Mzunguko wa Maisha

BenElohimy

Senior Member
Sep 21, 2021
181
222
Watu walio kwenye maisha yako, watakaokuja kwenye maisha yako ni wa ajabu sana tena sana usipokuwa makini ni ngumu kwenda mbele

Unashangaa kabisa rafiki anakwambia mtu fulani aweza kukusaidia katika mambo ya maisha yako yakaenda mbele.

Lakini cha kushangaza aliyekwambia huyo mtu aweza kukusaidia ndiye huyohuyo baadae anakwambia huyo mtu ni mhuni

Hivi jamani kama unakuwa na maisha ya kuzungukana je unadhani kuna kufika au kwenda mbele zaidi ya hapo ulipo??

Kuna watu katika maisha ukiwa unapitia magumu wanakuwa wa kwanza kukwambia pole jamani, Mungu ni mwema utaenda mbele, lakini unapoanza kuchanua kama mwelezi ndiyo hao hao baadaye wanakupinga.

Kuwa makini na ambao unawaita marafiki zako, waweza kukufanya usiende kwenye maisha yako yale ambayo unawish.

Hakika ruhusu Mungu aingilie kati ya maisha yako, utashinda.
 
Back
Top Bottom