N/Waziri Kigwangalla: Kuanzia sasa lazima kila mwananchi awe na Bima ya Afya

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86

Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Khamis Kigwangala amesisitiza kuwa kuanzia sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kuwa na Bima ya afya,huku akiwatoa hofu wananchi wasio na uwezo kwamba serikali kupitia Sera ya taifa ya afya ya mwaka 2007, itakuwa tayari kugharamia matibabu ya makundi maalumu ya kijamii wakiwemo wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, watoto chini ya umri wa miaka mitano na watu wenye magonjwa ya kudumu.

Naibu Waziri kigwangala, ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya miaka 50 ya utume wa injili kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza yaliyofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba, yakiwa yametanguliwa na zoezi la utoaji wa huduma za afya bure kwa wakazi hilo zilizofanywa na madaktari bingwa wa macho,meno,kibofu cha mkojo,tezi dume,kisukari na saratani ya shingo ya kizazi kwa siku saba mfululizo.

Sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza mnamo mwaka 1935,lililopo chini ya jimbo la Nyanza Kusini,ambalo hadi sasa limefikisha makanisa 84 pia zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.Angelina Mabula, ambaye amesema kazi kubwa ya kanisa ni kuendelea kuokoa maisha ya waumini wake kiafya na kiroho pamoja na kusimamia maadili mema ndani ya jamii.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato tanzania Dk.Godwin Lekundayo, ameiomba serikali kuharakisha usajili wa hospitali ya Pasiansi inayojengwa na kanisa hilo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa muda uliopangwa, lengo la kanisa la SDA jimbo la Nyanza Kusini ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za matibabu ya rufaa ili kuokoa maisha ya watu.
 
...
Kaizari anataka apelekewe vitu vyake.
Mpeni Kaizari yaliyo ya Kaizari. Kaizari anaitaka kila shilingi anayoipata mdanganyika.

Changa la macho hilo kwa wadanganyika wasio na uwezo wa kulipa kodi (bima ya afya) siri-kali itawalipia au "itawajaza mapesa" ili wajitumbuwe wenyewe.

Ni rahisi kuwahadaa kondoo milioni 44 kuliko kuwadanganya wadanganyika.

Elimu bure, Bima ya afya bure, sukari bure, Ajira bure, kutumbuliwa bure!

Nchi yetu imegeuka kutoka "maisha bora" kwa kila mdanganyika na kuwa pepo ya dunia katika kipindi kifupi. Bwana asifiwe!

Nchi hii kwa miaka 50 ilihitaji mtu mmoja tu muhimu, dakitali wa kuombewa dua na kutumbua majipu.
 
Magufuli ni chaguo la Mungu.

........ watanyooka tu
Mungu yule anayelipisha kodi unapotumia hewa yake?
Au Mungu yule aliyeipa ardhi ya wadanganyika rasilimali na mali ghafi za kuwafanya waishi "maisha bora"?
Wadanganyika watanyooka tu. Huku Kitaa wanatafutana , wamepigika mbele kwa mbele.

Kodi ya miamala ni 18%. Na ile kodi ya kuku, mbuzi na baskeli ikianzishwa kama Mbunge anayependa kondoo zake, Ally Kessy alipendekeza itakuwa 28%.

Wadanganyika wanainajisi nchi kwa ukondoo lakini wanataka waishi kama maisha ya "malaika"?
Watumbuliwe tu!
 
Kaizari anataka apelekewe vitu vyake.
Mpeni Kaizari yaliyo ya Kaizari. Kaizari anaitaka kila shilingi anayoipata mdanganyika.

Changa la macho hilo kwa wadanganyika wasio na uwezo wa kulipa kodi (bima ya afya) siri-kali itawalipia au "itawajaza mapesa" ili wajitumbuwe wenyewe.

Ni rahisi kuwahadaa kondoo milioni 44 kuliko kuwadanganya wadanganyika.

Elimu bure, Bima ya afya bure, sukari bure, Ajira bure, kutumbuliwa bure!

Nchi yetu imegeuka kutoka "maisha bora" kwa kila mdanganyika na kuwa pepo ya dunia katika kipindi kifupi. Bwana asifiwe!

Nchi hii kwa miaka 50 ilihitaji mtu mmoja tu muhimu, dakitali wa kuombewa dua na kutumbua majipu.

