N lini Azam dish mtaaonyesha local chanel bila ya malipo ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
kwa muda wa kama wiki moja sasa,kampuni ya ving'amuzi ya azama (siyo azam tv) kuanza kuonyesha local chanel kwa gharama badala ya bure kama ilivyokuwa imeelezwa mwanzo na serikali wakati tukitoka katika analogia kwenda digital.
mpaka sasa ni jambo la ajabu kupata television moja ya ndani kati ya zile tano (ambayo ni tbc peke yake ndio ipo hewani)huku chanel ten,itv,star tv na eatv zikiwa zimekatwa na huku chanel nyingi za nje zikiwa zimeachwa hewani na kuzimwa zile za ndani tu.
najua labda tcra walitoa majibu lakini wengi bado hatujaridhika na majibu hayo kulingana na hata serikali yenyewe haikosema badae kuwa watanzania watakuja kulipia local chanel zao.
pia tunajiuliza kwanini azam wapandishe bei ya vifurushi vyao na kuzima chanel za local ?
kingine ambacho kimetukosesha majibu ni kwanini chanel za nje kuachwa bila ya kulipiwa au ni mpangi wa mtanzania kupata habari za nje kuliko za ndani ?


siyo kwamba watanzania tunapenda vya bure ,la,kwani haya hayo madishi na matv hatukugaiwa wala huo umeme hatupati bure bure bali kwa jasho lenye maumivu
pia ndivyo serikali ilivyotuambia kuwa chanel za ndani zitapatikana bure
je ni lini zitarejea au ndio hivyo tulishaingizwa katika mfumo wa kumgharamisha mtanzania.
majibu ya TCRA yaliridhisha ?
au huu ndio mfumo wa upatikanai habari kwa mtanzania ?
 
azam ovyo sana yani wameona waachie tbc tu . tunalazimishwa kuangalia channels ambazo hatuzipendi...
 
Back
Top Bottom