IBRAHIM NGOGO
Member
- Sep 19, 2012
- 16
- 8
*TUJITADHIMINI UPYA KAMA TUNASLAHILI KUITWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI*
Unajua wanaCCM hawawezi kusema Chochote juu ya hizo kauli za rais zenye kila dalili za UCHOCHEZI na UZANDIKI kwa Watanzania? CHADEMA inatakiwa itoe MATAMKO kwa kila mamlaka inayosimamia uchaguzi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshatoa maagizo yake kwa Wakurugenzi na mamlaka nyingine za kusimamia uchaguzi na ameziagiza kuhakikisha CCM inashinda kwa mamlaka hizo kumtangaza mgombea wa CCM hata kama hajashinda.
CHADEMA isisubiri hadi wakati wa uchaguzi ndipo malalamiko yaanze kusema tumeibiwa au kuporwa ushindi. Anzeni sasa kudeal na mamlaka za usimamizi wa Uchaguzi kuanzia Kitongoji/Mtaa, Kijiji, Kata, Jimbo, hadi Taifa.
Tangazeni mgogoro na uwe mzito kweli ili rais aanze kuonja joto ya jiwe kwa kauli zake hizo zinazomega taifa na kuleta taharuki kubwa miongoni mwa jamii zetu.
Iwe mwisho kulalamika, nasema kulalamika sasa iwe mwisho, tuanze mapambano kabla ya wao hawajajipanga. Kama ni UCHOCHEZI wameanza wao ngoja tuwaunge mkono kwa kujibu mapigo.
Maisha haya na matamko haya tayari yanaaishiria kifo cha kimwili na Kidemokrasia, sasa mnangoja mfe kwanza ndipo muanze kutoa matamko?
Natamani ningekuwa kiongozi wa Chama kanda au mkoa au wilaya. Nadhani nisingechukua hata masaa 24 ningekuwa nimeshawapanga watu wangu na kutoa waraka mzito unaotekelezeka.
Nina hasira inayonipelekea hata kuugua! Unajua kuna watu wanaotutazama kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, wanatupima na kututathimini na mwishowe wanagundua, Hatujui nguvu yetu na wala hatujui mamlaka tuliyonayo. Kuna wakati wanaCCM wanatamani kuwa sisi lakini wanashindwa kwa sababu ya mfumo kandamizi kwenye chama chao.
Tunatakiwa tulipuke kama moto wa Petrol, tuwe na nguvu kama bulldoza, tuvimbe kama tairi iliyojazwa upepo, tuwe na msimamo kama wa akina Tundu Lisu na akina Besiege wa Uganda.
Siasa Africa hasa Tanzania kwa sasa zinahitaji mtu wa kuanza na kusimamia haki kwa nguvu zote. CCM walianza Kupiga marufuku bunge LIVE tukanyamaza kimya, wakapiga marufuku mikutano ya siasa ambayo ipo kikatiba tukanyamaza kimya, wamepiga marufuku kutembeleana na kusalimiana na ndugu zetu waliopo CCM bado tunataka kunyamaza tena, hapo hapo wametangaza kuwa mgombea yoyote wa CCM akishinda tu kwenye kura za maoni basi ameshashinda UCHAGUZI hapo tunataka kunyamza!!
Came on Guys hivi unataka wakunyang'anye mke au mume mbele ya macho yako ndipo uanze kufight? Au wambake mwanao mbele yako ndipo utangaze mapambano? Tumekuwa wazembe mno aiseee, yaani wazembe sana!
Nani yupo tayari, nani hataki kuona haya yakiendelea? Nani anataka mabadiliko na yeye mwenyewe amebadilika na yupo tayari kuchukua hatua? Nani atakuwa wa kwanza kama mimi kuanza kwa kuhakikisha tunaacha kulalamika bali tunaanza vitendo?
Tuwasiliane haraka!
Ahadi Mtweve
0764660220
Mbeya