Mzungu na mkewe watupwa jela miaka 30 kwa kulima bangi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,554
44,725
Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imewahukumu kifungo cha miaka 30 gerezani washtakiwa Damian Krzysztof raia wa Poland na mke wake Eliwaza Pyuza Mtanzania kwa makosa ya kulima mimea 729 ya bangi na kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha kilogramu 17.2 kinyume cha sheria.

Vilevile, Mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani au kulipa faini ya shilingi milioni nne kila mmoja washtakiwa Eliwaza Raphael Pyuza, Hanif Kanani raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi na Boniface Kessy Mtanzania, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Katika kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Florence Khambi ameeleza kuwa hukumu hiyo imetolewa leo Aprili 9, 2021mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Bernazitha Maziku wa Mahakama hiyo baada ya ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo kuthibitisha kwamba, washtakiwa wanajihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Sambamba na hukumu hiyo, Mahakama imetoa amri ya kutaifishwa kwa shamba hekari moja na nusu lililopo eneo la Himo njia panda, fedha taslim shilingi 26,765,000 alizokamatwa nazo Damian, Madiaba mawili yaliyokutwa na bangi, na pikipiki aina ya KTM Adventure yenye namba za usajili MC 972 AAD.

Pia Mahakama imeamuru kuteketezwa kwa simtank mbili za lita 2000 zilizokuwa zikitumika kumwagilia miche ya bangi kwenye shamba eneo la Himo na kiasi chote cha bangi kilichokamatwa.

Katika shauri hilo, upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali Ignas Mwinuka, Verdiana Mlenzana na Lilian Kowero huku Upande wa utetezi uliongozwa na wakili wa kujitegemea FaiyGrace Sadala ambae aliwatetea Damian, Eliwaza na Hanif huku mstakiwa wa nne Boniface Kessy akijitetea pekeyake.

Washtakiwa, walikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) tarehe 08 mwezi Februari 2020 eneo la njia panda ya Himo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, na kufunguliwa kesi ya jinai namba 79 ya mwaka 2020.

Washtakiwa wametiwa hatiani na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya Mwaka 2015 kama ilivyorejewa Mwaka 2019.
 
Kumekucha!!! Siku hiz wavuta bange tumekaliwa koon daa!

Yaan Bangi ya buku!! (3misokoto)

Mnanipeleka jela miaka minne.

Serious!!!
 
Yaani kukutwa na bangi siku hizi imekuwa sawa na ubakaji? Hizi sheria zetu sijui zikoje, na hawa mahakimu wanavyozitafsiri napata mashaka nao sana.
 
Hivi kulima mmea wa bangi ni kosa?

Mimi nilidhani kosa ni kuvuta au kuuza bangi ya kuvuta?
 
Serikali bhana ikikuta bangi shambani mwako hiyo ni Mali yako ila ikikuta madini ni Mali ya Serikali.

Hii bhangi ihalarishwe ili ishuke thamani.
 
Vitu kama Bange na Mirungi iondolewe jinai yake ni kuoneana Mbona watu wanapiga mamilioni na hawafungwi
 
Kuna watu wamekamatwa jana Uwanja wa Nyereere

Alafu maajabu..Mwanamke ndie ametajwa kwa majina.


Alafu mwanaume..et Jina limehifadhiwa????


Nani huyu Kigogo mpaka Jina lake lifichwe lkn la mwanamke litajwe??


Tutamkumbuka Jiwe
 
Back
Top Bottom