. Pia kuna mapato ambayo serikali inayapata ambayo kimsingi hayatokani na kodi(non taxable revenue), misaada kutoka nchi tajiri na mikopo kutoka benki za ndani na nje.

  Namna ya pekee ya serikali kuongeza wigo wa kodi ni kwa kutambua vyanzo vipya vya kodi, kama vile kuzitambua sekta zisizo rasmi, ambapo kuna vijana wengi wamejiajiri (sina takwimu sahihi), kuanza kutoza kodi katika mauziano ya nyumba na zile nyumba zinazopangishwa. Hapa kwenye nyumba serikali inapoteza mapato mengi sana maana hii kwa hapa mjini imekuwa ni biashara kubwa na yenye faida kwa wamiliki, maana akishalipa land rent na property tax aguswi wakati anatengeneza millions of money katika ardhi ambayo kimsingi ni ya serikali. Hapa pia mashirika yote ya umma kuanzia NHC, NSSF, PPF, NDC, LAPF na mengine mengi yaliyowekeza katika real estate yatoze kodi ya soko na waachane na ule ujamaa ya kwamba yameundwa kutoa huduma kwa umma, kumbe behind the scene kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.

  Lakini pia hata mamlaka ya mapato inapaswa kuweka mbinu ambazo zitaziba kabisa mianya ya ukwepaji wa kodi ili isitofautiane na makadirio ya serikali katika ukusanyaji wa mapato.

  Swala la misamaha ya kodi kama litafanywa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria sidhani kama linatatizo. Maana ni kivutio cha uwekezaji, after all wanatengeneza ajira nyingi bila kusahau wanachangamsha uchumi na soko kuwa na ufanisi zaidi.

  Swala la nidhamu katika matumizi ya mali za umma inabidi lizingatiwe na kutiliwa mkazo, kwa kuachana na matumizi yasiyo ya lazima maana ukweli ni kwamba taifa letu bado halijafikia hatua ya kuwa na vingozi wa kufanya hanasa, hapa siungi mkono manunuzi ya hayo mashangingi kabisa na manunuzi mengine yeyote yanayo litia mzigo taifa. Hapa naomba tusiwe biased kwa serikali tu, hata vyama pinzani hapa wamefeli katika swala la luxury.

  Swala la kutokomeza umaskini, ningependa tusiliongelee kwa sasa maana ni mapema mno, bali tunaweza kuupunguza kwa kiasi fulani kama hayo niyoyaeleza kwenye thread yangu ya mwanzo yatashughulikiwa.Tuwe na imani na serikali yetu.
   
 9. M

  Maseto JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Ujumbe wa mfano wako ni mzuri.lakin tatizo liko kwenye takwimu za wanafunzi.kwa mfano,kesho wanafunz karibu 900,000 wa darasa la saba tu wanafanya mitihani.Tukuchulie wastan kila darasa wako kiasi hiki.kwa hiyo tunaongelea wanafunzi wa shule za msingi pekee Tanzania karibu 7,000,000.
   
 10. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kitu kimoja na pekee ambacho kinanifanya nisiweze kuisamehe CCM ni kuporomoka kwa elimu hapa nchini! Elimu ndio mkombozi wa masikini na kila mtu.

  Bora watu wasile vizuri, wasipite kwenye barabara nzuri ila wapate elimu nzuri. Kuporomoka kwa elimu ni dhambi kubwa ambayo watawala wetu wa CCM wameifanyia nchi hii na vizazi kadhaa vilivyoikosa hiyo elimu. kwa rasilimali zetu tunaweza kabisa kuwa na elimu bora tena bila ya kuathiri ulaji wao watawala
  .
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Umetaja tatizo moja tu la madawati.

  Nchi inahitaji ilipe madeni nje, ilipe mishahara walimu, mishahara madaktari , wanajeshi, Polisi na watumishi wengine. Pia tunazo barabara nyingi hazina lami, vijiji havina umeme na maji, ofisi za serikali zimechoka, mahospitali hayana madawa,watoto chini ya mwaka mmoja wanahitaji chanjo, mashule hayana maabara, mito haina madaraja wala vivuko.

  Ukitaka kufanya tathmini nzuri weka mapato yoote na matumizi yoote halafu ndio useme mbona haya hayafanyiki na pesa zipo.
   
 12. commited

  commited JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  asante kwa hiyo takwimu mkuu Maseto lakini unadhani hili tatizo kwa miaka yoote 51 y uhuru tuliyonayo bado linapaswa kuwepo mpaka leo??
   
 13. commited

  commited JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umetaja tatizo moja tu la madawati.Nchi inahitaji ilipe madeni nje, ilipe mishahara walimu, mishahara madaktari , wanajeshi, Polisi na watumishi wengine.

  Pia tunazo barabara nyingi hazina lami, vijiji havina umeme na maji, ofisi za serikali zimechoka,hospitali zinaukosefu wa dawa,watoto chini ya mwaka mmoja wanahitaji chanjo,shule hazina maabara, mito haina madaraja wala vivuko.

  Ukitaka kufanya tathmini nzuri weka mapato yote na matumizi yote halafu ndio useme mbona haya hayafanyiki na pesa zipo.
   
 14. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,126
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Mnazungumzia mapato ya Serengeti, Ngorongoro nk? Kwani hamjui yanakwenda wapi? Waangalie maboss na waajiriwa wa hizo mamlaka za utalii walivyo mabilionea! Serikali haiambulii kitu.
   
 15. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 836
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  matatizo ya Tanzania ni mfumo Kristo ndio maana chi haiendelei
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  HAMY
  Haya uliyoyatolea darasa katika mchango wako ndiyo ambayo serikali inapaswa iyafanye. Usahihi zaidi ni kuwa ilipasa serikali iwe imeyafanya hayo zamani tu. Miaka 51 imepita, kama hutaki 51, tuchukue 15 tu. Tunajua kuwa imeshindwa kufanya hayo uliyayaeleza. Kwa hiyo hoja ya msingi ya mleta mada ni sahihi. Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake.

  Tunacheza na elimu, tunacheza na sekta ya elimu.
  Kwa mantiki ya hoja nikubaliane na wewe, kuwa wanakijiji wanaweza kutoa vikalio,madawati lakini serikali kwa miaka 51 imefanya nini la maana? Na hasa ukilinganisha na majirani zetu?
   
 17. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kati ya hayo uliyosema, lipi serikali ya ccm limetekeleza 100%?
   
Loading...