Mzunguko uliopo hospitali ya Bugando unatisha

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Kwa wagonjwa au ndugu wanaopeleka wagonjwa wao Bugando wanataabika sana wanapofika kwa matibabu pale Bugando. Mgonjwa akifika saa mbili asubuhi anaweza kuzunguka mpaka saa kumi hajapata huduma yeyote.

Tupo kwenye ulimwengu wa mtandao kwanini msitengenze njia ya kisayansi ambapo jina la mgonjwa likiisha ingizwa kwenye kompyuta basi hana haja ya mzunguko. Mfano hai ni pale Kituo cha Afya cha KKKT(Nyakato) wanatibu wagonjwa kisayansi. Jina lako likiishaingizwa kwenye kompyuta, Waganga wanaotibu wanakuwa na mawasiliano kimtandao.

Mgonjwa anapofika anaelekezwa sehemu ya kwenda na anachukua muda mchache sana. Mfano pale Bugando mgonjwa ukiwa kipofu ndiyo taabu ya mwaka. Utaaambiwa nenda pale, nenda ghorofa ya tatu, teremka ghorofa ya kwanza n.k.

Sisi wagonjwa tunawaomba sana punguzeni MZUNGUKO ULE WA KUTISHA. Tengenezeni Software ya kitabibu ili wagonjwa watibiwe kwa muda mfupi.
 
Una ushauri mzuri mkuu. Hii tabia ya kuzungushana nenda pale nenda pale huwa inachosha sana. Bila shaka wataboresha
 
Itakuwa wana matatizo na huduma kwa mteja... Ni vizur wakaboresha customer service kama ilivyo kwa ccbrt
 
Hospital ziongezwe pia... hospital kubwa zilizopo tz ni zile zile zilizojengwa wakati wa Nyerere... muhimbili, bugando , kcmc.... wakati watz tulikuwa chini ya 15m.... sasa tuko 50m hamna hospital za maana zilizo jengwa... wanajenga vituo vya afya tu.... awamu 4 tangu baba wa taifa wapo tu kazi kufuja pesa kununua viitu visivo na maana... bugando pia imeelemewa japo ushauri wako ni mzuri mkuu.... kama nyerere aliweza kwa resources ndogo za wakati ule hawa
wanashindwa nn???
 
Back
Top Bottom