Mzunguko wa Ulaji mema ya nchi unakatisha tamaa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,018
114,363
Tanzania ingekuwa gari basi mimi kama abiria ningeshashuka kitambo na kuwaacha peke yenu

Inaudhi na kukatisha tamaa sana,teuzi kubwa kubwa za kula vizuri bila bugudha mema ya nchi zinaenda kwa watu walewale kila siku.

Huku ni kujilimbikizia ulaji,ina maana mnataka mfie kwenye vyeo?

Siku mbili hizi nimewasikia Mama Blandina Nyoni kalamba cheo,jamani huyu mama amekuwa katibu mkuu na bosi maofisi mangapi?Hazina kapita,Ukaguzi kapita,Wizara ya Afya sijui TRA koooote huko kala nchi vizuri,daaaah ina maana wengine siye hatuna midomo ya kula vizuri?

Haya leo Mama Salma Kikwete,huyu kala miaka 10 kama mwanamke namba moja wa Bongo.Alichokuwa anakula mzee maarufu vyote kala. Tena wanavyopendana hawa usikute amekula vingi kuliko hata JK mwenyewe.Lakini kapewa tena ulaji.

Kina Mama Anne Makinda bado wameng'ang'anizwa kuendelea kula kule NHIF.

Orodha ni ndefu,sasa nyie mnaogawa ulaji,mnafikiria nini kuhusu sisi wengine?Mbona walaji ni walewale tu.....Halafu kama ndiyo utaratibu wa Chama mkumbukeni basi na Mzee Wassira
 
Back
Top Bottom