WELL SAID DEAR
 
Kuwa na bima ya afya sidhani kama itakuwa tatizo kubwa hembu tuangalie upande wa pili hizo hospitali na vituo vya afya vina hali gani? Nadhani humu ndio pange fanyiwa marekebisho kwanza dawa vifaa majengo ukarabati vitanda wauguzi wakutosha na wenye vigezo alafu ndio tuje kweny mpango madhubuti wa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Ni wazo tu
 
Huyo naibu waziri anaota ndoto za mchana asilimia kubwa ya...wa Tanzania wanashindia mlo mmoja kwa siku,wanaishi chini ya $ 1 kwa siku....leo hii waweze ku afford kulipia health insurance! Huo ni upunguani...mwingine.kwanza health care ya Tanzania is very poor ndio maana wao viongozi wanakimbilia..india, South Africa na UK kwa matibabu..hebu Aachen. Kuwahadaa...wa Tanzania
 
Kuwa na bima ya afya sidhani kama itakuwa tatizo kubwa hembu tuangalie upande wa pili hizo hospitali na vituo vya afya vina hali gani? Nadhani humu ndio pange fanyiwa marekebisho kwanza dawa vifaa majengo ukarabati vitanda wauguzi wakutosha na wenye vigezo alafu ndio tuje kweny mpango madhubuti wa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Ni wazo tu
Lakini jamani sio kila kitu tulaumu serikali,nafikiri jukumu la kujenga Hospital na vituo vya afya ni la wote sio serikali tuu,itabidi watanzania tuache kuwa malazy na kuanza kuchukua mikopo kujenga hizo Hospital then kuziendesha kwa ufanisi wa hali ya juu na kama kweli bima sio issue itakuwa ni biashara nzuri sana maana malipo yako yatatoka kwenye insurance companies moja kwa moja
 
Wazo lako pia sioni kama ni baya mkuu ila vipi swala la hizo zilizopo hivi sasa achilia mbali kuanzisha vipya kwanini wasi boreshe kwanza koz kama ww ni Mtanzania hali ya watanzania walio wengi kiuchumi unajuwa itachukua mda na process ndefu kuanzisha vipya wakati zoezi la kuhakikisha tu wote wa mepata bima ya afya ni shughuli pevu
 
Hivi mnataka vituo vya afya vichomwe moto...
Pamoja ni idadi ndogo ya wenye bima sasa bado wanakosa madawa itakuwaje kila mtanzania akiwa na bimA??
 
  • Thanks
Reactions: 999
Unakatwa ada ya bima ya Afya, ukienda hospitalini wanakuandikia prescription ukanunue madawa dukani...

Hizi ngonjera za kujifanya hii ni serikali ya superman bila kutatua kwanza changamoto za msingi itakuja kujikuta siku za usoni haina majibu kwa maswali ya wananchi!
 
Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Khamis Kigwangala amesisitiza kuwa kuanzia sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kuwa na Bima ya afya,huku akiwatoa hofu wananchi wasio na uwezo kwamba serikali kupitia Sera ya taifa ya afya ya mwaka 2007, itakuwa tayari kugharamia matibabu ya makundi maalumu ya kijamii wakiwemo wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, watoto chini ya umri wa miaka mitano na watu wenye magonjwa ya kudumu.

Naibu Waziri kigwangala, ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya miaka 50 ya utume wa injili kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza yaliyofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba, yakiwa yametanguliwa na zoezi la utoaji wa huduma za afya bure kwa wakazi hilo zilizofanywa na madaktari bingwa wa macho,meno,kibofu cha mkojo,tezi dume,kisukari na saratani ya shingo ya kizazi kwa siku saba mfululizo.

Sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza mnamo mwaka 1935,lililopo chini ya jimbo la Nyanza Kusini,ambalo hadi sasa limefikisha makanisa 84 pia zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.Angelina Mabula, ambaye amesema kazi kubwa ya kanisa ni kuendelea kuokoa maisha ya waumini wake kiafya na kiroho pamoja na kusimamia maadili mema ndani ya jamii.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato tanzania Dk.Godwin Lekundayo, ameiomba serikali kuharakisha usajili wa hospitali ya Pasiansi inayojengwa na kanisa hilo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa muda uliopangwa, lengo la kanisa la SDA jimbo la Nyanza Kusini ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za matibabu ya rufaa ili kuokoa maisha ya watu.
Hama wazeee mmeshindwa kuwahudumia mtaweza watoto na maskini? Wasio na uwezo
 
  • Thanks
Reactions: 999
Hii cabinet ya Magufuli ina comedian wengi sana ,nimeanza kuamini zile semina elekezi zilikuwa zinasaidia kidogo ingawaje ni gharama ningeomba zirudishwe ili kuficha hizi aibu
Ni kweli huu jamaa kama simwelewi vizuri hayuko realistic hata kidogo
 
siwezi kulipia bima ya afya wakati sina uhakika wa kupata huduma zinazostahili, naona kila waziri anataka asifike anavyokusanya mapato badala ya kufanya kazi kwa ufanisi
Kulipia out of pocket itakuwa ni very expensive ....kama unaweza kulipia toyo yako bima kwa nini ushindwe kulipia mwili wako?
 
Back
Top Bottom