Mzunguko wa pesa umekwama hapa

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Ngombe asiyelishwa anatoaje Maziwa?

Kuna kilio cha muda mrefu cha wazabuni mbalimbali wa serikalini kuanzia Halmashauri,Manispaa,Wizara,Taasisi na Idara za umma kutokulipwa malipo yao stahiki kwa huduma walizotoa ama bidhaa walizosambaza
Hali ilikuwa mbaya zaidi miaka michache iliyopita ambapo tender zilitolewa na walioshinda na kutoa huduma wamekuwa wakipata malipo kiduchu na wengine kutokulipwa kabisa.
Malipo yamekuwa yakitoka si kwa umuhimu wa huduma tena bali ni kwa kujuana na kwa vimemo vya wakubwa.
Cha kushangaza zaidi malipo yamekuwa yakifanyika kwa wazabuni ambao hawajatimiza huduma kamili na mfano mkubwa ni hili suala liloloibuliwa majuzi kuwa jeshi la polisi walimlioa mzabuni asilimia 99 kwa huduma isyofikia hata robo ama ile ya mabehewa ya TRL yaliolipiwa malipo yote kabla hayajaletwa
Ikumbukwe kupata uzabuni ni mtihani mzito kwani kampuni husika lazima iwe na ohysical office ikaguliwe ikiwa ni pamoja na nyaraka na leaeni zote hai za kuifanya ikidhi vigezo
Kutimiza hayo yote ni gharama kubwa na mtaji nje ya huduma yenyewe
Kuoanga ifisi au duka ama ghala la bidhaa, kulipia leseni zote,gharama za umeme, mafuta, ulinzi na mishahara
Pia gharama za bidhaa iwe ni kzalisha hapa nchini ama kuimport na kulipia kodi zote na gharama za clearing ama iwe ni gharama za manunuzi yote ni mzigo kwa mnunuzi pekee
Taratibu za serikali ni kutoa huduma kwanza then malipo hapo ndipo sinema yenyewe huanza.Mara bado kidogo, sijui hatujapata OC mara vile ili mradi tu hao jamaa wamehitimu ujuzi wa visingizio
Hawa wazabuni ndio walipao kodi za biashara zao na nyingine kama Import duty, excise duty, VAT, levy na fees mbalimbali pia stamp duty na withholding tax kwenye mikataba yao ya hapo hujawajumuisha watu wa Fire,OSHA,Jiji nk pamoja na bill za maji na umeme
Sasa pamoja na hayo yote mzabuni anacheleweshewa malipo ama jalipwi kabisa je atajimudu vipi kujiendesha na kila siku landlord wake yupo mlangoni ama maafisa wa TRA pia wanadai kodi zao kwa bidhaa ama huduma amanazo hazijalipwa
Je huyu mfanhabiashara atalipa hizo operation cost na nini?
Je atalipa kodi na nini?
Na je hizo huduma ataendelea kutoa kutika wapi?
Kuna wazabuni wa mahospitali, mashule, majeshi nk hivi hawa wakisimama kabisa wagonjwa, wanafunzi na askari wetu makambini watakula nini?
Kia siku tunasikia TRA wamevuka lengo la makusanyo sasa hizo pesa wanazokusanya zinapelekwa wapi
Bora bata makandarasi wana mikataba yenye vifungu vya riba kila anapocbeleweshewa malipo lakini kwa mzabuni wa kawaida ni invoive zake na LPO ama delivery notes tu na kama anadai laki tano toka 2012 hata akilipwa baada ya miaka 5 atalipwa biyohiyo laki tano japo kuwa itakuwa baina ile thamani yake kwa wakati huo
Jenga picha huyu mzabuni alikopa kwenye taasisi za kifedha akitegemea kurejesha baada ya kulipwa si atakuwa ameingia migogoro na kesi nyingine ama kupoteza mali na dhamana zake?
Kwa malalamiko haya naisihi hii serikali ya awamu ya tano iliyoonyesha nia ya dhati kuwakwamua wananchi wake toka kwenye lindi la umasikini basi ijitahidi kuwalipa wazabuni wake ili nao walipe kodi na kuendesha familia zao vinhinevyo biashara nyingi zitakufa taratibu
Nasema hivyo maana kwenye ripoti tuluyoiona ya mwezi machi hatujaona malipa kwa wazabuni wa ndani
Hawa wakilipwa mzunguko wa fedha utarejea na kunyamazisha vilio vya wengi kuwa hamna pesa kwenye mzunguko wa maisha
 
kweli kabisa mkuu, wazabuni wa ndni hawathaminiwi kabisa yaani mtu anatoa huduma malipo hayajulikani yatatoka lini. Mkuu wa nchi kama kweli anapaswa kuwaangalia na hawa wazabuni wa ndani kwa jicho la tatu make hawa wakilipwa kwa wakati hakika mzunguko wa pesa utakuwa mzuri. Juzi nimesikia wazabuni wa nyanda za juu kusini wakitishia kugoma kutoa huduma kwa kile kinachoonekana kupewa bei elekezai isiyo kuwa na tija kabisa, eti wa supply sukari kwa bei elekezi ya 1800/= kwa kilo, wakati wao sukari wananunua kwa bei juu ya hiyo wakati huo huo malipo hayajulikani lini wanalipwa. Kweli inasikitisha sana
 
Serikali zote duniani zinawalipa au hata kuwakopesha wananchi wake ili wafanikiwe. Serikali yetu kazi yake ni kuua wananchi wajasiriamali. Hili ni swala la muda mrefu sana.
 
Serikali zote duniani zinawalipa au hata kuwakopesha wananchi wake ili wafanikiwe. Serikali yetu kazi yake ni kuua wananchi wajasiriamali. Hili ni swala la muda mrefu sana.

Sijui huu uzi wataweza kuusoma maana hali ni tete huku mtaani, hakuna chapaa kabisaa na wao ndo wamezishikilia, hawalipi kwa muda husika ni balaa tupu!
 
Wamelimbikiza madeni mengi mno mpaka wanashindwa pa kuanzia
 
Sijui huu uzi wataweza kuusoma maana hali ni tete huku mtaani, hakuna chapaa kabisaa na wao ndo wamezishikilia, hawalipi kwa muda husika ni balaa tupu!
Wanausoma tu shida ipo kwenye utekelezaji wake
Kwa kweli wananchi wanaumia
 
Serikali zote duniani zinawalipa au hata kuwakopesha wananchi wake ili wafanikiwe. Serikali yetu kazi yake ni kuua wananchi wajasiriamali. Hili ni swala la muda mrefu sana.
Yaani hapa Tanzania ni kinyume.wakiona wana deni kubwa kwa supplier mmoja wanamhama kuanza na mwingine mpya ambaye kwa kutokujua ya wenzie atajiina amebahatika kuwa mzabuni mpya lakini kumbe ni Mkopwaji mpya
 
Sijui huu uzi wataweza kuusoma maana hali ni tete huku mtaani, hakuna chapaa kabisaa na wao ndo wamezishikilia, hawalipi kwa muda husika ni balaa tupu!
Kila wizara,idara,taasisi na halmashauri ni madeni tu
 
Back
Top Bottom